Wednesday, August 3, 2011

ZANZIBAR INATAKA PESA ZA MSAADA AU UHURU WA NCHI YA Z;BAR..?

 NYOKA
Imeandikwa na Eric Anthony, Dodoma; Tarehe: 3rd August 2011 ZANZIBAR imejipatia zaidi ya Sh bilioni 122 katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka wa fedha wa 2005/2006 kama mgawo wa fedha zitokanazo na wafadhili kwa ajili ya maendeleo nchini.Aidha, serikali kwa sasa inaweka utaratibu wa namna bora ya kuhakikisha pande zote mbili za Muungano zinafaidika na fedha za misaada, mikopo na miradi kutoka nje kwa kuweka mwongozo wa ushirikishwaji wa Zanzibar katika taasisi za kimataifa.Hayo yamo katika majibu ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Hassan Suluhu aliyekuwa anajibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Msabaha (Chadema) aliyehoji sababu za misaada kutotolewa kwa uwiano na wakati mwingine kutokuwafikia Wazanzibari.Waziri Suluhu alikiri kwamba, watu wakikaa pamoja, tofauti baina yao haziwezi kukosekana.Alisema hizo ni changamoto za Muungano na kusisitiza kwamba ipo dhamira ya dhati ya kuungana na kuimarisha Muungano.Alisema, Zanzibar inapata mgawo wake wa fedha za misaada ya kibajeti na zimekuwa zikipita katika Fungu namba 31 la Ofisi ya Makamu wa Rais na kuwasilishwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.“Fedha hizi hutolewa kwa ajili ya nchi nzima. Suala la mgawanyo wa misaada hii lilijadiliwa kwa pamoja na kukubalika kwa sasa kuwa formula’ ya muda ya kugawana misaada iwe ni asilimia 4.5 kwa sasa,” alisema.Alisoma takwimu ya mgawo wa Zanzibar kwa miaka mitano kwamba katika mwaka wa fedha wa 2005/2006 Zanzibar ilipata Sh 18,651,800,000.00, mwaka uliofuata ilipata Sh 23,020,440,000.00.Aidha mwaka 2007/2008 Zanzibar ilipata Sh 27,338,623,000.00 na mwaka uliofuata ilipata Sh 23,040,964,000.00 kabla ya mwaka 2009/2010 mgawo kupanda na kufikia Sh 30,214,131,000.00

No comments:

Post a Comment