Friday, October 23, 2015

NCHINI ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD ASEMA MSIHOFU KATIKA KUHITIMISHA MKUTANO WA KAMPENI KWENYE UWANJA WA MNAZI MOJA MAISARA

Mgombea urais wa Zanzibar wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wananchi wakati akifunga kampeni za chama hicho katika Uwanja wa Maisara Unguja, jana. Picha: Mwananchi

Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia katika mkutano wa kufunga kampeni za Chama cha wananchi CUF kwa Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini nchini Zanzibar.


Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika ((Tanzania)) kupitia Chadema Mhe. Juma Duni Haji, akihutubia kwenye Mkutano huo wa kufunga kampeni mnazi moja maisara nchini Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti wa Timu ya Kampeni ya chama cha wananchi CUF Mansour Yussuf Himid, akiwahutubia melfu ya wananchi wa nchi Zanzibar katika mkutano wa kufunga kampeni za chama cha wananchi CUF katika viwanja vya mnazi moja maisara nchini Zanzibar.

Wafuasi na wapenzi wa chama cha wananchi CUF chini ya mwamvuli wa Ukawa, wakifuatilia mkutano wa kufunga kampeni katika viwanja vya Maisara.

Nchini Zanzibar. Mgombea urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewaambia watumishi wa umma kuwa kura watakazopiga kwenye Uchaguzi Mkuu ni za siri na hivyo Serikali haitajua wamepigia chama gani. Akihutubia maelfu ya wafuasi wa vyama vinavyounga Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na wananchi kwa ujumla wanao taka mabadiliko ya kweli na sio mabadiliko hewa ya miaka 50 ya domo tupu. Wakati wa mkutano wa kuhitimisha kampeni zake kwenye Uwanja wa Mnazi Mmoja maisara kisiwani Unguja nchini Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad aliwataka watumishi hao kuondoa hofu ya kufukuzwa kazi kwa kuipigia kura CUF. “Hakuna kamera zitakazokuwa kwenye vyumba vya kupigia kura,” alisema Maalim Seif Sharif Hamad, “Kura utakayopiga ni siri yako na hakuna mtu yoyote atakayejua mgombea uliyempigia.” Alisema kumekuwa na uzushi unaoenezwa na CCM kwamba watumishi wa Serikali, hasa askari wa KMKM, wametakiwa wasithubutu kuipigia CUF kwa kuwa watajulikana. “Msiwe na wasiwasi, wanawatisha kwa sababu wanaona maji yamefika shingoni. Fanyeni uamuzi sahihi kwa kuichagua CUF ili iweze kuboresha maslahi yenu,” alisema.
Maalim Seif Sharif Hamad amemwambia Rais Jakaya Kikwete wa nchi ya Tanganyika, ambaye ni amiri jeshi mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama kutofanya uamuzi utakaoitumbukiza nchi kwenye migogoro na vurugu. “Rais wangu Kikwete, ninajua kuna wagombea unaowapenda na wengine usiowapenda. Wewe kama baba wa familia usibague, tenda haki ili kuepusha nchi isiingie kwenye vurugu. “Ninawaelekeza wafuasi wa CUF kamwe wasifanye vurugu siku ya uchaguzi, lakini naomba Tume ya Uchaguzi hapa Zanzibar (ZEC) nayo itende haki.” Katibu huyo mkuu wa CUF pia alimwomba Shein kusimamia haki akisema uchaguzi isiwe sababu ya Wazanzibari kuuana. “ Shein tuna uchaguzi keshokutwa. Elewa kwamba katika uchaguzi kuna uwezekano wa kushinda au kushindwa. Ukishindwa uwe imara kukubali matokeo, vinginevyo nchi ikichafuka wewe utakuwa mwajibikaji namba moja,” alisema. “Mimi na wewe Shein tuna jukumu kubwa la kuwaeleza wapigakura wetu kuwa katika uchaguzi kuna kushinda au kushindwa. Nikishindwa nitakuwa wa kwanza kukupongeza hadharani.”alisema
Hata hivyo, Maalim Seif Sharif Hamad alisema anamshangaa Shein kutowajenga kisaikolojia wafuasi wake kwa kuwaeleza kuwa kushinda na kushindwa kunawezekana kwenye uchaguzi. Hata hivyo, mgombea huyo alisema kama Rais Kikwete na Shein watashindwa kusimamia haki katika uchaguzi huu, wasimtafute kama walivyokuwa wakifanya katika chaguzi zilizopita kwa kuwa hawatajua alipo. “(Mwanasiasa mkongwe) Mzee Nassor Moyo, mambo yakiharibika wasije kukutuma kwangu kwa kuwa utanitafuta na hutaniona. Wenye kazi ya kudai Zanzibar yao ni vijana,” alisema. Maalim Seif Sharif Hamad alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kukiwezesha chama hicho kufanya mikutano yake kwa amani na utulivu tofauti na ilivyokuwa katika kampeni zilizopita. “Polisi walituongoza vizuri kwenye mikutano yetu ya kampeni kulikuwa na amani na utulivu. Tunaomba hayo yaendelee siku ya uchaguzi,”alisema. Kwa upande wake, mgombea mwenza wa urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Juma Duni Haji alisema kwa mara ya kwanza wamepata mgombea wa urais wa Tanzania ambaye amekubali kushirikiana na Zanzibar ili kupata serikali tatu. “Wenzenu Tanzania Bara wako tayari kwa mabadiliko na nyie mko tayari....??” aliuliza na kujibiwa, “tuko tayari”.

Amesema iwapo wananchi watawachagua wagombea wanaotokana na Umoja wa Ukawa wataendeleza maridhiano na umoja wa wananchi, sambamba na kurejesha katiba iliyopendekezwa na wananchi ambayo itato haki kwa wananchi wote.Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Timu ya Kampeni ya CUF Mansour Yussuf Himid, amewataka wananchi kumchagua Maalim Seif ili aweze kuleta mabadiliko ya kiuchumi nchini. Amesema Maalim Seif ni kiongozi anayejiamini, jasiri na mwenye uwezo wa kuongoza nchi, na kwamba iwapo wazanzibari watafanya maamuzi sahihi watajionea mabadiliko kwa kipindi kifupi baada ya uchaguzi.

Akihutubia kwenye mkutano huo, Moyo alisema wakati walipoteuliwa, viongozi wa ZEC walikula kiapo kwa kushika kitabu cha Quran kueleza kuwa watatenda haki
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment