Saturday, June 27, 2015

MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD ANENA SHEIN APOROJA NA KUBWABWAJA KUFURAHISHA BARZA



Nchini Zanzibar Hawa ndio ccm Maalim Seif Shariff Hamad wacha Umma uwahukumu mara hii wasidhani ukitishwa utakwenda kuwaangukia. hawa hawabebeki CCM ikiwa huwajuwi wote ni watumwa wa Dodoma maskini majuha hawa. Ikiwa CCM wanasema nchi hawatowi kwa vikaratasi walimpinduwa Sultani ? basi mara hii Sultani watakua wao na chama lao la Wakoloni Weusi Tanganyika zidi ya Umma wa Wananchi wa Zanzibar hatulitaki chama hili la CCM hapa nchini kwetu Zanzibar lirudi kwao liliko zaliwa huko Gining Dodoma nchi Tanganyika kwa Wakoloni Weusiiiiiiiii.               
Posted Jumamosi, Juni 27, 2015 (11:12am)
Wakati Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad ameunga mkono kitendo cha mawaziri na wajumbe wa CUF kususia baraza, Shein amekipinga. Kauli tofauti za viongozi hao wa ngazi ya juu katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), zimekuja baada ya mawaziri na wawakilishi wa CUF kutoka ndani ya Baraza la Wawakilishi, wakisusia kujadili muswada wa sheria wa bajeti kuu ya matumizi ya serikali ya mwaka wa fedha 2015/2016. Akizungumza jana, Maalim Seif Shariff Hamad alisema wajumbe waliona ni njia sahihi ya kufanya ni kutoka ndani ya baraza, kwa sababu walikuwa hawasikilizwi kila wanapozungumzia mchakato unaoendelea kwa sasa wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura. Maalim alisema anashangazwa na wajumbe wa baraza kushindwa kujadili hoja iliyojitokeza, kiasi cha kusababisha baadhi ya wajumbe kususia kikao cha bajeti. Alisema kwamba tangu kuanza kwa uandikishaji, kumekuwa na mambo yanayofanyika kinyume kabisa na sheria, yakiwamo watoto chini ya umri wa miaka 18 kuandikishwa katika daftari la wapiga kura. Kadhalika alisema vyombo vya ulinzi na usalama kutumika kutisha watu huku wakiwa wamevaa ‘kininja’, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.
“Ni wazi inaonyesha kwamba kuna kasoro kwenye uandikishaji wananchi kwenye daftari la kudumu na usajili wa Vitambulisho vya mzanzibari mkazi,” alisema Maalim Seif Shariff Hamad. Kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), Maalim Seif Shariff Hamad alisema kwamba haiwezi kuvunjika, kwa sababu hakuna wa kuivunja kwa kuwa ilipitishwa kwenye Azimio la Baraza la Wawakilishi. Hivyo, alisema ikiwa inatakiwa kuvunjwa ni lazima, serikali ifuate sheria ya kuanza mchakato wa Kura ya Maoni, kuuliza wananchi watoe maoni yao na kisha kufikisha tena kwenye Baraza la Wawakilishi waijadili. Pia, Maalim Seif Shariff Hamad alisema wanasiasa wanaojadili suala la kuendelea au kutokuendelea kwa SUK, wanastahili kujiuzulu au kufukuzwa ndani ya vyama vyao. Maalim Seif Shariff Hamad ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar, Alisema kuwa, hoja ya CCM kutaka kufuta SUK inapaswa kulaaniwa kwani italeta machafuko Zanzibar. “Serikali ya Umoja wa Kitaifa si ya CCM wala CUF tu, ni ya wananchi wote, ni makosa makubwa kudhani kuwa serikali hiyo ni ya vyama hivyo viwili…Ilifanyika hivyo ili kutokuendelea umwagaji damu.” Aliongeza: “Tangu asubuhi kwa hapa Zanzibar ilifahamika kabisa kwamba nitazuiwa kuingia kwenye kikao cha Baraza la Wawakilishi hata watoto walijua .‘’ Maalim Seif Shariff Hamad alisema kisheria hatakiwi aingie kwa sababu yeye siyo mjumbe wa baraza hilo na anachotakiwa ni kupatiwa mwaliko tu.
POROJO NA BWABWAJA LA SHEIN.Shein akizungumzia kutoka nje kwa wajumbe na mawaziri wa CUF, alisema atii  haikuwa mwafaka hasa kwa kuzingatia hoja waliokuwa wakiilalamikia haikuwa na uhusiano na muswada uliokuwa ukijadiliwa, uliohusu kupitisha matumizi ya bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016. Akihutubia baraza hilo kabla ya kulivunja jana Shein alisema, kitendo cha kususa baraza atii hakikuwa cha ufumbuzi hakikuzingatia umoja wao, SUK na maslahi ya Zanzibar na kuwataka wajumbe kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba na sheria. Shein alisema matarajio yake makubwa ni kuona wajumbe atii wanarejesha heshima kwa chombo hicho ikiwa ni pamoja na kutimizia matarajio ya wananchi ili waendelee kushuhudia maendeleo  ((maendeleo ya domo tupu labda)) na ufumbuzi wa matatizo yao((miaka 50 na usheiya ufumbuzi hamujaupata tu CCM..?)).Alisema pia kuwa SMZ itahakikisha kila mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura, anapewa haki yake na kuwataka atii wanasiasa wasiwapotoshe wananchi juu ya haki ya raia ya kuchagua na kuchaguliwa, na badala yake atii waiacha Tume ya Uchaguzi ifanye kazi yake.((ifanye kazi yake au ifanye ukiritimba wake ili wewe ubaki madarakani kwa miaka mitano mengine ili utamalize kutuuza kwa Masultani wako wa Kitanganyika Wakoloni Weusi Tanganyika..??))
Hata hivyo, Shein alisema ni wajibu kwa kila mtu kuheshimu sheria ((wewe mwenyewe hufuati sheria unawafunga watu jela bila ya hatia unawapa watu urai wasio Wazanzibari baya zaidi Uchaguzi 2010 huku shinda kwa nini ukakubali kama sio mvujifu wa sheria..)) na kutoa ushirikiano kwa Tume ya Uchaguzi na kuhakiksiha Zanzibar inakuwa na uchaguzi huru na wa haki,((mawee wambiye basi wasiandikishe watoto na mamluki katika kambi za jeshi wambiya basi wasiandikishe watu mara mbili mbili wambiye basi wawaondowe walio vaa ninja na wawache kuwatisha wananchi kama kweli unataka uchaguzi wa huru na haki)) huku akijidai kuonya kuwa serikali yake haitasita kumchukulia mtu yeyote za kisheria ili kulinda amani ya wananchi wake.((wewe unamuonya nani hapa hii nchi sio yako hata kama Mkoloni Mweusi Tanganyika kakuweka na kukulinda hii ni nchi ya Wazanzibari na Wazanzibari hawakukupigia kuru wewe 2010 au ushasahau...?? unajidai unalinda amani ya wananchi ni wananchi gani hao unao sema wewe maana kama ni Wazanzibari hakutaki ilaa kama unalinda faida anazo pata Mkoloni Mweusi Tanganyika toka alipotunyanganya nchi 1964 sawa lakini usijidai unalinda wananchi wewe ndio uliye wasafirisha Masheikh wakafungwe jela huko Tanganyika kisha unajida unalinda wananchi au hao wahafidhina wenzio mnao ibaa pamoja na kuwauwa na kuwakandamiza Wazanzibari.))
 Akizungumzia Muungano feki wa Tanganyika na Zanzibar, Shein alisema mapendekezao ya Katiba inayopendikizwa atii itafungua mlango mpya wa uchumi kupitia uchimbaji wa nishati ya mafuta na gesi na kuwataka wananchi kujitokeza wakati wa kura ya maoni wakati ukifika.((wewe kweli kipofu shein hivi bado unadoto kuwa hilo katiba la wazi wa ESCROW Wazanzibar Watalikubali...?? ))Kabla ya kulivunja baraza,  Sheina alielezea atii mafanikio ya Serikali yake katika miaka mitano iliopita katika sekta ya miundombinu, anga, kilimo, utalii, uvuvi na uwekezaji na kueleza maeneo hayo yalioanishwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM yalielezwa kwa upana wake.((tumeona maendeleo siunajenga mnara Kisonge hahahaha)) Shangwe ndani ya ukumbi huo iliibuka baada ya Spika, Pandu Ameir Kificho kuwatambulisha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Firauni Jecha na Mkurugenzi wake, Firauni Kasim Ali na wajumbe wa baraza hilo kuchukua muda mrefu kupiga makofi. Viongozi walioalikwa kuhudhuria hafla hiyo ni pamoja na mabalozi wadogo wa India, Italia, Uingereza, China na Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya UNDP, UNFPA, Unicef, WHO, ILO, wakiwemo wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama, viongopzi wa dini, wanasiasa na Naibu Msajili wa vyama vya siasa Zanzibar, Rajabu Baraka

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment