Wednesday, October 21, 2015

NCHINI TANGANYIKA GOODLUCK JONATHAN ALIYEKUWA RAIS WA NIGERIA ASEMA UKAWA NA CCM USHINDANI WAO NI MKALI


Goodluck Jonathan  Akiri  Ushindani  Ni  Mkali  Kati  Ya  UKAWA na CCM
Mkuu wa Jopo la Waangalizi kutoka Jumuiya ya Madola na aliyekuwa Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amekiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu nchini Tanganyika na nchini Zanzibar una ushindani mkali kutokana na namna vyama vilivyojiandaa lakini akawataka wagombea wote wa nafasi za urais kujiandaa kukubali matokeo kwa maslahi mapana ya taifa lao kwa ujumla.

Wagombea wanaochuana kwa karibu ni, Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Lowassa kwa upanda wa umoja wa UKAWA wa vyama vilivyo ungana.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam nchi Tanganyika mara baada ya kuwasili nchini, Jonathan aliyekubali kuondoka madarakani Mei mwaka huu na kumpisha Muhammad Buhari baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu nchini mwake huko Nigeria, alisema katika uchaguzi wowote kuna kushinda na kushindwa na hivyo wagombea wajiandae kwa matokeo yoyote ili kuiacha nchi yao ikiwa salama.

Alisema ijapokuwa ushindani ni mkali, Jumuiya ya Madola inaamini kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki na kwamba imani yao kubwa ni Zanzibar na Tanganyika kusimamia demokrasia iliyokuwapo wakati wote tangu Tanganyika ipatre uhuru wake mwaka 1961 na nchi ya Zanzibar pia. jonathan anaongeza jopo lenye waangalizi 14 kutoka mataifa mbalimbali yaliyo wanachama wa Jumuiya ya Madola.
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment