Friday, June 5, 2015

VIDEO-BILAL ASEMA AKIWA RAISI ATAIMARISHA UTAWALA WA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU. BINADAMU GANI HAO......? WALE MASHEIKH SIO BINADAMU....? WEWE NI MAKAMO WA RAISI NINI UMESEMA KUHUSU UDHALILISHWAJI WALIO FANYIWA...????



Nchini Tanganyika Giningi Dodoma. Makamu wa Rais wa nchi ya Tanganyika, Bilal amesema nchi inaendelea kupoteza maadili, hivyo kuahidi kusimamia uwajibikaji katika sekta ya umma endapo atapitishwa na CCM na kisha kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo ya Tanganyika katika Uchaguzi Mkuu ujao.((usijali baba utapitishwa na CCM huu ni mpago kamili toka kesi yako na Komando wa udongo alivotaka kukupa Zanzibar mukapingwa na chini mkakasirika ukatulizwa na umakamo wa urais wa nchi ya Tanganyika Kikwete akakuweka benchi ukae kimya ili sasa aje akuweke katika urais wa nchi ya Tanganyika sisi tunajuwa michezo yenu munayo icheza.))  Akizungumza baada ya kuchukua fomu ya kuomba kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo, Bilal alisema Serikali yake haitavumilia uvunjwaji wa miiko ya uongozi.((sasa hiyo miaka kumi ya kuwa makamo ilikuwa sio serekali yako sasa umakamo wa kazi gani basi...? acheni kufanya watu kama ni watoto wadogo nyinyi vichwa maji.))  Huku akisisitiza kuwa kaulimbiu yake, ni mabadiliko ndani ya umoja,((umoja upi....? wa hao mafisadi na wizi wa mali za umma na wala hawapelekwi mahakamni wanabadilishwa vyeo wakisha ibaa sana ili wakaibe kwengine.))  

NIMEONA NIKUWEKE NA HIZI PIC BILAL LABDA HUNA HABARI HAKI ZA BINADAMU SIO ANZA NA HAWA BASI SI NI MAKAMO WEWE WA RAISI
Bilal alisema vipaumbele vyake ni kusimamia matumizi mazuri ya rasilimali za Taifa na kuboresha na kusimamia matumizi ya mapato.((sasa haya yote hukuweza kuyafanya wakati wewe ni makamo wa raisi ila utayafanya ukiwa raisi nauliza tena faida yake nini basi huo umakamo...?)) Alitaja kipaumbele kingine kuwa ni kulinda haki za binadamu na kuhakikisha nchi inasimamiwa kwa misingi ya sheria “Nitahakikisha Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea, kusimamia na kuimarisha utawala wa sheria, haki za binadamu,.((haki za binadamu haaa wapi niaze oh yaaa labda huna habari kuna Masheikh kama 26 au 32 walikuja kuchukuliwa nchini Zanzibar nchi nyengine wakasafirishwa kinyemela na kuishia katika majela ya nchi hiyo ya Tanganyika ambayo wewe ni makamo wakathalilishwa na wewe ni makamo wakateswa na wewe ni makamo na mpaka leo wanaendelea kuthalilishwa na kuteswa na wewe bado ni makamo sijuwi ni haki za binadamu gani unazo zizungumza au za kuendelea kuwalinda hao mafisadi wanao iba mabillioni kwa mabillioni maana wao ndio banadamu wengine ni....))  haki za kina mama na watoto, walemavu hasa wa ngozi,((walemavu haswa wa gozi ni lini wewe umesimama na kuwatetea na wewe ni makamo...?)) haki ya kuunda na pamoja na uhuru wa kupata habari.”((haahahahaha bora nicheke ati na pamoja na uhuru wa kupata habari))

NIMEONA NIKUWEKE NA HIZI PIC BILAL LABDA HUNA HABARI HAKI ZA BINADAMU SIO ANZA NA HAWA BASI SI NI MAKAMO WEWE WA RAISI
Bilal alisema atahakikisha analinda misingi ya utaifa ulioasisiwa na wazee na ambayo imelifikisha Taifa katika miaka 54 likiwa moja, imara, lenye upendo na mshikamano. Alipotakiwa kuwatoa hofu watu wanaodhani kuwa ana mitazamo ya kihafidhina, Bilal alisema yeye ni mwanasayansi na siku zote sayansi inabadilika kulingana na mazingira.((hahahaha ndio kubadilika kwako ukaja Zanzibar kusema wauza vinyago wote wapewe ardhi wajenge sio hahahaha)) “Hakuna uamuzi uliokuwa sahihi zaidi ya uamuzi wa kisayansi. Mimi siku zote uamuzi wangu unafuata utaratibu huo, ndivyo nilivyolelewa na kufunzwa na nitaendelea kuongozwa kisayansi,” alisema. Akijibu swali lililomtaka afafanue mtazamo wa watu kwamba sasa ni zamu ya Zanzibar kutoa Rais, Bilal alisema chama chake hakina vitu hivyo, bali kinachagua kiongozi au mwanachama ambaye ataweza kuwavusha. ((asio kuwavusha mafisadi na wizi muzidi kuwamaliza wananchi na nyinyi yenu yana kwenda vizuri kwa hiyo CCM ni kuvushana tu na kuwawacha wananchi wa kihaha na maisha maana nyinyi si mshavushana))

NIMEONA NIKUWEKE NA HIZI PIC BILAL LABDA HUNA HABARI HAKI ZA BINADAMU SIO ANZA NA HAWA BASI SI NI MAKAMO WEWE WA RAISI
“Hatujali wapi ametoka, hatujali rangi yake, hatujali kabila lake, hatujali dini yake ilimradi ni Mtanganyika. Mimi ninadhani ninaweza kulivusha Taifa hili,” alisema. Alisema amejitokeza kwa sababu anayo hamu na uwezo wa kulifikisha Taifa liwe la kutiliwa mfano. Alisema Muungano ulivyo hivi sasa si kama hapo zamani, sasa unakabiliwa na changamoto nyingi zaidi kwa hiyo ni jukumu lake kuhakikisha kuwa anashirikiana na wadau mbalimbali ili kutatua changamoto zilizopo. Hali ilivyokuwa Kabla ya kuingia ndani ya ukumbi, wakati na baada ya kuzungumzia na waandishi wa habari, Bilal alikuwa akishangiliwa na wapambe wake kila mara alipojibu swali la mwandishi au kumaliza hatua moja kwenda nyingine. Mbali na kushangiliwa wakati anaingia baadhi ya wapambe walijipanga nje ya mlango wa kuingilia jengo la makao makuu kwa ajili ya kumlaki. Alisindikizwa kwa nyimbo za hamasa za CCM na za kumpongeza. Wapambe hao na baadhi ya watumishi wa ofisi za makao makuu ya chama walikuwa wamevalia mavazi yenye rangi za chama. Baadhi ya nyimbo zilizosindikizwa na makofi ni pamoja ‘ Bilal tutamlinda na kumtetea’.


KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment