Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipokelewa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, baada ya kuwasili akitokea Dar es Salaam nchini Tanganyika ambako aliteuliwa Rasmi kuwa Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya CUF mwaka 2015.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa nchi ya Zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi Taifa (CUF) Professa Ibrahim Haroun Lipumba amemtaka Rais Kikwete kuhakikisha haki inatendeka katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu unakuwa huru na wa haki. Lipumba ameyasema hayo jana katika viwanja vya Kibanda Maiti wakati akimthibitisha Maalim Seif kuwa ndio mgombea urais wa nchi ya Zanzibar katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelefu katoka sehemu mbali mbali. Mwenyekiti huyo alisema ni vyema kwa Rais Kikwete kuelewa kuhakikisha kwamba dunia imebadilika na viongozi wasiotenda haki wakasababisha maafa katika nchi zao hawatasita kupelekwa the Hegue.
“Ninamwambia Rais Kikwete ambaye ndio amiri jeshi mkuu hivi sasa ulimwengu umebadilika tunashuhudia viongozi wenye kujifanyia mambo ovyo wanafikishwa The Hegue kwa kuvunja haki za msingi za binadamu na kusababisha machafuko katika nchi zao” alitahadharisha. Professa Lipumba alisema uchaguzi wa mara hii ahakikishe atakayeshinda ndiye atakayekabidhiwa ushindi na kusiwepo kuporwa ushindi kwani kufanya hivyo hakutawezekana kwani chama hicho kimechoshwa na tabia hizo. Akitilia mkazo kauli hiyo, Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Shariff Hamad amesema katika chaguzi zote zilizofanyia kuanzia kurudi kwa mfumo wa vyama vingi amekuwa akiwakataza vijana kuingia barabarani na kutofanya fujo baada ya kuporwa ushindi wao lakini mara hii atajizuwia kufanya hivyo.“Mara zote vijana wanasema Maalim anatuzuwia lakini mara hii nasema wazi Kikwete ajue na Dk Shein ajue kabisa sitawazuwia vijana kudai haki yao kabisa kabisa, nitawaambia vijana daini haki yetu” alitahadharisha Maalim Seif Shariff Hamad huku akishangiriwa na vijana katika uwanja huo. Amesema kwamba uchaguzi huu ufanyike kwa haki na anayeshinda apewe ushindi wake na yeye yupo tayari kukubali matokeo iwapo ameshindwa kihalali lakini lisipofanyika hilo haitawezekana kuporwa ushindi wake. Aidha Maalim Seif Sharrif Hamad amesema Zanzibar inahitaji kiongozi jasiri na mwenye kujiamini kuwaunganisha wazanzibari na watanzania wote. Alisema kuna kiongozi ambaye ametangaza nia na kusema ataudumisha muungano jambo ambalo amesema muungano huu ulivyo hauwezekani kwani muungano unaotakiwa ni ule ambao wa heshima na kila nchi iwe na mamlaka yake na kama sivyo ulivyo sasa. “Nimesikia kuna mtu ametangaza nia anasema ataulinda muungano sisi tunamwambia kiongozi wa aina hiyo hatufai sisi tunataka mamlaka kamili kila nchi iwe na mamlaka yake tunataka muungano wa manufaa sio kama huu” amesema Maalim
Maalim Seif Shariff Hamad amemwagia sifa Dk Shein kwa kuendesha vizuri serikali ya umoja wa kitaifa pamoja na kuimarisha mafao kwa wazee na kuwaongezea mshahara watumishi wa serikali lakini amesema licha ya mishahara hiyo bado watumishi hao wanahitaji kuongezewa zaidi kutokana na hali ya maisha. Akitaja vipaumbele vyake Maalim Seif Shariff Hamad amesema jambo la kwanza ni kuunda wizara ya mafuta na gesi Zanzibar ili kuimarisha uchumi wa Zanzibar. Aidha amesema ataimarisha biashara kwa kufungua mpango wa bandari huru na ataondoa vikwazo vyote kwa wafanyabiashara ili wawe huru kufanya biashara zao popote ndani na nje ya nchi. Amesema suala la uchumi litapewa kipaumbele na atachuja watendaji wake ili kuimairisha sekta zote za afya elimu na miundombinu huku akisema suala la kuingarisha Zanzibar linahitaji mipango madhubuti tu kwa kuwa fedha zinazokusanywa kwenye kodi zinatosha kuifanya Zanzibar kuwa juu kiuchumi. “Wapo watu wanaweza kusema pesa hizo tutazipata wapi lakini jamani siku hizi kuna kitu kinachoitwa PPP Public Private Patneship watu wanawekeza katika nchi muhimu kuwepo usalama tu ”
Amewaambia wafuasi hao kwamba kila kitu ambacho wamekipanga kukifanya watakitekeleza kwa wakati kwa kuwa jambo kubwa ni dhamira ya kutenda hayo yaliokusudiwa na uwezo ambapo tayari ameshaunda tume maalumu ya kupitia mapendekezo na vipaumbele vyote vilivyoelezwa. “Haya ninayoyasema tayari tumeshaunda tume yangu ya kuyapitia yote haya niliyoyaeleza na bajeti yake haya mapendekezo yetu tutakuja kuyasema wakati ukifika sasa hivi kampeni bado lakini tutasema hili linahitaji kiasi gani na tutazitoa wapi” aliongeza Katibu Mkuu huyo. Maalim Seif Shariff Hamad alisema ataiga mfano wa Rais Chisano wa Zambia ambaye alikuwa akifuatilia mwenyewe wawekezaji katika nchi yake kwa lengo la kuimarisha uchumi wa Zanzibar. Akizungumzia suala la mikopo ya wanafunzi amesema suala hilo linamuumiza sana kwa kuona vijana wana sifa za kujiunga na vyuo vikuu lakini hawapewi fursa na badala yake fedha zinatolewa kwa watoto wa wakubwa tu wale wa wanyonge hawapewa fursa hiyo.
“Linanikereketa sana hili la wanafunzi maskini wasio na uwezo wanashindwa kusoma lakini nasema chini ya uongozi wangu in shaa allah mtasoma kuanzia darasa la kwanza hadi mnamaliza kusoma bure hakuna mkopo kutakuwa na ufadhili” aliahidi. Katika suala la michezo Maalim Seif Shariff Hamad amesema wazanzibari waliopo nje ya nchi wamekuwa wakishiriki michezo mbali mbali na kushinda katika nchi tofauti hivyo kuna sababu ya vipaji hivyo kuendelezwa hapa hapa nyumbani. Akizungumza katika mkutano huo Mzee Hassan Nassor Moyo amesema hivi sasa yupo huru kuongea chochote kwa kuwa ameshafukuzwa katika Chama Cha Mapinduzi na sasa hivi yupo tayari kuitwa na chama chochote akazungumze kama Mzee kama Matanzania. “Siku zile nilikuwa napanda jukwaani nazungumza kama Mzee lakini nilikuwa CCM lakini sasa hivi sina chama hata Chadema wakinita nizungumze katika mkutano wao nitapanda jukwaani kama Mzee nina haki ya kuongea” alisema Mzee Moyo huku akishangiriwa.
Aliwaambia wafuasi hao wa CUF kwamba Zanzibar inahitaji kiongozi jasiri na kiongozi mwenye mtazamo wa serikali tatu ili kila nchi iwe na serikali yake na kila nchi iwe na mamlaka kamili na yeyote asiyataka hivyo hafai kuwa rais wa Zanzibar. “Kiongozi anayeitetea Zanzibar ndiye tunayemtaka lakini kiongozi ambaye haitetei Zanzibar huyo hatufai na hawa CCM wao hawataki tupate mamlaka yetu kwa hivyo hawatufai hawa” alisema Mzee Moyo. Naye Masoor Yussuf Himid amemtaja Maalim Seif Shariff Hamad pekee atakayeweza kuivusha Zanzibar ilipo na kuipeleka kwenye maendeleo kwa kuwa ni mtu mwenye busara na mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuleta maendeleo ya kiuchumi na kisiasa lakini pia dhamira yake ni kuwaunganisha wazanzibari wote na watanzania.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO
No comments:
Post a Comment