Viongozi waandamizi wa UKAWA wamesema hawayatambui matokeo ya Urais yanayoendelea kutangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi NEC kwa madai kuwa yamehujumiwa. Kauli hizo za kutoyatambua matokeo zimetolewa na Freeman Mbowe,Profesa Safari na James Mbatia wakati wakiongea na vyombo vya habari leo kuhusiana na mwenendo wa uchaguzi mkuu. Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe amesema serikali ya CCM imeamua kuwatumia wakurugenzi,NEC na jeshi la polisi kupindua maamuzi ya wananchi na kuamua kutangaza matokeo ya uongo. Mbowe ametumia muda mwingi kulilaumu jeshi la polisi kuwakamata Ma IT wa Chadema waliokamatwa wakijumlisha matokeo ya Lowassa jijini Dar es Saalam, huku professa Safari akieleza jinsi NEC ilivyochakachua matokeo....
"Nimesikitishwa na taarifa za kukamatwa kwa vijana wenzetu Wataalamu Wenzangu wa IT waliokuwa katika vituo vya majumuisho ya kura za mgombea Urais UKAWA."Huu ni UONEVU dhahiri kabisa. Inauma zaidi kwa wao kunyimwa kabisa dhamana.Hii si HAKI."Sitaki kuamini tumefikia hapa,sitaki kuamini uonevu wa kiasi hiki unatendeka kwa manufaa ya kisiasa." Amesema Mbowe
Katika tamko lake, Profesa Safari ametolea mfano jimbo la tandahimba ambapo amesema, kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na NEC katika jimbo hilo,Magufuli amepewa kura 49,098 huku Lowassa akiambulia 46,288
Kwa mujibu wa Profesa Safari, matokeo halisi waliyoyakusanya toka kwa mawakala wao yanaonyesha kuwa Magufuli ana kura 44,253 huku Lowassa akiwa na kura 44,537
Kwa upande wake Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia amesema NEC watachakachua matokeo lakini sio hisia za wananchi.
Viongozi hao wa UKAWA wamesema kesho Oktoba 28 watakutana kwa dharura na kutoa msimamo wao kwa wananchi juu ya mwenendo wa uchuguzi mkuu
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
No comments:
Post a Comment