KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
MIAKA 50 YA UHURU WA NCHI YA TANGANYIKA NA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA NCHI YA ZANIBAR MAJI 20% UMEME 20% ELIMU 0% HOSPITALI 1% MADAWA 0% MLO MOJA KWA SIKU TAFAKARI SANA.CCM MNASHANGA LOWASSA KUPANDA DALADALA HAMSHANGAI TWIGA KUPANDA NDEGE.VIONGOZI WA CUF WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI 2015 WAKIONYESHA SHAHADA ZAO ZA USHINDI ZILIZO SAINIWA NA KUPIGWAMUHURI NA ZEC CCM HAYA HAMUNA,AIBU HAMUINI,FEDHEHA HAMUHISI,UBINADAMU UMEWATUKA,M.MUNGU HAMUMUOGOPI HEBU JIULIZENI NYINYI VIUMBE WA AINA GANI...?????
Saturday, June 27, 2015
VIDEO-WAZIRI OMAR SHARI AKIZUNGUMZA NA WANA HABARI KUHUSU UWEKAJI CAMERA
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha mradi mkubwa wa kiulinzi katika maeneo mbali mbali ya Miji na mitaa nchini Zanzibar katika kukabiliana na vitendo atii vya uhalifu vinavyoendelea kuongezeka kila siku. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum Haji Omar Kheir ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Vuga Mjini nchini Zanzibar.
Alisema katika siku za karibuni hapa nchini Zanzibar tumeshuhudia vitendo vya uhalifu ikiwemo ujambazi, uporaji, hujuma, kuwamwagia watu tindikali pamoja na matokeo ya uchomaji moto mali za umma, taasisi na watu binafsi. Hali hiyo imeleta wasi wasi mkubwa atii kwa wananchi na wageni wanaoitembelea nchini Zanzibar kitu ambacho kinaweza kuathiri biashara ya Utalii inayoingiza fedha nyingi za kigeni.((fedha nyingi za kigeni mbona hatuzioni kujengea nchi badala yake mnajitajirisha nyinyi ni wazi munalinda matumbo yenu tu))
Alieleza kuwa mradi huo utahusisha uwekaji wa Kamera za kiulinzi katika maeneo yote ya Mji Mkongwe na baadhi ya maeneo ya kuingiilia mji wa nchi ya Zanzibar na maeneo yenye taa za kuongezea magari. Alizitaja Kampuni ya Raviltalco ya Romania na Rome Solutions iliyosajiliwa Zanzibar kuwa wamepewa kazi hiyo na zaidi ya kamera 900 zitafungwa katika maeneo hayo.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD ANENA SHEIN APOROJA NA KUBWABWAJA KUFURAHISHA BARZA
Nchini Zanzibar Hawa ndio ccm Maalim Seif Shariff Hamad wacha Umma uwahukumu mara hii wasidhani ukitishwa utakwenda kuwaangukia. hawa hawabebeki CCM ikiwa huwajuwi wote ni watumwa wa Dodoma maskini majuha hawa. Ikiwa CCM wanasema nchi hawatowi kwa vikaratasi walimpinduwa Sultani ? basi mara hii Sultani watakua wao na chama lao la Wakoloni Weusi Tanganyika zidi ya Umma wa Wananchi wa Zanzibar hatulitaki chama hili la CCM hapa nchini kwetu Zanzibar lirudi kwao liliko zaliwa huko Gining Dodoma nchi Tanganyika kwa Wakoloni Weusiiiiiiiii.
Posted Jumamosi, Juni 27, 2015 (11:12am)
Wakati Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad ameunga mkono kitendo cha mawaziri na wajumbe wa CUF kususia baraza, Shein amekipinga. Kauli tofauti za viongozi hao wa ngazi ya juu katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), zimekuja baada ya mawaziri na wawakilishi wa CUF kutoka ndani ya Baraza la Wawakilishi, wakisusia kujadili muswada wa sheria wa bajeti kuu ya matumizi ya serikali ya mwaka wa fedha 2015/2016. Akizungumza jana, Maalim Seif Shariff Hamad alisema wajumbe waliona ni njia sahihi ya kufanya ni kutoka ndani ya baraza, kwa sababu walikuwa hawasikilizwi kila wanapozungumzia mchakato unaoendelea kwa sasa wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura. Maalim alisema anashangazwa na wajumbe wa baraza kushindwa kujadili hoja iliyojitokeza, kiasi cha kusababisha baadhi ya wajumbe kususia kikao cha bajeti. Alisema kwamba tangu kuanza kwa uandikishaji, kumekuwa na mambo yanayofanyika kinyume kabisa na sheria, yakiwamo watoto chini ya umri wa miaka 18 kuandikishwa katika daftari la wapiga kura. Kadhalika alisema vyombo vya ulinzi na usalama kutumika kutisha watu huku wakiwa wamevaa ‘kininja’, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.
“Ni wazi inaonyesha kwamba kuna kasoro kwenye uandikishaji wananchi kwenye daftari la kudumu na usajili wa Vitambulisho vya mzanzibari mkazi,” alisema Maalim Seif Shariff Hamad. Kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), Maalim Seif Shariff Hamad alisema kwamba haiwezi kuvunjika, kwa sababu hakuna wa kuivunja kwa kuwa ilipitishwa kwenye Azimio la Baraza la Wawakilishi. Hivyo, alisema ikiwa inatakiwa kuvunjwa ni lazima, serikali ifuate sheria ya kuanza mchakato wa Kura ya Maoni, kuuliza wananchi watoe maoni yao na kisha kufikisha tena kwenye Baraza la Wawakilishi waijadili. Pia, Maalim Seif Shariff Hamad alisema wanasiasa wanaojadili suala la kuendelea au kutokuendelea kwa SUK, wanastahili kujiuzulu au kufukuzwa ndani ya vyama vyao. Maalim Seif Shariff Hamad ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar, Alisema kuwa, hoja ya CCM kutaka kufuta SUK inapaswa kulaaniwa kwani italeta machafuko Zanzibar. “Serikali ya Umoja wa Kitaifa si ya CCM wala CUF tu, ni ya wananchi wote, ni makosa makubwa kudhani kuwa serikali hiyo ni ya vyama hivyo viwili…Ilifanyika hivyo ili kutokuendelea umwagaji damu.” Aliongeza: “Tangu asubuhi kwa hapa Zanzibar ilifahamika kabisa kwamba nitazuiwa kuingia kwenye kikao cha Baraza la Wawakilishi hata watoto walijua .‘’ Maalim Seif Shariff Hamad alisema kisheria hatakiwi aingie kwa sababu yeye siyo mjumbe wa baraza hilo na anachotakiwa ni kupatiwa mwaliko tu.
POROJO NA BWABWAJA LA SHEIN.Shein akizungumzia kutoka nje kwa wajumbe na mawaziri wa CUF, alisema atii haikuwa mwafaka hasa kwa kuzingatia hoja waliokuwa wakiilalamikia haikuwa na uhusiano na muswada uliokuwa ukijadiliwa, uliohusu kupitisha matumizi ya bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016. Akihutubia baraza hilo kabla ya kulivunja jana Shein alisema, kitendo cha kususa baraza atii hakikuwa cha ufumbuzi hakikuzingatia umoja wao, SUK na maslahi ya Zanzibar na kuwataka wajumbe kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba na sheria. Shein alisema matarajio yake makubwa ni kuona wajumbe atii wanarejesha heshima kwa chombo hicho ikiwa ni pamoja na kutimizia matarajio ya wananchi ili waendelee kushuhudia maendeleo ((maendeleo ya domo tupu labda)) na ufumbuzi wa matatizo yao((miaka 50 na usheiya ufumbuzi hamujaupata tu CCM..?)).Alisema pia kuwa SMZ itahakikisha kila mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura, anapewa haki yake na kuwataka atii wanasiasa wasiwapotoshe wananchi juu ya haki ya raia ya kuchagua na kuchaguliwa, na badala yake atii waiacha Tume ya Uchaguzi ifanye kazi yake.((ifanye kazi yake au ifanye ukiritimba wake ili wewe ubaki madarakani kwa miaka mitano mengine ili utamalize kutuuza kwa Masultani wako wa Kitanganyika Wakoloni Weusi Tanganyika..??))
Hata hivyo, Shein alisema ni wajibu kwa kila mtu kuheshimu sheria ((wewe mwenyewe hufuati sheria unawafunga watu jela bila ya hatia unawapa watu urai wasio Wazanzibari baya zaidi Uchaguzi 2010 huku shinda kwa nini ukakubali kama sio mvujifu wa sheria..)) na kutoa ushirikiano kwa Tume ya Uchaguzi na kuhakiksiha Zanzibar inakuwa na uchaguzi huru na wa haki,((mawee wambiye basi wasiandikishe watoto na mamluki katika kambi za jeshi wambiya basi wasiandikishe watu mara mbili mbili wambiye basi wawaondowe walio vaa ninja na wawache kuwatisha wananchi kama kweli unataka uchaguzi wa huru na haki)) huku akijidai kuonya kuwa serikali yake haitasita kumchukulia mtu yeyote za kisheria ili kulinda amani ya wananchi wake.((wewe unamuonya nani hapa hii nchi sio yako hata kama Mkoloni Mweusi Tanganyika kakuweka na kukulinda hii ni nchi ya Wazanzibari na Wazanzibari hawakukupigia kuru wewe 2010 au ushasahau...?? unajidai unalinda amani ya wananchi ni wananchi gani hao unao sema wewe maana kama ni Wazanzibari hakutaki ilaa kama unalinda faida anazo pata Mkoloni Mweusi Tanganyika toka alipotunyanganya nchi 1964 sawa lakini usijidai unalinda wananchi wewe ndio uliye wasafirisha Masheikh wakafungwe jela huko Tanganyika kisha unajida unalinda wananchi au hao wahafidhina wenzio mnao ibaa pamoja na kuwauwa na kuwakandamiza Wazanzibari.))
Akizungumzia Muungano feki wa Tanganyika na Zanzibar, Shein alisema mapendekezao ya Katiba inayopendikizwa atii itafungua mlango mpya wa uchumi kupitia uchimbaji wa nishati ya mafuta na gesi na kuwataka wananchi kujitokeza wakati wa kura ya maoni wakati ukifika.((wewe kweli kipofu shein hivi bado unadoto kuwa hilo katiba la wazi wa ESCROW Wazanzibar Watalikubali...?? ))Kabla ya kulivunja baraza, Sheina alielezea atii mafanikio ya Serikali yake katika miaka mitano iliopita katika sekta ya miundombinu, anga, kilimo, utalii, uvuvi na uwekezaji na kueleza maeneo hayo yalioanishwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM yalielezwa kwa upana wake.((tumeona maendeleo siunajenga mnara Kisonge hahahaha)) Shangwe ndani ya ukumbi huo iliibuka baada ya Spika, Pandu Ameir Kificho kuwatambulisha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Firauni Jecha na Mkurugenzi wake, Firauni Kasim Ali na wajumbe wa baraza hilo kuchukua muda mrefu kupiga makofi. Viongozi walioalikwa kuhudhuria hafla hiyo ni pamoja na mabalozi wadogo wa India, Italia, Uingereza, China na Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya UNDP, UNFPA, Unicef, WHO, ILO, wakiwemo wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama, viongopzi wa dini, wanasiasa na Naibu Msajili wa vyama vya siasa Zanzibar, Rajabu Baraka
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
VIDEO-SAFARI YA MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD KWA KIKWETE RAIS WA NCHI YA TANGANYIKA HAIKUFUWA DAFU NA HALI KWA NCHI YA ZANZIBAR KUHUSU JESHI LA JWT KUWEKA VITUO VYA UANDIKISHWAJI NDANI YA KAMBI ZA KIJESHI NA KUANDIKISHA MAMLUKI BADO INAENDELEA
PART 1
PART 2
Safari ya Maalim Seif Shariff Hamad kwa Kikwete Rais wa nchi ya Tanganyika haikufua dafu na hali kwa nchi ya Zanzibar kuhusu jeshi la JWT kuweka vituo vya uandikishaji ndani ya kambi za kijeshi na kuandikisha mamluki bado inaendelea . Kwa hio inaonekana JWT,ZEC na vyombo vya Dola hapa nchini Zanzibar vimepewa baraka na Raisi wa nchi ya Tanganyika Kikwete ambae ni amiri Jeshi mkuu wa nchi hizi mbili Zanzibar na Tanganyika zilizo unganishwa kwa kini macho cha kutaka kuimeza nchi ya Zanzibar ili kutumia uwezo wao wote ili CCM chama chao cha Wakoloni Weusi Wa Tanganyika kibakie madarakani hapa nchini Zanzibar kwa lazima hata kama Wazanzibari hawakitaki je huwo ni Muungano au Ukoloni.....?? Kwa hali ilivyo njia peke yake yakuikomboa nchi ya Zanzibar zaidi ya UDHALIM wa CCM na UNYAMA wao kwa wananchi wa nchi ya Zanzibar na MASHEIKH wetu wanao endelea kuteseka ndani ya mwezi huu mtukufu wa ramadhani gerezani , kilicho baki sasa nikujipanga kwa kufa au kupona ili CCM iondoke kabisa katika nchi yetu ya Zanzibar.
Ikiwa wananchi wa nchi ya Zanzibar katika mwezi mtukufu huu wa Ramadhani tutamuelekea Allah kisawa sawa basi 2015 oct CCM itangoko . Laa tukisema hali hii haituhusu sisi ni yawana siasa ? Sasa tujiulize jee wale Masheikh wetu tuta wagomboa vipi...?? Au ndio tumuachie M/mungu...?? Hivi sasa wana siasa wamegonga ukuta na CCM kuondoka hawataki hawajali Sheikh wala Wazanzibar,kwa hio wakati umefika wa umma wa Zanzibar kutoa mamuzi ya kuingoa CCM. Kama ni kufanya subra na kunusuru umwagaji damu Maalim Seif Shariff Hamad ameshajitahidi hata kunyanganywa ushindi wake zaidi ya mara moja na kuridhia shingo upande ili tu,kunusuru Zanzibar na umwagaji damu. Lakini wapiiii tangulini Mkoloni Mweusi Tanganyika au hata Mkoloni mweupe akakwambia haya hii nchi kwenye kisahani nakupa. Kama CCM wa Zanzibar vitumwa vya Mkoloni Mweusi Tanganyika wangelikuwa ni waungwana na watu wenye kujua samani ya Maalim Seif Shariff Hamad na upole na hekma yake wasingali mtumia watoto wadogo wahuni wa CCM kumchafua kwa kumtukana kwenye majukwaa. Lakini kila kitu kina ukomo wake ,mara hii tunamuomba Maalim abakie kwake na ilobaki ni kazi ya umma wa Zanzibar kudial na CCM kuingoa au kuwauwa Wazanzibar wote, Maana washazoe watuuwe na njaa na hali ngumu ya maisha wao wanakula raha mara hii na nyinyi hatolala salama hayo makasiri yenu mlio jenga yatwawakia moto na in shaa allah hatutorudi nyuma kwa vitisho vya vyombo vya Dola.
Wazanzibar tuna zima juu ya Masheikh wetu wanao teseka gerezani ugenini na hii ni kipimo mbele ya Allah kutuangalia jee tutatumia jitihada gani kuwagomboa zidi ya madhalimu CCM...?? Maalim Seif Shariff Hamad marahii tuwacheye umma wa wazanzibar kuingoa CCM ,CCM hawajali hekma yako na wanatumia weekness hio ili kukupokonya ushindi na Zanzibar na Wazanzibari kuaangamia kwenye mikono ya Mkoloni Mweusi Tanganyika. Umma wa Zanzibar mara hii haurudi nyuma kwa vitisho vya vyombo vya Dola vya Wakoloni Weusi Vilivyo wekwa hapa toke 1964 na Nyerere au Ubabaishaji wa ZEC , ZEC ni CCM na tunasubiri oct in shaa allah Tunamuelekea Allah kwa kuikomboaa nchi yetu ya Zanzibar na Masheikh wetu juu ya udhalimu wa CCM.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
Friday, June 26, 2015
JECHA FARAUNI JECHA NA CCM WAJIANDA KUUWAULISHA WAZANZIBARI KWA MBINU CHAFU ZA UWANDIKISHAJI WA ((BVR))
HUYU NDIO FIRAUNI JECHA BIN FIRAUNI JECHA TUNAO TAKA MAMLAKA KAMILI IKIFIKA OKTOBA HUYU NA WENZAKE WAKAJIDAI KUITAGAZA CCM ATII NDIO MSHINDI NADHANI SOTE TUNAJUWA TUMFANYE NINI HIYO SIKU MAANA ASHAZOE YEYE KUCHEZA MCHEZO MCHAFU NA KULISHA WATU ILA MARA HII MARA HII MARA HII
MBINU zinazotumika kuvuruga uchaguzi zinajulikana vizuri Zanzibar. Tume kutumwa kuandikisha watoto wadogo, kuandikisha watu kwenye maeneo wasikoishi, na kutolihakiki daftari kubaini majina yaliyokuwemo mwaka 2005 ulipofanywa uandikishaji wa kwanza kwa mfumo wa BVR, ni maarufu.
Hii maana yake yaliyoanza kushuhudiwa kwenye vituo vya uandikishaji tangu Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) – inayoongozwa na kada Jecha Salim Jecha – ilipoanza kuandikisha wapigakura wapya Juni mosi katika Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, si mapya.
Hata ushenzi uliofanywa na Jeshi la Polisi katika kijiji cha Chwaka, kisiwani Tumbatu, wa kuwafyatulia wananchi mabomu ya kutoa machozi, badala ya kudhibiti makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokusanya makundi ya vitoto ili vikaandikishwe kuwa wapigakura, ni uthibitisho tu wa uzandiki wa viongozi wa CCM kujitia kuongoza kwa sheria.
Ndiyo yaleyale yanayotokea kwenye vituo vya uandikishaji wapigakura vya majimbo ya Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja tangu mwisho wa wiki iliyopita.
Baada ya kukamilisha ushetani wao wa kukusanya watu na kuwaandikisha makambini, sasa ni zamu ya kuwapeleka vituoni iwe ushahidi kuwa waliandikishwa vituoni kisheria.
Pale Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad alipoyaeleza uchafu uliogunduliwa katika utafiti uliofanywa kuanzia Aprili 2014, na wataalamu wa masuala ya uchaguzi wa chama hicho, kinachofanywa ni kutoa malalamiko ya muda mrefu kuwa CCM haina nia njema.
CUF inachofanya ni kuonesha wakuu wa Tume kwamba hakuna kinachoweza kufanywa kama hujuma kikabaki kisijuilikane. Kila ubaya unaotendwa, hata iwe mvunguni namna gani, hufikia siku ukajuilikana tu. Hauwezi kufichwa kwa miaka yote ya uhai. Ina maana waliotenda ubaya, hawana njia ya kuuficha milele.
Kwani si kweli kwamba Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK) la Zanzibar lilikuwa na wapigakura walioandikishwa zaidi ya mara moja kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005?
Kwani si kweli kuwa mpaka leo hii, miaka kumi kamili, si Tume ya Uchaguzi wala serikali iliyothubutu kuwapeleka mahakamani ili kushitakiwa wale waliobainika kujiandikisha zaidi ya mara moja?
Kwamba wakati inajuilikana wazi kitendo cha mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi Na. 11 ya 1984 na kuwa anayepatikana na hatia ya kosa hilo anastahili kuhukumiwa kifungo jela, serikali imeshindwa, ukweli imekataa kukamata na kuwashitaki wakosaji.
Bado ipo kwenye kumbukumbu za wengi kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilikuwa imegoma kuruhusu wataalamu wa uhakiki wa daftari kutoka kampuni ya Afrika Kusini kulifanyia uhakiki daftari hilo wakati walishawasili nchini kwa kazi hiyo kama ilivyoridhiwa kwa mkataba kati ya kampuni hiyo na Tume ya Uchaguzi.
Inakumbukwa bado wataalamu hao walikaa, kula na kulala bila ya kazi kwa kiasi cha wiki nzima wakisubiri ufumbuzi wa mvutano uliojengwa na uongozi wa juu wa serikali kwa kuzuia wataalamu hao kuingia ofisi za Tume na kukabidhiwa nyaraka za daftari ili kufanya ukaguzi.
Tena, mgomo huo wa serikali ulikuja wakati ikijua wazi kwamba gharama za kazi ya uhakiki zilikuwa chini ya wahisani waliofadhili mfuko wa kugharamia uchaguzi Zanzibar kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Kumbe nini hasa kilichoisukuma serikali kugoma wakati viongozi wanajinasibu kuongoza kwa haki na sheria na kwamba wanairidhia demokrasia na dhana nzima ya utawala bora?
Kwa kuzuia kazi ya uhakiki wa daftari la kudumu la wapigakura, ndio serikali inaonesha kupenda uadilifu na umakini kweli; au uvunjaji sheria na udhaifu kidhamira na kiuongozi?
Nani serikalini alijali kadhia ile ilipotokea? Nani alijiuliza na kupata jibu kuwa ni nini itakuwa hatima ya serikali kugoma kwa suala ililojua kuwa lilihusu mkataba wa kazi na kampuni ya kigeni?
Ni baada ya wahisani kushikilia na kutishia pamoja na shinikizo kubwa za CUF, ndipo serikali ikaruhusu uhakiki kufanywa, ingawa ulifanywa kwa masharti ya siri. Hivi viongozi wa serikali walikuwa na jibu gani la sababu ya kufanya uhuni na aibu kama vile?
Haikuwa na jibu zaidi ya kudhihirisha ilivyojiegemeza kwenye utawala mbaya usioleta tija kwa maslahi ya kweli ya Zanzibar. Bado wakasikika mawaziri mzigo wa Amani Abeid Karume kuvimbia nchi wafadhili. Unafiki mtupu. Nchi huru ipi isiyojilisha na kujivisha?
Basi viongozi wa CCM wa Zanzibar hawana pa kukimbilia. Aibu zao zinawekwa hadharani hata pale wanapojitahidi kuzificha. Hadithi ya mbuni kuzika kichwa kwenye minjugu kumbe shingo yote iko juu inaonekana.
Kufichuliwa kwa mbinu chafu za kuvuruga uchaguzi, zile zilizofanywa wakati wa kuelekea Oktoba 2010 na zinazofanywa mchana kweupe sasa nchi ikibakiwa na miezi mitatu tu kuendesha uchaguzi mwingine, kuna maana moja tu – CCM haijiamini hata inapokiuka taratibu za kuendesha uchaguzi huru, wa haki na ulio wazi.
Ni humohumo chama hiki kinatangazwa kushinda uchaguzi na wenyewe wakitamba walishinda kwa kishindo, kimbunga na kwa raha zao, baada tu ya kuchukua, kuweka, waaa!
Kama walivyofanya miaka ile ya nyuma ya uchaguzi – kuandikisha watoto wasiotimiza umri wa miaka 18, kuandikisha watu zaidi ya mara moja na kuhamisha watu kwenye maeneo wasiyoishi ambako huandikishwa kama wapiga kura – ndivyo wanavyofanya leo.
Mabasi yanayobeba watu majimbo ya wilaya ya Magharibi na kuwapeleka majimbo ya Mkoa wa Kaskazini, yanaonekana mchana yakienda na kurudi kupeleka watu.
Leo, watu, ambao Wazanzibari wamezoea kuwaita mamluki, wanapelekwa kwenye kambi za vikosi vya majeshi ya Jamhuri ya Muungano, wanasajiliwa na kupewa kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, halafu wanapelekwa maofisa wa Tume wanaoandikisha wapigakura wanaandikishwa.
Wakati ushetani huo unafanywa mchana kwa jeuri, unamsikia waziri katika serikali ya Muungano, tena Mzanzibari, analiambia bunge “wanayoyasema walete ushahidi ili yachunguzwe.” Mchunguzi ni nani, na huo uchunguzi ufanywe kumnufaisha nani?
Katika vitendo kama hivyo unamsikia mtu anayeitwa Mkinga anashambulia kwa maneno ya chuki mwandishi anayehamasisha utawala bora na unaofuata sheria. Anakasirika tunapowaeleza makada wa CCM wanaosaka urais kuwa hawana ajenda njema na Zanzibar na kwa kuwa wanajulikana, hawatasikilizwa.
Potelea mbali Mkinga. Wakati akiendelea kuchukiwa kwa kuwa tunayoyaeleza yanagusa rafiki zake waliopitisha katiba muflisi wakaita inayopendekezwa, ambayo wametahayari haijapigiwa kura na wananchi, tulioamua tunasonga mbele.
Ni vema kina Mkinga wajue, hatuna cha kuogopa wala wa kumuogopa, zaidi ya Mola aliyetuumba. Wanaopanga kutuhujumu washindwe na kulegea.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
VUAI ALI VUAI AJIVUA NGUWO MWENYEWE NA KUBAKI UCHII ((TUACHIWEEEE TUPUMUWEEEE WAZANZIBARI))
Pamoja na mchanganyiko wa wageni kutoka nchi mbali mbali wanaoishi katika nchi ya Zanzibar, bado inabakia kwamba ukimkuta mtu anaejinasibu kwamba yeye ni Mzanzibar akiwa amevaa nguo nusu uchi ama zinazo onyesha sehemu zake za siri basi kwa jamii ya Kizanzibari iliyomzunguka basi hiyo huwa ni laana kwake ambayo amejisababishia mwenye.
Nasema hivyo kwa kuwa jana tarehe 24/06/2015, nilimsikia kwa mbali Vuai Ali Vuai ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi nchini Zanzibar akijivua nguo mwenyewe hadharani na kujisukumizia laana yeye mwenyewe, tukio hilo lilitokea pale alipo zungumza na waandishi wa habari kuhusiana na baada ya Mawaziri wanaounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutoka upande wa chama cha CUF pamoja na Wawakilishi wote wa Chama hicho kuamua kutoka katika baraza la wawakilishi, baraza ambalo ndio kitovu ama chombo kinachotumika kutunga sheria za nchi pamoja na kujadili mambo yanayowahusu wananchi.
Nasema hivyo kwa kuwa jana tarehe 24/06/2015, nilimsikia kwa mbali Vuai Ali Vuai ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi nchini Zanzibar akijivua nguo mwenyewe hadharani na kujisukumizia laana yeye mwenyewe, tukio hilo lilitokea pale alipo zungumza na waandishi wa habari kuhusiana na baada ya Mawaziri wanaounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutoka upande wa chama cha CUF pamoja na Wawakilishi wote wa Chama hicho kuamua kutoka katika baraza la wawakilishi, baraza ambalo ndio kitovu ama chombo kinachotumika kutunga sheria za nchi pamoja na kujadili mambo yanayowahusu wananchi.
Kitendo alichokifanya Vuai cha kuzungumza na waandishi wa habari na kuwaambia kwamba analaani kitendo walichokifanya Mawaziri na Wawakilishi wa CUF akimaanisha kutoka kwao katika baraza la wawakilishi mimi nasema ni laana, mimi nasema hapa Vuai anajivua nguo na kujilaa nishaa mwenyewe, ukichukulia suala hili ukalivalisha mfano wa imani zetu za kidini, iwapo wewe ni baba mzazi ndani ya nyumba yako una watoto, na ukaamua kutowashughulikia watoto wale ilhali mungu amekupa uwezo wa kuwahudumia, basi watoto wale watanyonga roho zao na hapo huenda ukapata laana kwa tendo lile, nimetoa mfano huo kwa kuwa Vuai na chama chake CCM ingawa CUF ni mshirika katika Serikali lakini yeye hapa ndiye baba wa nyumba hii ya Zanzibar, na kwenye baraza la Wawakilishi ndio matatizo ya wananchi yanapojadiliwa, sasa anaposema kwamba pale hapakuwa pahala pa kujadili matatizo wanayoyapata wananchi katika zoezi zima la uandikishwaji wa wapiga kura wapya, madhila wanayoyapata na kero mbali mbali sasa wapi likajadiliwe......???
Bado naendelea kusema kwamba Vuai amejivua nguo hadharani mwenyewe na hapa sikosei, kwa Mzanzibar mwenye upeo mdogo wa kupambanua mambo basi hapati shida ya kulitafakari hili na atathibitisha kwamba ni kweli Vuai amefanya hivyo, alisikika akisema kwamba, “Sisi CCM tuligundua mapema mpango uliopangwa na CUF wa kuwazuilia wafuasi wa CCM wasiandikishe badala yake wahakikishe wao CUF wanaandikisha kwa wingi”, sasa hapa pana suala la kujiuliza ikiwa wewe ni chama unaeshika dola, wewe ndiye mwenye kutoa maamuzi ya juu katika nchi hii, kama uliligundua hili kwa nini usilizungumze kabla ya zoezi kuanza.....?? ingekuwa busara kama wangelifanya mkutano wa pamoja na wenzao wa CUF kuwaeleza kugundulika kwa mpango huo, au hata wangezungumza na waandishi wa habari kama wenzao wa CUF wanavyofanya mara wanapogundua jambo lolote linalowakwaza, lakini kwa kauli kama hii bado narudia kwamba amejivua nguo mwenyewe na asubiri laana, kwani kama kweli mpango huo ulikuwa unafanyika na CUF wa kuwazuia wafuasi wa CCM wasijiandikishe, basi wawakilishi wa CCM kule barazani walitakiwa waunge mkono ile hoja ya dharura iliyowasilishwa barazani ijadiliwe, kwa kuwa pande zote zilikuwa zina lawama zinazofanana, hapo tungesema kweli tumewatendea haki wananchi kwa kuwa tumejadili kuhusiana na kero wanazo zipata katika uandikishwaji na kutatua kero zao hizo.
Malalamiko waliyoyatoa CUF katika chombo cha kutunga sheria za nchi hii yaani Baraza la Wawakilishi na kudharauliwa na Kiongozi wa Baraza Hilo Spika Pandu Ameir Kificho, mimi nasema ni madai ya msingi na yenye ukweli kwa asilimia nyingi, kwa kuwa CUF hawajaanza leo kudai malalamiko hayo, kwa kauli ya Katibu Mkuu wa CUF ambaye pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad, malalamiko hayo yalishapelekwa katika Baraza la Mapinduzi, yalishawasilishwa kwa Shein ambaye yeye katika utawala wake ni kukaa kimya hata katika mambo muhimu ya nchi, yalishazungumzwa mara kadhaa katika mikutano ya hadhara ili kuwatanabahisha wananchi.
Na kama haitoshi Maalim Seif Shariff Hamad kwa kuonyesha wasiwasi wake juu ya hili aliona ni busara akauhutubia ulimwengu siku ya tarehe 10/05/2015 pale katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel Dar-Es-Salaam nchini Tanganyika, pale alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kadhia hiyo hiyo, ambayo CCM iliwakera sana, ndipo Vuai huyu huyu akasimama katika mkutano wa hadhara uliokuwa na wafuasi si zaidi ya 50 kwa mikoa mitatu kwa mikoa mitatu ya Unguja kujibu hoja za Maalim Seif Shariff Hamad na kumlamu kwa nini akafanya hivyo na kutoa rai mbadala kwamba, alitakiwa awasilishe malalamiko hayo kwao kwa kuwa wao ni washirika katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa jambo ambalo Maalim Seif Shariff Hamad alipohojiwa na Mohammed Abdurahman wa Sauti ya Ujerumani kwa kuwa Maalim Seif Shariff Hamad yuko juu Kisisiasa kama mlima kilimanjaro kumzidi Vuai Ali Vuai aliyekichuguu alisema kwamba hatua hizo alishazipita na hakuna muafaka uliofikiwa.
Haikuishia hapo nayo tume ya Uchaguzi ya ZEC, kupitia Mkurugenzi wake Salim Kassim Ali tarehe 11/06/2015, akajariibu na yeye pia atii kujibu hoja za Maalim Seif Shariff Hamad na alikataa yote ambayo aliyazungumza Maalim Seif Shariff Hamad wa CUF kama alivyokataa Vuai katika mkutano wa hadhara na ule wa waandishi wa habari mara baada Maalim Seif Shariff Hamad kutoa malalamiko yake mbele ya waandishi wa habari.“Kama kweli ana ushahidi wa kile anachokizungumza, kwa nini haleti malalamiko yake ZEC badala yake analalamika kwenye vyombo vya habari.....??” nukuu hii ilitolewa na ndugu Salim Kassim Ali siku ya tarehe 11/05/2015, na mfano wa nukuu kama hii ilitolewa na huyu Vuai Ali Vuai katika mkutano wake katika viwanja vya kwa Mabata, sasa kama CUF kupitia kwa wawakilishi wake waliamini kwamba Baraza la Wawakilishi ndipo miongozi mwa vikao vya Serikali hufanyika, ZEC nayo ni miongozi mwa taasisi za Serikali ambayo ZEC imekabidhiwa jukumu la kuendesha shughuli zote za Uchaguzi wa nchi ya Zanzibar, na katika nchi kuna malalamiko yanayoihusu Serikali kupitia ZEC, hivyo hakukuwa na ajabu wala aibu wala sababu ya kulaani kuwasilishwa kwa hoja binafsi inayohusu malalamiko juu ya Uandikishwaji, kwani ZEC ni taasisi ya Serikali na Baraza la Wawakilishi ni Sehemu ambayo matatizo ya Wananchi hujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi pamoja na kutungiwa Sheria.
Rai yangu, kama Vuai atakuwa ni mkweli aligundua njama alizozisema juu ya CUF pale aliposema kwamba wao waligundua mapema mpango wa CUF wa kuwazuilia wafuasi wa CCM wasijiandikishe, na CUF walishalalamikia mara kadhaa, hadi juzi kuamua kuliancha Baraza la Wawakilishi likiwa na wajumbe wa upande mmoja kitendo kilichichafua nchi ya Zanzibar na Serikali ya Shein, kitendo ambacho kwa mara ya pili kinatokea katika serikali ya Shein, ambapo hakijawahi kutokea katika awamu zilizopita, ni vyema Shein aakhirishe ufungaji wa baraza siku ya 26/06/2015, badala yake aunde Tume ya Muda mfupi kuchunguza tuhuma hii, ikiwa litafanyika hili nililoshauri basi tutakuwa tunaitengenezea jina na hadhi mpya ya nchi yetu ya Zanzibar. Lakini hili nililoshauri likifanyika ama lisifanyike bado Vuai ataendelea kujivua nguo mwenyewe hadharani na kujilaani hadi atakapoamua kuzivaa.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
WAWAKILISHI WA CCM WAMEMZUI MAKAMO WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR KUHUDHURIA SHUGHULI YA KUVUNJA BARAZA HILO
Nchini Zanzibar Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM, wamemzuia Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad kuhudhuria shughuli ya kuvunja Baraza hilo itakayoongozwa na Shein leo. Uamuzi huo ulitolewa baada ya Spika wa Baraza hilo, Pandu Ameir Kificho kutoa utangulizi kwa wajumbe akiwataka watengue kanuni ili viongozi wa kitaifa watakaohudhuria shughuli hiyo waweze kuingia ukumbini badala ya kukaa sehemu ya kawaida ya wageni waalikwa. Baada ya kutoa utangulizi, Spika Kificho alianza kuwahoji wajumbe wanaokubali viongozi wa kitaifa waruhusiwe kuingia ndani ya Ukumbi wa Baraza kwa kuwataja wakiwamo Rais wa Zanzibar, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, mpambe wa Rais na kuungwa mkono kwa kupigiwa makofi na sauti za ndiyo.
Hata hivyo, alipomtaja Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad wajumbe wote waliokuwapo katika Baraza hilo, ambao wote ni wa CCM, walikataa wakisema kwa sauti “hapana hapana hapana,” kitendo ambacho kilimfanya Spika kurudia kutaja jina hilo kwa zaidi ya mara tatu na majibu yalikuwa hapana. Hatua ya wawakilishi kumkataa Maalim Seif Shariff Hamad, imekuja siku moja baada ya mawaziri na wajumbe wa CUF kutoka nje ya baraza wakisusa kujadili na kupitisha muswada wa sheria wa bajeti kuu ya matumizi ya Serikali ya mwaka wa fedha 2015/16 wakipinga pamoja na mambo mengine, mchakato unaoendelea sasa wa uandikishaji wapigakura katika Daftari la Kudumu. “Mnakubali kutengua kanuni kuruhusu viongozi wa kitaifa kuhudhuria katika shughuli yetu ndani ya ukumbi...? Wageni wetu ni Rais wa Zanzibar, mpambe wake, Jaji Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais,” alihoji Spika Kificho lakini alipingwa baada ya kulitaja jina la Makamu wa Kwanza wa Rais. Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed aliwasilisha hati ya Serikali kuhusu marekebisho ya kanuni za Baraza.
Waziri Aboud alisema, Rais wa Zanzibar atakagua gwaride maalumu la Polisi kabla ya kuhutubia Baraza hilo saa 9.30 alasiri na kuwataka wajumbe wote kufika kabla ya kuwasili kwa Rais.
Kuhusu uamuzi wa kumkataa Maalim Seif Shariff Hamad, Aboud alisema upo katika mamlaka ya wajumbe kwa mujibu wa kanuni za Baraza hilo na kwamba hatua itakayofuata ni Spika kumwandikia barua Maalim Seif Shariff Hamad ya kutohudhuria shughuli hiyo ili kulinda uamuzi wa baraza hilo. “Baraza ni chombo cha kikatiba, Serikali hatuna uwezo wa kuliingilia na kanuni ndivyo zinavyosema. Wageni ambao ni viongozi wa kitaifa lazima utengue kanuni kwa kuwauliza wajumbe kama wanakubali au kukataa,” alisema. Waziri Aboud alisema SMZ haitaongeza muda wa Baraza ili kutoa nafasi ya Mwakilishi wa Kwa Mtipura (CCM), Hamza Hassan Juma kuwasilisha hoja binafsi ya kutaka wananchi waulizwe kama wanataka kuendelea na mfumo wa sasa wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) au la akisema kwa mujibu wa ratiba ya kikao cha bajeti, muda umemalizika na kumtaka kuangalia hoja yake katika siku za baadaye.
Kaimu Mnadhimu wa CCM, Ali Salum Haji ambaye pia ni Mwakilishi wa Kwahani, alisema wajumbe walifikia hatua ya kumzuia Maalim Seif Shariff Hamad kuhudhuria shughuli hiyo akisema ni Katibu Mkuu wa CUF, hivyo kitendo cha mawaziri na wawakilishi kususia Baraza hilo, kwa vyovyote, kulikuwa na baraka zake. “…hatujasikia kauli yoyote kutoka kwake ya kuwakemea na kama tungemruhusu ingeonekana anawachuuza wenzake.” Hata hivyo, alisema kama Maalim Seif Shariff Hamad anataka kuhudhuria, anaweza kuingia katika ukumbi wa wageni unaotumiwa kufuatilia matukio ya baraza hilo lakini si kujumuika na viongozi wengine walioalikwa ambao watakuwa ndani ya ukumbi. Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF, Ismail Jussa Ladhu alisema wamesikitishwa na tukio hilo, lakini hawajashangazwa kwa sababu wanaofanya hivyo ndio waliokuwa wakipinga kuanzishwa kwa SUK. Alisema tangu kuundwa kwake, SUK ilipata misukosuko mikubwa ikiwamo baadhi ya mawaziri na wawakilishi wa CCM kuwahamasisha wananchi wa majimbo yao kupiga kura za hapana wakati wa Kura ya Maoni ya kuchagua kuanzishwa kwa mfumo huo mwaka 2010. “Kinachotokea wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu, kinaleta ufa ndani ya Serikali ya pamoja na tayari tumeanza kuchukua hatua mbalimbali kuvilalamikia vyombo vinavyohusika na dhamana ya uandikishaji, polisi na jumuiya za kimataifa,” alisema Jussa.
Alisema inasikitisha wajumbe wa Baraza wameshindwa kujadili hoja iliyojitokeza ya wao kususia kikao cha bajeti ili kujua ukweli wake. Jussa alisema kuwa tangu kuanza kwa uandikishaji, kumekuwa na mambo yanayofanyika kinyume na sheria yakiwamo watoto chini ya umri wa miaka 18 kuandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, vyombo vya ulinzi na usalama kutumika kutisha watu pamoja na kuibuka kwa watu wenye silaha wakiwa wameficha nyuso usoni (ninja) na wengine wakivaa vinyago. Alisema matatizo yanayojitokeza, hivi sasa, yamechangiwa na utata mkubwa katika uandikishaji wananchi kwenye Daftari la Kudumu na Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi. Akizungumzia hatua ya wajumbe wa CUF kususia vikao, Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar, Awadh Ali Said alisema walikuwa sahihi kwa vile utaratibu waliotumia ni moja ya njia za kisiasa za kutoa hisia zao kidiplomasia. “Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi anatumikia mabwana watatu kwa wakati mmoja, jimbo na wananchi, chama chake cha siasa na maelekezo yake na Serikali, ndiyo maana Tume ya Mabadiliko ya Katiba tulisema mawaziri wasiwe wabunge au wawakilishi ili kutenganisha majukumu yao,” alisema Awadh ambaye alikuwa Kamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Alisema kwa kuwa wananchi ndio waathirika wa mambo ya uandikishaji na usajili wa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi, mwakilishi hawezi kukaa kimya hata kama ni waziri, kwa vile huo ndiyo wajibu wake.
Hata hivyo, alisema kitendo cha kuzuiwa kwa Maalim Seif Shariff Hamad kushiriki katika shughuli ya Baraza kinaweza kudhoofisha SUK kwa sababu wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu, Serikali inatakiwa kuwa na umoja pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wananchi wake. “Wawakilishi walitakiwa kujadili hoja au malalamiko yaliyotolewa na wenzao ikiwezekana waunde tume ya kufuatilia na kuchunguza ili kubaini ukweli wa mambo, badala yake wamejadili kuondoka kwao badala ya chanzo cha wao kususia kikao hicho ndani ya Baraza la Wawakilishi,” alisema mwanasheria huyo. Hata hivyo, alisema wakati bado unaruhusu kwa viongozi wa vyama vyote vya CCM na CUF kukaa pamoja na kujadili kasoro zinazojitokeza ili kuivusha Zanzibar salama.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
Thursday, June 25, 2015
NCHINI TANGANYIKA WATOTO WA UMRI YA CHINI YA MIAKA 18 AU KUJIANDIKISHA MARA MBILI AU TATU NA MASHINE ZA ((BVR)) UNACHUKULI HATUWA KALI ZA KISHERIA LAKINI ZANZIBAR ANDIKISHA TU MADAMU ATAIPIGIA KURA CCM
Nchini Tanganyika mji wa Geita. Kazi ya uandikishaji wapigakura imezidi kukumbwa na matatizo baada ya wananchi kuwafungia waandikishaji ndani ya kituo kutokana na kupata taarifa kuwa muda uliopangwa kwa ajili ya mitaa ya Buhalahala, Kisesa na Moringe umekwisha, huku wakiwa hawajapata nafasi ya kusajiliwa. Wakati vurugu hizo zikitokea, wananchi wa kata nne za wilayani Bukombe wanahofia kukosa nafasi ya kuandikishwa kutokana na maeneo yao kutoingizwa kwenye mfumo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), huku watu watatu, wakiwamo watoto wawili wilayani Hanang wakikamatwa kutokana na kujiandikisha mara mbili huku wakiwa hawajafikia umri unaotakiwa.
Tukio la Geita limetokea siku chache baada ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuwataka wananchi mkoani Kilimanjaro kutoruhusu mashine zinazotumika kuandikishia wapigakura kwa njia ya kielektroniki (BVR) kuondolewa vituoni endapo kuna watu ambao hawajaandikishwa. Uandikishaji mkoani Geita ulianza Juni 17, mwaka huu kwa kata tatu za Buhalahala, Mwatulole na Kalangalala na muda uliopangwa kumalizika ni juzi. Hali ilikuwa mbaya kwenye kata hizo baada ya wananchi kukaa vituoni hadi usiku wakisubiri kuandikishwa, na walipopata taarifa kuwa kazi hiyo haitaendelea kwa kuwa siku zilizopangwa zimemalizika, walichukua uamuzi huo wa kuzuia waandikishaji hadi watakapoandikisha wote waliokuwa wamesalia. “Nimekuja hapa nina siku ya tano leo (juzi). Kila nikija sipati nafasi ya kuandikishwa wengine wanakesha vituoni siku ya tano, lakini hawajaandikishwa na leo ndiyo mwisho,” alilalamika mkazi wa Mwatulole, Marwa Ernest. Mkazi mwingine, Neema Charles alisema:“Mwandikishaji anatuambia macho hayaoni, kwa hiyo sisi tufanyeje, tunataka kitambulisho kwani ndiyo cha msingi mwaka huu.”
Wananchi hao ambao walionekana kuwa na jazba, huku wakitishia kuchoma mashine kama wasingeandikishwa, walidai kuwa shughuli hiyo imetawaliwa na rushwa. Hali hiyo ilikikumba kituo cha Shule ya Sekondari ya Kalangalala, ambako hadi saa 1:30 usiku mwandishi alishuhudia zaidi ya wananchi 200 wakiwa kituoni wengine wakipigana na kusukumana kila mmoja akitaka kuandikishwa. “Hapa muda unaisha na leo (juzi) ndiyo mwisho, hatujui hatima yetu, wananchi wengi hatujaandikishwa, tumeshaomba tuongezewe mashine lakini hatusikilizwi zaidi tunashuhudia wenye fedha ndiyo wanaandikishwa,” alisema mkazi wa Kisesa, Mariana Peter. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Hellen Kahindi alikiri kuwapo kwa vurugu hizo na kwamba walikosea kuweka vituo pembezoni mwa mji, jambo lililosababisha wananchi wa mjini kukimbilia maeneo hayo wakihofia kutoandikishwa. Alisema vurugu hizo zilisababisha magari mawili ya Serikali kuvunjwa vioo, huku waandikishaji wakiponea chupuchupu kutokana na kuwapo na vurugu kubwa eneo la kutokea hadi polisi walipoingilia kati.
“Tunashukuru hakuna madhara makubwa yaliyotokea kwa waandikishaji na vifaa, lakini tumejipanga kwa zoezi hili jipya ili matatizo hayo yasijitokeze kwani tumeongeza wino na kwenye mashine,” alisema Kahindi. Wakati huohuo; wananchi wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, huenda wakashindwa kuandikishwa kutokana na kata zao nne kutowekwa kwenye mfumo wa utawala na hivyo kutotambulika na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi, maofisa wa kata hizo mpya za Katente, Katome, Bulangwa na Bulenga walisema maeneo yao hayamo kwenye mfumo wa NEC. Ofisa mtendaji Kata ya Katome, Lukuba Shitwala alisema kutokana na kata yake kutokuwa kwenye mfumo huo, huenda zaidi ya wananchi 9,000 wakakosa kuandikishwa. Hata hivyo, mkurungenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, James Ihunyo alisema tayari kata hizo zimeingizwa NEC, licha ya awali kutokuwamo, hivyo akawaomba watendaji kuhamasisha wananchi kujitokeza vituoni.
Watoto wawili wenye umri wa miaka 15 wa Kijiji cha Nangwa, wilayani Hanang’ na mtu mwingine mmoja wilayani Babati mkoani Manyara wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kujiandikisha zaidi ya mara tatu huku wakiwa hawajafikia umri wa 18 unaotakiwa. Mkuu wa mkoa wa Manyara, Joel Bendera alisema atahakikisha wote wanafikishwa mahakamani ili wachukuliwe hatua kali za kisheria kwa kuwa alishapiga marufuku watu kujiandikisha zaidi ya mara moja.
Mbali na watoto hao, mtu mwingine alijiandikisha mara tatu ni mkazi wa Boay wilayani Babati aliyetumia majina tofauti, akiitwa Petro Hhari kwenye kituo cha Shule ya Msingi ya Ditsoma A, Peter Tluway katika kituo cha zahanati na Peter Hary katika kituo cha ofisi ya kijiji hicho. Mratibu wa BVR mkoani Manyara, Mwajabu Nyamkomola alithibitisha kupata taarifa za matukio hayo. Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Mahamud Kambola alisema uandikishwaji unaendelea vizuri na wananchi wajitokeze.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
Wednesday, June 24, 2015
NCHINI ZANZIBAR MAWAZIRI WA CHAMA CHA CUF WASUSIA BAJETI
Nchini Zanzibar kasheshe zinaendelea. Mawaziri wa Serikali
ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na Wawakilishi kutoka chama cha
CUF jana walitoka kwenye kikao cha bajeti cha Baraza la
Wawakilishi, wakipinga urasimu katika utoaji vitambulisho
vya ukazi wa nchi ya Zanzibar na uandikishaji
wapigakura. Muda mfupi baada ya tukio hilo, Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ilitoa taarifa yake ikisema
kitendo cha mawaziri wa CUF kutoka kwenye kikao cha bajeti
ni kuvunja katiba, kwa kuwa wameshindwa kuheshimu
kiapo cha utii katika utekelezaji wa majukumu yao, kwa
mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
Mawaziri hao walitoka nje ya kikao hicho muda mfupi baada
ya Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Juma Duni Haji
kusimama na kutoa malalamiko ya kutoridhishwa na utendaji
wa SUK katika kusajili na kutoa vitambulisho hivyo
vinavyotumika katika kuandikisha wananchi kwenye Daftari
la Wapigakura. Wakati wawakilishi hao wanaondoka ndani
ya ukumbi, wenzao wa CCM walikuwa wakipiga makofi huku
wakiimba “CCM, CCM, CCM”, na baadaye baraza
kuendelea na muswada wa kupitisha mapato na matumizi ya
bajeti ya mwaka 2015/2016. Mawaziri waliohudhuria
mkutano huo ni Abubakar Khamis Bakar ambaye ni Waziri
wa Sheria na Katiba, Fatma Abdulhabib (Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais), Abdilahi Jihadi Hassan
(Mifugo na Uvuvi) na Haji Mwadini Makame (Ardhi,
Makazi, Maji na Nishati).
“Tumeamua kutoka ndani baada ya kuona wenzetu
tuliowaamini, wametubadilikia. Hawana nia njema ya
kuendesha serikali ya pamoja,” alisema makamu
mwenyekiti wa CUF, Juma Duni Haji alipoongea na
waandishi baada ya kutoka kwenye ukumbi
huo. “Wameanzisha Serikali ndani ya Serikali na sasa
wanawanyima haki wananchi kinyume na
katiba.” Juma Duni alisema kwa miaka mingi wananchi
wamekuwa wakizungushwa kusajiliwa na kupewa
vitambulisho vya ukazi, hali inayowaweka katika hatari ya
kupoteza haki zao za kijamii, ikiwa ni pamoja na fursa ya
kushiriki Uchaguzi Mkuu. Hata hivyo, alisema uamuzi wao
haujavunja katiba ya nchi ya Zanzibar na kwa hiyo
wataendelea na shughuli za Serikali kama kawaida.
Alisema kuwa kazi ya uandikishaji wapigakura kwenye
Wilaya ya Magharibi, Unguja imetawaliwa na vitisho na
kwamba watu wasiojulikana wamekuwa wakionekana
wakiwa na silaha za moto na kujifunika vitambaa usoni
mithili ya maninja na wengine kuvaa vinyago. “Katika
maisha yangu sijawahi kuona askari anayekwenda
kulinda akificha uso na huu ni mkasa mpya duniani.
Huwezi kumlinda raia kwa silaha za moto wakati yeye
hana chochote zaidi ya mikono yake,” alisema Juma
Duni. Naibu katibu mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui
alisema kuna vijana wame kwama kuandikishwa na
kuitaka Serikali kuondoa urasimu katika upatikanaji wa
vitambulisho vya ukazi.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
Subscribe to:
Posts (Atom)