Sijashangaa kabisa
By Farell Jnr. Foum ( Kureish Wa Zanzibar)
By Farell Jnr. Foum ( Kureish Wa Zanzibar)
Against all odds.. tume yao.. mahakama zao.. polisi.. jeshi.. na mabilion ya pesa..jeuri.. kibri.. matusi.. uhasama.. visasi na yote yanafanyika kwa sababu moja tu wanamabadiliko wasishinde. Lakini against all odds tumeshinda.. tena kwa ushahidi na tutashinda tena kwa ushahidi hata tukirejea uchaguzi kesho. Hilo halina mjadala, nchi imebadilika njia pekee kwa watawala kubaki ni kufuta mfumo wa vyama vingi na kurudi kule kwa kudumu kwa fikra za Mwenyekiti.
Tazama vizingiti tulivyovuka, kuanzia ZanID, daftari, vipigo vya wavaa masoksi, unyanyasaji, ukatwaji wa majimbo kwa upendeleo, utumiwaji wa vikosi kwa sababu tu ya uchaguzi na hata kule kujinata kwa goli la mkono lakini bado tumeshinda.
Tazama namna ya ujanja mkubwa wa kuzima demokrasia ulivyoshindwa kunyanyuka. Kuanzia watoto wadogo walioingizwa katika daftari kinyume na sheria, maiti zilizoachwa katika daftari, na kuandikishwa kwa wageni wasiostahiki kuwamo katika daftari. Na jee tume ilifanya nini ilipopewa malalamiko na wanamabadiliko? Wakaona bado hawajaridhika, wakakata tena mipaka kwenye daftari kiasi kwamba nyumba moja ya mume na mke wamefanywa kuwa wapiga kura wa shehia tafauti. Na Mwenyekiti wa Tume alikuwa mtetezi mkubwa wa zoezi la wazi kabisa la upendeleo.
Tazama namna ya ujanja mkubwa wa kuzima demokrasia ulivyoshindwa kunyanyuka. Kuanzia watoto wadogo walioingizwa katika daftari kinyume na sheria, maiti zilizoachwa katika daftari, na kuandikishwa kwa wageni wasiostahiki kuwamo katika daftari. Na jee tume ilifanya nini ilipopewa malalamiko na wanamabadiliko? Wakaona bado hawajaridhika, wakakata tena mipaka kwenye daftari kiasi kwamba nyumba moja ya mume na mke wamefanywa kuwa wapiga kura wa shehia tafauti. Na Mwenyekiti wa Tume alikuwa mtetezi mkubwa wa zoezi la wazi kabisa la upendeleo.
Wazanzibari wamenena kwa pamoja kwamba hawako tayari kuendelea na siasa za maji taka, ubabe na kuwaita mabwege. Majimbo tisa Unguja yanaanguka kutoka mikononi.mwa watawala katika sehemu ambazo hazikufikiriwa huko nyuma. Nungwi, Kijini (Mkwajuni) na Bumbwini zote katika kaskazini ya unguja kwa pamoja wanakataa siasa zisizo na maslahi yao. Mwanakwerekwe, mpendae, mto pepo, kipange nazo pia zikatoweka huku Malindi iliopelekwa hadi Makadara, gulioni na miti ulaya nayo bado ikabaki katika himaya ya wanamadiliko.
Chukwani ndio kabisa na mizengwe yote ya uhasama uliojengewa hata mazingira ya kuzigawa familia zilizokuwa kioo cha umoja, ukatwaji wa mipaka ya ajabu kabisa na kufutwa kwa majina ya watu wa shehia moja kwa sababu tu ya kumkomoa mtu mmoja bado wananchi waliowengi wakakataa kuendekeza siasa za utoto na ugomvi wa kuviziana. Tazama namna gani binaadam hawezi kushinda kudra ya Mungu, maana shehia tatu katika nne, mgombea wetu alikuwa nyuma kwa kura kuanzia shakani, kisauni na hata chukwani kwenyewe. Lakini wakasahau kwamba shehia ya tomondo ilikuwa na wapiga kura zaidi ya 3000 na miongoni mwao watu 1936 wakasimama na mabadiliko na hivyo jitihada zote za binaadamu zikashindikana kwa vile qudra ya Mungu haipingiki matokeo yake wanamabadiliko wa chukwani wakashinda kwa kura 72 zaidi.
Rehma ya Mungu haipingiki kwa nguvu za mwanaadamu na qadar yake si ya kucheza nayo. Tupime mantik pana zaidi kwamba chaguzi hizi zilizofanyika ambako wanalalamika ati Pemba kumeibiwa kura lakini wakazikubali kura zile zile za ubunge na Rais wa Muungano zilizopigwa siku moja, sehemu moja na katika mazingira yale yale walioyaita si ya haki na huru. Kweli inaingia akilini?
Wanazidi kulikoroga na kwa ubishi tu watalinywa hata kama magae kwa kisingizio tu cha Mapinduzi na ati mgombea mmoja ana dhambi zisizofutika wakibeba utukufu wa uungu tena wa kukataa hata lile Mwenyezi Mungu alilolipigia kelele la kwamba ni mwingi wa maghfira. Laiti wangelijitazama wenyewe na dhambi walizotenda nyuma halafu wakapima tena mantik ya utukufu wanaojipa wakiamini kabisa katika maghfira ya Mwenyezi Mungu lakini wakawanyoshea wengine kwamba maghfira hazitafika huko wangeliweza kurudi nyuma na kupima uzandiki wanaoueneza.
Tuwacheni tupumue na mkubali uzandiki wa upemba na uunguja hauna nafasi tena katika kizazi cha sasa. Dhambi ya kibri, chuki na siasa za hasama zitaendelea kuwatafuna na kuwakosesha kukubalika na wananchi waliowengi. Tumefuta uchaguzi kwa hoja dhaifu tena kinyume kabisa na katiba inayotuongoza na hata mantik mapana ya uono wa mwanaadamu. Wazanzibari wako tayari wakati wowote kwa wingi wao kuwakata tena hata ikiwa mtarudia uchaguzi mara 100 hamtashinda kwa chaguzi huru na za uwazi. Ile dhana ya goli la mkono au bandua bandika kwa sasa imepitwa na wakati na kamwe hamutatuita tena mabwege wa kuendelea kuibiwa kura.
Kaeni chini mutafakari kwamba kuna makubwa zaidi yanayohitajika kuendelezwa kuliko siasa za ubishi wa kitoto wa kushindwa ukatia mpira kwapani na kuondoka nao. Nchi yetu sote, turudi kwenye wema na kukubali uongozi wa kupokezana. Mtu mwenye elimu pevu ya utafiti wa maradhi na tiba kwa jamii leo anajisahau kiasi kwamba heshima yake anahiari ipotee kwa kung’ang’ania madaraka ambayo hayana ridhaa ya wananchi. Tulichagua matarajio mwaka 2010 hatukuchagua mfalme wa miaka 10.
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
No comments:
Post a Comment