“Tunauza roho zetu kwa kusaka riziki…. mikono iende kinywani na
midomo iweze kucheza cheza ‘’.
Hayo ni maneno ya wachimbaji wa mawe eneo la Kwareni Vitongoji ndani ya
wilaya ya Chakechake Pemba nchini Zanzibar.“Hatuna hila wala uwezo
wakutafuta kazinyengine ya kutuwezesha maisha yetu ambayo hatuna ajira’’
walikua wanalalamika nilipofika machimboni. Pamoja na yote hayo kazi hii ya
uchimbaji wamawe ni hatari wakati mwengine kupoteza viungo na kupoteza
maisha pia. “Najitahidi tu lakini mawazo telee kichwani na machozi kunilegalega
nikikumbuka mwenzangu Hamadi Zahor Faki, alivyo weza kukatikiwa na
mwamba wa jiwe na kufariki hapo hapo” alinieleza kwa uchungu Abdalla ‘bati
ambae nikiongozi wa chimbo hilo.
Hao ni baadhi tu ya mamia ya watu, wakati wanapokuwa wakiendelea na kazi
yao ya uchimbaji wa mawe katika eneo hilo kisiwani Pemba , wanapo pambana
na kazi ngumu na yenye kuhitaji ujasiri. Wengine huchimba mawe hayo hata kwa
kutumia mapango, na kujikata vidole, huku nyundo nazo zikitawala eneo hilo kwa
Kware, ambao palichangamka ni sawa na soko la Mwanakwerekwe
Unguja. Kubwa ambalo unaweza kulishangaa na kudondokwa na machozi hasa
kwa alie na huruma, ni kuona wapo wanachimba na kuvunja mawe wakikosa
zanabora za kufanyia kazi sambamba na mbinu bora za kuchimbia mawe .
Kalamu ya makala hii, haikutosheka na jicho la mbali, ndipo ilipojongea karibu na
kumsaka alau mmoja, na kumkatisha kazi ili aweze kuzungumza name.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
No comments:
Post a Comment