Tuesday, October 27, 2015

NCHINI ZANZIBAR MASKANI YA KISONGE YAWASHUTUMU VIKALI VIONGOZI WAKE WA JUU WA CCM KWAKUSABABISHA CCM KUSHINDWA UCHAGUZI MWAKA HUU 2015 WATAKA WAFUKUZWA WOTE MARA MOJA


MASKANI YA KISONGE YAWATUHUMU SANA VIONGOZI WOTE WA JUU WA CCM KWA KUSHINDWA UCHAGUZI WAMTAKA SHEIN AWATIMUWE WOTE VIONGOZI WA JUU WALIOSABABISHA CCM KUSHINDWA UCHAGUZI MWAKA HUU 2015
KISONGE WATAKA CCM YAO WAMTAKA DR. SHEIN KUTIMUA “RIGHT HAND MAN” WAKE KWAMBA NI MAMLUKI WAMEIGHARIMU CCM KUSHINDWA

Maskani kaka na makada wahafidhina wa CCM wametaka na wanawatuhumu mamluki ndani ya CCM na kutokuwajibika kama sababu ya CCM kushindwa na kumtaka Dr Shein kama makamo Mwenyekiti wa CCM kuwaweka pembeni. Duru za siasa za kihafidhina ndani ya CCM zikishadidiwa na maskani kaka ya kisonge wanamtaka Dr. Sheni sasa kuwatema rasmi Mohamed Aboud na Omari Yussuf Mzee kwa madai kuwa ni mamluki wa CUF na hawana uchungu na CCM kwani hawana jimbo na wala hawagombei lakini Dr. Sheni anawakumbatia na kukigharimu Chama cha Mapinduzi.Makada hao wa mrengu wa kihafidhina ndani ya CCM wanamtaka Dr Shein kuchagua “Great Thinkers” wa CCM ambao wana damu ya Kiafro Shirazi sio akina Mohamed Aboud na Omar Yussuf Mzee ambao hawana uchungu na CCM, maana kama kweli ni CCM ngangari wangetafuta majimbo ya kugombea badala yake wanasimama nyuma ya Dr Shein na kumuhujumu yeye na CCM. sasa wakati umefika waondoke.
Aidha makada hao wametupa lawama kali kwa Balozi Seif Ali Idd kwamba pamoja na kuwa na mamlaka makubwa kiserikalini ameshindwa kabisa kuiwezesha CCM kushinda na kurejea kushindwa kwake kumpatia Amani Karume ushindi wa kishindo mwaka 2000 akiwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM ambapo alitimuliwa na Karume aliposhika wadhifa wa makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar na kumteua Ramadhan Feruzi. Kisonge wanadai Balozi Seif hana mbinu za kushinda siasa za kiushindani ingawa hawana mashaka na U-CCM wake, aidha wametaka pia Dr Shein kuachana na makada wengine maarufu wakitajwa kuwa ni Pandu Ameir Kificho aliyekuwa spika wa baraza la wawakilishi, haji Omar Kheri na Ramadhani Abdallah Shaaban kuwa ni mzigo mkubwa kwa CCM na hawawezi kuisaidia CCM kuimarika kwani wapo kwa maslahi yao tu na si kwa maslahi ya CCM, na kwamba sasa umefika wakati kwa Dr Shein kutowakumbatia wachumia Matumbo yao na kutaka apate “Great Thinkers” watakao imarisha CCM kwa kutokana na damu ya Afro Shirazi na pia wenye uwezo kitaaluma na kimkakati kwani Kificho, Shaaban na Kheri wamechoka kiakili,kifikra na hawana elimu, na kwamba kwa sasa CCM inahitaji wasomi sio kuongozwa na vichwa mchungwa buru matari zero kichwani.
Aidha Ali Vuai Naibu katibu Mkuu wa CCM hakuachwa katika lawama za kushindwa kwa CCM katika uchaguzi huu kwamba hakuwa makini kuhakikisha maslahi ya CCM yametimizwa kabla ya zoezi la uchaguzi kuanza na sasa kutoa visingizio visivyo mashiko wala havina kichwa wala miguu amekuwa mbabaifuu akidai mawakala wa CCM hawakutambuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wakati, hali ya kuwa siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika alikuwa na mkutano na waandishi wa habari kuelezea tathmini ya maandalizi ya CCM kuelekea uchaguzi, ni kwa nini hakuliona hilo wanadai Kisonge. Na kumtaka aachie ngazi mara moja aachie ngazi mara moja tunasema tena hafai, ili CCM ipate waliotayari kuifanyia kazi CCM kwa moyo wote na sio kuzembea na kutoa visingizio.
Kisonge wamedai historia ya CCM itawaandika vibaya akima Mohamed Aboud, Omar Yusuf Mzee, Pandu Ameir Kificho, Ramadhan Abdallah Shaabani na Haji Omar Kheri kwamba walichangia kuiangamiza CCM kutoka katika medani ya siasa za ushindani, na kuwataka waondoke, na kwamba hawako tayari kuona CCM ikitoweka kama ilivyo kwa KANU ya nchi ya Kenya na ZANU ya nchi ya Zambia.
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment