Thursday, October 15, 2015

NCHINI TANGANYIKA BALOZI MWAPACHU ARUDISHA RASMI KADI YA CHAMA CHA CCM NA KUTANGAZA KUJIUNGA NA UKAWA



Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kada wa CCM, Balozi Juma Mwapachu leo amerudisha kadi ya uanachama katika ofisi za CCM Kata ya Mikocheni jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika. Amesema anajiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kwamba baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 atatangaza chama anachojiunga miongoni mwa Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD vinavyounda umoja huo.

Mwapachu amesema haoni sababu ya kutaja chama hicho sasa kwa vile lililo muhimu kwao hivi sasa ni umoja miongoni mwa wanamabadiliko na kujipambanua katika imani ya chama cha siasa hakuwezi kuwa na tija kwa umoja huo.Amesema Lowassa anakwenda kuwa Rais wa Wanaukawa wote, hivyo watu wote wanaoamini katika mabadiliko ndani ya vyama hivyo wanapaswa kuwa wamoja kwa kuuwezesha umoja huo kuibuka na ushindi.

Jumanne wiki hii, Balozi Mwapachu alitangaza kujitoa CCM akikituhumu kukiuka misingi ya kidemokrasia wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais Julai mwaka huu ambapo Dk John Magufuli alichaguliwa huku mgombea anayeamini kuwa na maono ya kiuongozi Tanzania ijayo, Edward Lowassa akikatwa.
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment