Wednesday, April 27, 2011

WAZNZ WASUSIA SHEREHE ZA MUUNGANO,WAWACHIA VIONGOZI WA SMZ,WAZAZI BAR NA VIKUNDI VILIVYOLETWA KUTOKA BARA YANI TANGANYIKA

IMG_1577
 .
WENGI WA WA HAWA WATU KTK JUKWA NI SURA
NGENI WATU KUTOKA BARA WATANGANYIKA WENYEJI
WATU WA ZANZIBAR HAWAPO KABISA


.HAWA NDIO MUUNGANO UDUMU WZ''BAR WADUMIKE
 
kundi vilivyoletwa kutoka Bara.
Juu yakuwa sherehe za Muungano zimefanyika Zanzibar na shamra shamra nyingi kuandaliwa kutoka Bara kwa lengo la kipima joto kwa Wazanzibar lakini kubwa Zaidi nikuonekana kuwa majukwaa mengi ya raia wa kawaida yamekuwa wazi hayana watu na kuonekana  yalokuwa na watu ni yale yenye wageni walikwa na vikundi kutoka Bara.
Hii ni ishara moja tosha kuwa Wazanzibar wameshachwoshwa na Muungano na hawana hamu nao wengi wanahisi Muungano nikitu cha kulazimishwa na sio kitu cha ridhaa ya Wazanzibar wenyewe, Baada ya maadalizi makali ya Jeshi la polisi na Usalama wa taifa kuzuia harakati za Wazanzibar kupeleka mabao yao ya ujumbe mkali kupinga Muungano wameamua kususia kabisa kwenda na kuonekana hata jitihada za Serekali kupeleka magari bure mashamba kupata wingi wa watu ktk sherehe hizo imekonga wazanzibar wamesusia kabisa na sherehe hizo kusherehekewa na wageni walikwa na viongozi pamoja na vikudi vya sanaa.
Hii ni ishara moja ya kuupinga Muungano Wazanzibar na kusema washa tupelekwe kinguvu nguvu iko siku kamba hukata jiwe, Takribani watu wengi mitani walikuwa wakisema sherehe za leo ni za Bunuasi na Juha, Viongozi wa SMz kuwa Majuha na Wale wabara kuwa Bunuasi, Vipi pasherehekewe Muungano wa nchi mbili zilizo ungano yani Tanganyika na Zanzibar wakati hio Tanganyika wenyewe haipo?.
Hii nikufanywa Majuha viongozi wa SMz kwa matamanio yao ya nafsi na kuipeleka nchi pabaya, Wazanzibar wamesusia na kusema kama Serekali ni ya SMz basi wao ndio watakao kwenda kula sherehe zao za kuimarisha Muungano wa Tanzania na Zanzibar.
Wazanzibar wanasema Muungano umekufa tokea ilipokufa Tanganyika na katiba yake na hivi sasa gundi yakugandisha Muungano wa Tanzania na Zanzibar haigandi tena na kilichobaki nikuwa na urafiki mwema na kila mtu akawa na maslahi ya mambo yake mwenyewe kuliko kupoteza muda wa kuzungumzia Muungano ambao una mvutana wa kila upande kuona haufanyiwi haki.
 

No comments:

Post a Comment