Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Mahmoud Mohammed Mussa ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alikuwa akiendesha kikao cha baraza hilo leo alikuwa na wakati mgumu kidogo baada ya kuendesha kikao ambacho kilikuwa moto baada ya pande mbili kuvutana upande upande wa serikali na upande wa wawakilishi.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi leo waliingia katika mjadala mkali na wa kuvutana kati ya pande mbili moja upande wa serikali na upande wa pili ni wawakilishi kutoka pande zote mbili (backbenchers) kuhusu hoja ya kutaka iundwe Kamati Teule kuchunguza ufisadi kwenye Baraza la Manispaa la Zanzibar.
Hoja ilikuwa kuchunguza tuhuma za ubadhifu mkubwa na rushwa katika Manispaa huku Waziri na baadhi ya maafisa wakitajwa kuchukua 10% lakini Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini alipinga vikali kuhusika na tuhuma hizo na kumtaka Mwakilishi Makame Mshimba Mbarouk wa Jimbo la Kitope (CCM) aliyetoa tuhuma hizo aombe radhi ndani ya baraza hilo lakini Mwakilishi huyo alikataa kuomba radhi kabisa na kushikilia msimamo wake kwamba ikiwa tuhuma sio za kwlei basi kamati teule ndio itasafisha tuhuma hizo na sio kuombwa radhi Waziri.
Hatimae baraza la wawakilishi chini ya Mwenyekiti wake Mahamoud Mohammed Mussa akaamua kupigwe kura ya kuulizwa kama wajumbe wanakubaliana na kuundwa kamati teule bau laa walipoulizwa wajumbe jumla ya wajumbe 29 walitaka uindwe kamati teule na wajumbe 28 walikataa isiundwe.
Lakini baadae alisimama Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakari na Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni Kisiwani Pemba (CUF) akawaomba wajumbe watumie utaratibu wa kura ya kuulizwa mjumbe mmoja mmoja juu ya kuundwa kamati teule na ndipo hapo matokeo ya kura yakatofautiana kutokana na wajumbe wengine wasiokuwa na msimamo wakaogopa ndipo kura 39 walitaka isiundwe kamati teule na waliotaka iundwe ni wajumbe 20 na hivyo suala la kutokuundwa kamati teule likazimika mara moja.
Wajumbe wa baraza la wawakilishi walisimamia hoja yao ya kutaka kuundwa kwa kamati teule ili kuisafisha serikali na kutafuta uoza na tuhuma zilizoelekezwa kwa watendaji juu ya kuwepo uharififu wa fedha kutoka kwa makampuni yalopewa tenda ya kuweka matangazo barabarani ambapo jumla ya makampuni matatu ndio yaliopewa tenda hiyo.
Kwa mujibu wa Waziri Makame anasema kimisingi kuna kosa limetendeka kutoka kwa maafisa wa Manispaa lakini linatokana na hayo makampuni matatu ambayo yanashindana na kila mmoja ametaka kumshitaki mwenzake kwani wamepewa kupashika matangazo barabarani ikiwemo yale ya kampuni za simu za mkononi za zanzitel na tigo lakini kwa mujibu wa Waziri anasema haoni kama huna sababu ya kuunda kamati kuchunguza suala hilo.
HIYO KAMATI NA IUNDWE NA WATAKAO KATA NDIO WANAFIKI NA NDIO WEZE. KWANZA WAJIUZULU KWA LAZIMA KISHA WASHTAKIWE WOTE NA WAELEZE MALI WALIZO NAZO WAMEZIPATA VIPI. MAANA MISHAHARA YAO SIYO INAYO WAFANYA WAKAJIJENGEYA MAJUMBA KUMI KUMI NA MAGARI YA KIFAHARI NA KUWAPELEKA WATOTO WAO NJE KUSOMA NA HUKU WAKIWAWACHA WANANCHI WA ZANZIBAR WAKILIYA NA UKAMEE. ULIYO SABABISHWA NA HAO MAWAZIRI WANAFIKI.
No comments:
Post a Comment