Tuesday, June 9, 2015

SHEIKH FARID NA WENZAKE WAGOMA KUSHUKA KATIKA BASI LA MAHABUSU WALIPO FIKA MAHAKAMA YA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA HAKIMU MKAZI KISUTU JIJINI DAR NCHINI TANGANYIKA.


Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho ya Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki) nchini Zanzibar, Sheikh Farid na wenzake walio bambikiwa na kesi atii ya kula njama na kujihusisha atii na ugaidi nchini Zanzibar na kusafirishwa kinyemela mpaka nchi ya jirani kwa Wakoloni Weusi Tanganyika Masheikh walmegoma kushuka kwenye basi la magereza na kuto kuingia katika mahakamani ya Wakoloni Weusi Tanganyika nchini humo jana kutokana na hatma ya upelelezi wa kesi yao kutojulikana na kupigwa dana dana. Wadhulimiiwa hao wanao endelea kudhulumiwa na Mkoloni Mweusi Tanganyika walifikishwa kwenye viunga vya Mahakama ya Mkoloni Mweusi Tanganyika Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam nchini humo Tanganyika saa 2:50 asubuhi kwa ajili kusikiliza kesi yao iliyopangwa kutajwa jana.
Kabla ya mgomo huo, wasdhulimiwa hao wanaotoka nchi ya Zanzibar, waliiomba mahakama kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa nchi ya Zanzibar kuwatembelea mahabusu kwa ajili ya kusikiliza kero zao kuhusiana na kushitakiwa kwao katika mahakama za Wakoloni Weusi Tanganyika badala ya mahakama ya nchini kwao Zanzibar. Viunga vya mahakama hiyo vilifurika askari kanzu na wenye sare za Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Magereza kwa ajili ya kuimarisha ulinzi. Hata hivyo, baada ya kufikishwa mahakamani hapo wadhulumiwa wote waligoma kushuka kwenda kusikiliza kesi yao kwenye ukumbi wa mahakama hiyo ya Mkoloni Mweusi Tanganyika. Saa 4:56 asubuhi, mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Renatus Rutatinisibwa, huku upande wa Jamhuri ukiongozwa na mawakili wa serikali, Peter Njike na George Barasa, wakisaidiana na wakili wa serikali mwandamizi, Tumaini Kweka.
Wakili Njike alidai kuwa washtakiwa wamegoma kushuka kwenye basi la Jeshi la Magereza tangu wafikishwe mahakamani hapo kutoka mahabusu. Wakili wa utetezi, Abdallah Juma, alidai kuwa upande wao hauna taarifa kuhusiana na washtakiwa kugoma kuingia mahakamani na kwamba, upande wa Jamhuri ndiyo una wajibu wa kujua chochote kuhusu washtakiwa waliopo mahabusu. Wakili Kweka, alidai kuwa askari magereza wamefanya juhudi za kuwataka washuke kwenye basi ili kuingia mahakamani lakini imeshindikana. “Mheshimiwa, Mei 25 mwaka huu, mahakama yako ilitoa amri kwamba kesi hii itatajwa leo… Jamhuri tunaomba washtakiwa wahesabike kwamba hawajafika mahakamani. Pamoja na kwamba wapo katika viunga vya mahakama, tunaomba mahakama itoe amri wapangiwe tarehe nyingine na wafike mahakamani,” alidai Wakili Kweka wa upande wa Jamhuri.
Hakimu Rutatinisibwa alisema mahakama haiwezi kuwafuata washtakiwa nje ya ukumbi unaoendesha shughuli zake na kwamba, (mahakama) inaendesha kazi zake kwa mujibu wa sheria, hivyo inaahirisha kesi hiyo hadi Juni 18 mwaka huu itakapotajwa tena. Mbali na Sheikh Farid, watuhumiwa wengine ni Noorid Swalehe, Ally Hamis Ally, Jamal, Nassoro Hamad, Hassan Bakari, Ahtari Humoud, Mohamed Isihaka, Abdallah Hassan, Hussein Mohamed, Juma Sadala, Said Kassim, Hamis Amour, Abubakar Abdallah, Salum Ali, Salum Amour, Alawi Othuman, Rashid Ally, Amir Hamis, Kassim Salum na Said Shehe pamoja na wenzao.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment