Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na viongozi wa dini ya Kikristo waliopo Zanzibar katika kituo cha utengamano kilichopo Welezo
Nchini Zanzibar. Mgombea urais wa chama cha wananchi CUF, Zanzibar chini ya mwamvuli wa Ukawa, Maalim Seif Shariff Hamad amesema amewataka Shein na Balozi Ally Idd kuhakikisha wanadhibiti vurugu zinazoweza kutokea katika uchaguzi mkuu ujao la sivyo watapelekwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC). Maalim Seif Shariff Hamad alisema hayo, katika viwanja vya Fumba, jimbo la Dimani mkoa wa Mjini Magharibi wakati akihutubia mkutano wa kampeni jana. Alisema kumekuwa na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani ikiwamo kusambaza sare za CUF ambazo vijana wa CCM, wamekuwa wakizutumia kufanya vurugu. Alisema kitendo hicho kinaifanya CUF kuonekana kama mashabiki wake, ndiyo wanaofanya vurugu jambo ambalo siyo sahihi.
Maalim Seif Shariff Hamad alisema mbinu zote zinazofanywa na CCM, yeye na viongozi wenzake wa chama cha CUF wanazitambua na kuwa wamekuwa wakizipata baada ya muda mfupi. Aliwataka wananchi na wanachama wa chama hicho, kukichagua chama chake ili kipate nafasi ya kuongoza katika kipindi kijacho cha miaka mitano. “Katiba iliyopitishwa na CCM inayo mambo ambayo yanakisaidia chama hicho na ikiwa nitaingia madarakani mchakato huo utaanza upya ili kuweka mambo yatakayowafaa Wazanzibari na siyo CCM peke yao.” Naibu wa katibu mkuu wa CUF nchini Zanzibar, Nassor Mazrui alisema kuwa wakati umefika kwa Wazanzibari kuichagua CUF kwa madai kuwa tangu CCM iongoze, maendeleo yalisimama. Alisema Wazanzibari wanaotaka maendeleo kamili wawashawishi wenzao, kuipigia kura CUF ili wasiendelee kuburuzwa na Serikali ya Muungano.
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
No comments:
Post a Comment