Waziri wa Kilimo na Mwakilishi wa jimbo la Kiembe samaki (CCM) Mansoour Yusuf Himid alisema mswaada huo ni kudanganywa wazanzibari na si jambo jengine.“Nashukuru siku hii ya leo kamati ya bunge imekuja kutudanganya Wazanzibari na siku ya leo nina huzuni kubwa sana kama Mtanzania kama mzanzibari naona kiini macho tu tunfanyiwa kama baraza la Wawakilishi hawajashirikishwa basi hakuna haja ya kukubali hilo” alisema Mansoor na kuongeza kwamba.
“Lazima tushirikishwe ipasavyo na muungano huu tumeungana kwa hiari sisi tumekwenda katika jamhuri wenyewe hii ni jamhuri ya ya pande mbili tumekwenda kwa hiayari tutarudi kwa hiyari tutabaki kwa hiyari”.alisema Mansoor.
Kama Wazanzibari hawajashirikishwa kupitia kura ya maoni na kufanyiwa kiini macho hicho basi wasikubali kudangwanywa alisema huku akiungwa mkono na wananchi wnegine wlaioshiriki kongamano hilo.
Mansoor alisema yeye binafsi muswada huo ataukataa barazani na ataukataa akiwa njiani ili kluonesha kwamba muungano huo una matatizona alisema hiyo ni nafasi pekee ya kuhakikisha Muungano unafanyiwa marekebisho kwani kukaa bila ya kukataa hilo hiyo ni fursa ya mwisho ambayo wananchi wa zanzibar hawataipata tena iwapo mswada huo ukenda barazani na kumalizwa.
“huu ndio fursa yetu ya mwisho wazanzibar nakwmabie tukicheza hapa ndio basi hatutakiona kitu chochote ndio basi tena” alisisitiza.
No comments:
Post a Comment