Mimi kawaida siendi mazikoni kwa viongozi wanafiki na wala wakifaa vifoo vibaya vyakuteseka hua sisikitiki na kuona huruma hayo ndio yanakuwa ndio malipo yao kwa watu wabaya wenye kuikumbatia dunia na kumsahau M/Mungu.
Hii ilikuwa hata Bw Mtume akifanya hivo, ilikuwa akiona kuna mnafiki kafaa basi haendi mazikoni na kulikuwa badhi ya Masahaba walikuwa mtu akifaa wanamuangalia Bw Mtume atakwenda kama hakwenda basi nawao hawendi.
Kwa hio na sisi Zanzibar katika Serekali ya SMZ kunaa viongozi wengi ni wanafiki Mindumi ya kuwili hukumbatia dunia na kuacha haki na kukumbatia batili kwa tamaa zao za kimaisha, ukiwauliza ktk utendaji haki huwa na msemo uliozoweleka kuwa USICHANGANYE DINI NA SIASA na huhisi siasa haina DINI na NICHAKA unaweza kufanya MASI bila ya kuhukumiwa na. ALLAH.
Kila kiongozi anae ona anakula starehe za uongozi leo kesho atajuta pindipo MAUTI yakimtambalia na ishara zikisha wadia kwake, hapo ndipo atakapojuwa kuwa hakuna ilani ya chama wala uongozi wa chama kumsaidia ni yeye na amali yake mbele ya ALLAH.
Leo hii tumesherehekea sherehe za uongo wa Muungano haliyakuwa viongozi wetu wa Zanzibar wanajuwa kuwa Muungano hapa ulipofika ni uongo na mzigo mkubwa Walio bebeshwa Wazanzibar kwa kisingizio cha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wakati chakujiuliza hio Tanganyika yenyewe haipo na wala hawataki Watanganyika iwepo kwa lengo la kuwa ikiwepo Tanganyika itakuwa hawatoweza kuimeza Zanzibar na kuizofisha kwa jina la Tanzania ni mmoja.
Lakini kuwepo kwa Tanganyika na kuto kuwepo hilo sio jukumu la Wazanzibar bali jukumu la Wazanzibar kudai haki ya nchi yao ambayo ni ZANZIBAR ndio muhimu kwa sasa, lakini chakusikitisha ktk jamii ya Wazanzibar nikutokana na viongozi wetu kuwa wanafiki na mindumi ya kuwili kupenda madaraka wasio yaweza yani kujipalia moto mbele ya .ALLAH.
Viongozi wetu hujifanya kifua mbele kukinga haki na kuhakikisha wanapata maslahi yao na kuwadidimiza wanchi wao ambao ndio wazanzibar walio wachagua wakati wa kupiga kura na sasa wanawabana Wazanzibar kudai haki zao kutokana tu naujabari wao wa madaraka lakini tu wasisahau yuko jabari mkubwa kuliko wao na huyo ana nguvu kuliko ilani ya chama kama kuna ilani ya chama ingemzuia BABA WA TAIFA ASIFE MAPEMA?
Wenyekukumbatia uongozi kwa matamanio ya dunia ole wao na athabu zenye kuumiza ambazo amesha zitaja M/mungu kwa hio musisahau kuwa kulikuwa na wenye sifa na mafahari leo hatuko nao tena na ukibanwa punzi tu dakika hushukuwe umewasili mbele ya Allah kwa hio uongozi ni jukumu na kila mwenye jukumu asiache kujitarisha majukumu ya kumjibu ALLAH mkubwa mola wa viombe vyote ulimwenguni. M/MUNGU IBARIKI ZANZIBAR NA WAZANZIBAR PIA.
No comments:
Post a Comment