Monday, August 8, 2011

MAJENGO YA ZAMANI Z;BAR KUNA MISIKITI NA YOTE YAMEPEWA WAWEKEZAJI

PRINCESES SALME

SASA NI MAHALI PAA KITALI NA KUOWANA
Moja ya wawekezaji wa Zanzibar, wakiwemo Mtoni Marine, wanadai kuwa lile eneo lIle la palace ya zamani ya Mtoni (Mtoni Palace) aliyokuwa anaishi Princess Salme, ni yao au ni sehemu ya milki yao.

Ndani ya magofu yale, ndani yake upo msikiti mzuri sana wa kizamani. Ulijengwa pamoja na palace ya Mtoni. Inashangaza sana, muwekezaji huyu, Mtoni Marine, anadai kuwa eneo hili lipo chini ya milki yake, ikiwemo Msikiti. Na hakuna ruhusa hata kusali katika msikiti huo, hata kwa dharura. Mambo hayo.Msikiti mmoja mzuri sana, mkubwa kiasi — upo ndani –sehemu ya majengo ya gofu la palace, Mtoni.
SMZ-GNU inalijua hili, lakini hawataki kulisemea wala kudai haki –sio tu haki ya Wazanzibari; bali hata haki ya dini yetu ya kiislamu: wako tayari waone dhulma inafanyika, so long, wanabaki madarakani kwa njia ya utulivu!
Mnasema, mimi nimefanya nini? Msikiti huu tumeshaudai, na Jumuiya ya Uamsho na Mihddhara Zanzibar (UAMSHO) wamedai na madai yetu yapo serikalini, lakini pia tulikwenda pale kusali na kuadhin kwa sauti kubwa sana, mpaka wenye milki ya hoteli walitaharak.
Sisi hatukusubiri SMZ-GNU wala Balozi Seif Idd kwenda kusuluhisha, sulhu amabzo hatuoni matokeo yake, sulhu BUTU.
Tumeamua na takriban msikiti uko mikononi mwa waislamu, then, tutauchukua tu.
Hawa ndio aina ya wawekezaji waliopo Zanzibar. Wanachukua mpaka msikiti, wao wanautumilia na kupata pesa.
Kisiwa cha Chumbe wanafanya hivyo. Upo msikiti pale mkubwa – wao walikuwa wanakataza hata watu kusali mle na hususan wavuvi na waliopte anjia (ambalo hasa ndio ilikuwa lengo la kujengwa msikiti ule).
Tulipiga kelele miaka ile ya 90s, sasa at least nafuu kidogo. Sisi wengine tukiwezeshwa, tunaweza….na tukiamua,tumeamua ..hatusubiri CCM wala CUF wala GNU.
Basi hata msikiti au misikiti inakuwa sehemu ya hoteli au inafikiriwa kufanywa madanguro.Hatuoni aibi hata ya kukashifiwa kwa dini yetu eti tunakuza utalii.
Jana nimeuliza swali: ikiwa mpaka sehemu z akihistoria tunaziuza, hao watalii watapokuja Zanzibar, watakwenda kuangalia nini? Moja ya utamaduni wetu na sehemu yetu kubwa ya kihistoria ni UISLAMU, UJIO wa Uislamu, na Utamaduni wa kiislam. OK, leo msikiti mmewakabidhi wataliana…itakuaje?
Kama yupo anaishi hapa zanzibar au maeneo ya Mtoni, aende pale akaangalie…..upo msikiti mle ndani. Nafikiri wengi wenu hamlijui hili.
Wafalme (walikuwa watu wabaya sana) lakini walijenga msikiti japokuwa mdogo kila palace. Ingia pale People’s palace, au skuli ya Forodhan, au palace ya Kibweni n.k…utayaona hayo. Haya hatuyaoni, ila tunaona masnamu ya Anglican Church, masanamau ya kutengenezwa…masnamu ya bandia.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi. Hakiiiiii. GNU Oyeee!

No comments:

Post a Comment