Alisema Serikali ya Awamu ya Saba chini ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein, itakuwa makini na haitovumilia kuona uchafu ukifanyika ikiwemo wa uvunjaji wa sheria na taratibu zilizowekwa na nchi.Katika hilo, aliwataka watendaji wakuu wakiwemo mawaziri kuwa makini kusimamia utekelezaji wa majukumu yao na kamwe wasitoe nafasi kuwepo vitendo vinayorudisha nyuma imani ya wananchi kwa Serikali yao.Kuhusu muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Balozi alisema mfumo wa Serikali mbili ndiyo uliokubaliwa hadi sasa na Chama Cha Mapinduzi ambacho sera zake ndiyo zilizotumika kikatiba katika kuongoza nchi na Serikali ya Umoja wa Kitaifa.“Hili nataka kulifafanua tena, mfumo wa Serikali mbili ndiyo uliokubalika na wananchi walio wengi ambapo kwa upande wetu sisi tunatekeleza sera ya Chama Cha Mapinduzi katika mfumo wa Serikali ya umoja wa kitaifa,” alisema Balozi Idd.Aidha, alikemea baadhi ya tabia za Wazanzibari kuwatimua wenzao wa Tanzania Bara ikiwemo kuwahamisha na kuwafukuza kwa nguvu kwamba ni sehemu ya vitendo vya kibaguzi ambavyo havikubaliki.Alisema Mtanzania kwa mujibu wa Katiba, anayo haki ya kuishi sehemu yoyote ya Tanzania kama ilivyo kwa Wazanzibari kuishi sehemu yoyote katika ardhi ya Tanzania Bara bila ya kubughudhiwa.
MIMI NAKUAMBIA USITULETE MAMBO YA MAPINDUZI MAANA HAYO NDIO YALIYOUTIZA ZANZIBAR UMASIKINI NA KUWAFANYA WAZANZIBAR KUKIMBIA KWAO NA KUWA WAKIMBIZI MPAKA SASA WAZENJI KIBAO NI WAKIMBIZI KWA SABABU YA MAPINDUZI UNAYOJISIFIA WEWE ZIMWI BALOZI IDD PIA USHAWAHI KUWAULIZA WAZENJI KAMA WANAUTAKA MUUNGANO HUWO WA SEREKALI MBILI AU UNANGOJEA MPAKA WATU WAJAZANE BARABARANI KUUPINGA NDIO UJUWE KAMA HAWAUTAKI..?KAMA HUNA LA KUSEMA NYAMAZA KIMYA ULE ULUWA WAKO WAKATI KUISHA URUDI BARA HUKO KAMA NI UBAGUZI MULIANZA NYINYI BAADA YA KUONA ZNZ IMEPEWA UHURU UHASIDI UKAWAINGIA NA KUIVAMIYA MPAKA LEO ZNZ INAGARANGARA KWA AJILI YA MAPINDUZI MUSITULETE HAPA HAKUNA MAPINDUZI WALA ACHARI.
No comments:
Post a Comment