Nchini Zanzibar kasheshe zinaendelea. Mawaziri wa Serikali
ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na Wawakilishi kutoka chama cha
CUF jana walitoka kwenye kikao cha bajeti cha Baraza la
Wawakilishi, wakipinga urasimu katika utoaji vitambulisho
vya ukazi wa nchi ya Zanzibar na uandikishaji
wapigakura. Muda mfupi baada ya tukio hilo, Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ilitoa taarifa yake ikisema
kitendo cha mawaziri wa CUF kutoka kwenye kikao cha bajeti
ni kuvunja katiba, kwa kuwa wameshindwa kuheshimu
kiapo cha utii katika utekelezaji wa majukumu yao, kwa
mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
Mawaziri hao walitoka nje ya kikao hicho muda mfupi baada
ya Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Juma Duni Haji
kusimama na kutoa malalamiko ya kutoridhishwa na utendaji
wa SUK katika kusajili na kutoa vitambulisho hivyo
vinavyotumika katika kuandikisha wananchi kwenye Daftari
la Wapigakura. Wakati wawakilishi hao wanaondoka ndani
ya ukumbi, wenzao wa CCM walikuwa wakipiga makofi huku
wakiimba “CCM, CCM, CCM”, na baadaye baraza
kuendelea na muswada wa kupitisha mapato na matumizi ya
bajeti ya mwaka 2015/2016. Mawaziri waliohudhuria
mkutano huo ni Abubakar Khamis Bakar ambaye ni Waziri
wa Sheria na Katiba, Fatma Abdulhabib (Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais), Abdilahi Jihadi Hassan
(Mifugo na Uvuvi) na Haji Mwadini Makame (Ardhi,
Makazi, Maji na Nishati).
“Tumeamua kutoka ndani baada ya kuona wenzetu
tuliowaamini, wametubadilikia. Hawana nia njema ya
kuendesha serikali ya pamoja,” alisema makamu
mwenyekiti wa CUF, Juma Duni Haji alipoongea na
waandishi baada ya kutoka kwenye ukumbi
huo. “Wameanzisha Serikali ndani ya Serikali na sasa
wanawanyima haki wananchi kinyume na
katiba.” Juma Duni alisema kwa miaka mingi wananchi
wamekuwa wakizungushwa kusajiliwa na kupewa
vitambulisho vya ukazi, hali inayowaweka katika hatari ya
kupoteza haki zao za kijamii, ikiwa ni pamoja na fursa ya
kushiriki Uchaguzi Mkuu. Hata hivyo, alisema uamuzi wao
haujavunja katiba ya nchi ya Zanzibar na kwa hiyo
wataendelea na shughuli za Serikali kama kawaida.
Alisema kuwa kazi ya uandikishaji wapigakura kwenye
Wilaya ya Magharibi, Unguja imetawaliwa na vitisho na
kwamba watu wasiojulikana wamekuwa wakionekana
wakiwa na silaha za moto na kujifunika vitambaa usoni
mithili ya maninja na wengine kuvaa vinyago. “Katika
maisha yangu sijawahi kuona askari anayekwenda
kulinda akificha uso na huu ni mkasa mpya duniani.
Huwezi kumlinda raia kwa silaha za moto wakati yeye
hana chochote zaidi ya mikono yake,” alisema Juma
Duni. Naibu katibu mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui
alisema kuna vijana wame kwama kuandikishwa na
kuitaka Serikali kuondoa urasimu katika upatikanaji wa
vitambulisho vya ukazi.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
No comments:
Post a Comment