Monday, October 26, 2015

NCHINI TANGANYIKA WATU 166 WAKAMATWA NA POLISI ATII KWA KUTANGAZA MATOKEO KABLA YA TUME


Kamanda mkuu wa kanda maalum ya Dar es Salaam, amesema kiasi cha watu 166 wakiwemo wageni wamekamatwa pamoja na vifaa vya kurushia habari zikiwemo computer kwa kile alichodai kuwa wametangaza matokeo kabla ya Tume ya Uchaguzi. Vile Vile Kamanda Kova ametoa onyo kwa mtu yeyote kusita mara moja kutoa habari ambazo zitapelekea uvunjifu wa amani,Ikiwemo kutoa matokeo ya uchaguzi kabla Tume kutoa matokeo hayo,na atakaefanya hivyo ni makosa na atakamatwa kufikishwa mahakamani .
Akihojiwa na ITV Tanzania,Kamanda Kova amesema ,wana askari wa kutosha ,magari na mafuta ya kutosha na Askari wengine wamepewa likizo wanasubiria nini kitatokea waitwe kazini. Pia Kamanda Kova amesema hana taarifa yoyote ya mtu kupigwa risasi ,kujeruhiwa au kuuwawa,na mpaka sasa hali ya usalama ipo shwari,akiwataka wananchi wafanye subra,waendelee na shuhuli zao na pia Tume ifanye kazi zake kwa uweledi.
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment