HUYU NDIO FIRAUNI JECHA BIN FIRAUNI JECHA TUNAO TAKA MAMLAKA KAMILI IKIFIKA OKTOBA HUYU NA WENZAKE WAKAJIDAI KUITAGAZA CCM ATII NDIO MSHINDI NADHANI SOTE TUNAJUWA TUMFANYE NINI HIYO SIKU MAANA ASHAZOE YEYE KUCHEZA MCHEZO MCHAFU NA KULISHA WATU ILA MARA HII MARA HII MARA HII
MBINU zinazotumika kuvuruga uchaguzi zinajulikana vizuri Zanzibar. Tume kutumwa kuandikisha watoto wadogo, kuandikisha watu kwenye maeneo wasikoishi, na kutolihakiki daftari kubaini majina yaliyokuwemo mwaka 2005 ulipofanywa uandikishaji wa kwanza kwa mfumo wa BVR, ni maarufu.
Hii maana yake yaliyoanza kushuhudiwa kwenye vituo vya uandikishaji tangu Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) – inayoongozwa na kada Jecha Salim Jecha – ilipoanza kuandikisha wapigakura wapya Juni mosi katika Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, si mapya.
Hata ushenzi uliofanywa na Jeshi la Polisi katika kijiji cha Chwaka, kisiwani Tumbatu, wa kuwafyatulia wananchi mabomu ya kutoa machozi, badala ya kudhibiti makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokusanya makundi ya vitoto ili vikaandikishwe kuwa wapigakura, ni uthibitisho tu wa uzandiki wa viongozi wa CCM kujitia kuongoza kwa sheria.
Ndiyo yaleyale yanayotokea kwenye vituo vya uandikishaji wapigakura vya majimbo ya Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja tangu mwisho wa wiki iliyopita.
Baada ya kukamilisha ushetani wao wa kukusanya watu na kuwaandikisha makambini, sasa ni zamu ya kuwapeleka vituoni iwe ushahidi kuwa waliandikishwa vituoni kisheria.
Pale Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad alipoyaeleza uchafu uliogunduliwa katika utafiti uliofanywa kuanzia Aprili 2014, na wataalamu wa masuala ya uchaguzi wa chama hicho, kinachofanywa ni kutoa malalamiko ya muda mrefu kuwa CCM haina nia njema.
CUF inachofanya ni kuonesha wakuu wa Tume kwamba hakuna kinachoweza kufanywa kama hujuma kikabaki kisijuilikane. Kila ubaya unaotendwa, hata iwe mvunguni namna gani, hufikia siku ukajuilikana tu. Hauwezi kufichwa kwa miaka yote ya uhai. Ina maana waliotenda ubaya, hawana njia ya kuuficha milele.
Kwani si kweli kwamba Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK) la Zanzibar lilikuwa na wapigakura walioandikishwa zaidi ya mara moja kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005?
Kwani si kweli kuwa mpaka leo hii, miaka kumi kamili, si Tume ya Uchaguzi wala serikali iliyothubutu kuwapeleka mahakamani ili kushitakiwa wale waliobainika kujiandikisha zaidi ya mara moja?
Kwamba wakati inajuilikana wazi kitendo cha mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi Na. 11 ya 1984 na kuwa anayepatikana na hatia ya kosa hilo anastahili kuhukumiwa kifungo jela, serikali imeshindwa, ukweli imekataa kukamata na kuwashitaki wakosaji.
Bado ipo kwenye kumbukumbu za wengi kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilikuwa imegoma kuruhusu wataalamu wa uhakiki wa daftari kutoka kampuni ya Afrika Kusini kulifanyia uhakiki daftari hilo wakati walishawasili nchini kwa kazi hiyo kama ilivyoridhiwa kwa mkataba kati ya kampuni hiyo na Tume ya Uchaguzi.
Inakumbukwa bado wataalamu hao walikaa, kula na kulala bila ya kazi kwa kiasi cha wiki nzima wakisubiri ufumbuzi wa mvutano uliojengwa na uongozi wa juu wa serikali kwa kuzuia wataalamu hao kuingia ofisi za Tume na kukabidhiwa nyaraka za daftari ili kufanya ukaguzi.
Tena, mgomo huo wa serikali ulikuja wakati ikijua wazi kwamba gharama za kazi ya uhakiki zilikuwa chini ya wahisani waliofadhili mfuko wa kugharamia uchaguzi Zanzibar kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Kumbe nini hasa kilichoisukuma serikali kugoma wakati viongozi wanajinasibu kuongoza kwa haki na sheria na kwamba wanairidhia demokrasia na dhana nzima ya utawala bora?
Kwa kuzuia kazi ya uhakiki wa daftari la kudumu la wapigakura, ndio serikali inaonesha kupenda uadilifu na umakini kweli; au uvunjaji sheria na udhaifu kidhamira na kiuongozi?
Nani serikalini alijali kadhia ile ilipotokea? Nani alijiuliza na kupata jibu kuwa ni nini itakuwa hatima ya serikali kugoma kwa suala ililojua kuwa lilihusu mkataba wa kazi na kampuni ya kigeni?
Ni baada ya wahisani kushikilia na kutishia pamoja na shinikizo kubwa za CUF, ndipo serikali ikaruhusu uhakiki kufanywa, ingawa ulifanywa kwa masharti ya siri. Hivi viongozi wa serikali walikuwa na jibu gani la sababu ya kufanya uhuni na aibu kama vile?
Haikuwa na jibu zaidi ya kudhihirisha ilivyojiegemeza kwenye utawala mbaya usioleta tija kwa maslahi ya kweli ya Zanzibar. Bado wakasikika mawaziri mzigo wa Amani Abeid Karume kuvimbia nchi wafadhili. Unafiki mtupu. Nchi huru ipi isiyojilisha na kujivisha?
Basi viongozi wa CCM wa Zanzibar hawana pa kukimbilia. Aibu zao zinawekwa hadharani hata pale wanapojitahidi kuzificha. Hadithi ya mbuni kuzika kichwa kwenye minjugu kumbe shingo yote iko juu inaonekana.
Kufichuliwa kwa mbinu chafu za kuvuruga uchaguzi, zile zilizofanywa wakati wa kuelekea Oktoba 2010 na zinazofanywa mchana kweupe sasa nchi ikibakiwa na miezi mitatu tu kuendesha uchaguzi mwingine, kuna maana moja tu – CCM haijiamini hata inapokiuka taratibu za kuendesha uchaguzi huru, wa haki na ulio wazi.
Ni humohumo chama hiki kinatangazwa kushinda uchaguzi na wenyewe wakitamba walishinda kwa kishindo, kimbunga na kwa raha zao, baada tu ya kuchukua, kuweka, waaa!
Kama walivyofanya miaka ile ya nyuma ya uchaguzi – kuandikisha watoto wasiotimiza umri wa miaka 18, kuandikisha watu zaidi ya mara moja na kuhamisha watu kwenye maeneo wasiyoishi ambako huandikishwa kama wapiga kura – ndivyo wanavyofanya leo.
Mabasi yanayobeba watu majimbo ya wilaya ya Magharibi na kuwapeleka majimbo ya Mkoa wa Kaskazini, yanaonekana mchana yakienda na kurudi kupeleka watu.
Leo, watu, ambao Wazanzibari wamezoea kuwaita mamluki, wanapelekwa kwenye kambi za vikosi vya majeshi ya Jamhuri ya Muungano, wanasajiliwa na kupewa kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, halafu wanapelekwa maofisa wa Tume wanaoandikisha wapigakura wanaandikishwa.
Wakati ushetani huo unafanywa mchana kwa jeuri, unamsikia waziri katika serikali ya Muungano, tena Mzanzibari, analiambia bunge “wanayoyasema walete ushahidi ili yachunguzwe.” Mchunguzi ni nani, na huo uchunguzi ufanywe kumnufaisha nani?
Katika vitendo kama hivyo unamsikia mtu anayeitwa Mkinga anashambulia kwa maneno ya chuki mwandishi anayehamasisha utawala bora na unaofuata sheria. Anakasirika tunapowaeleza makada wa CCM wanaosaka urais kuwa hawana ajenda njema na Zanzibar na kwa kuwa wanajulikana, hawatasikilizwa.
Potelea mbali Mkinga. Wakati akiendelea kuchukiwa kwa kuwa tunayoyaeleza yanagusa rafiki zake waliopitisha katiba muflisi wakaita inayopendekezwa, ambayo wametahayari haijapigiwa kura na wananchi, tulioamua tunasonga mbele.
Ni vema kina Mkinga wajue, hatuna cha kuogopa wala wa kumuogopa, zaidi ya Mola aliyetuumba. Wanaopanga kutuhujumu washindwe na kulegea.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
No comments:
Post a Comment