Monday, August 1, 2011

WANANCHI ENDELEANI KUFAA VIONGOZI WASTAAFU KUNUFAIKA ZANZIBAR

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema inatarajia kutumia Sh Bilioni 9.9 kuwahudumia viongozi wake wakiwemo wastaafu kwa kuwalipa pensheni na safari za nje katika Mwaka huu Fedha.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Uchumi Omar Yussuf Mzee, Wakati akifunga mjadala wa Bajeti yake katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea katika mji wa Chukwani mjini Zanzibar.Alisema kwamba kati ya fedha hizo Sh Bilioni 4.4 zitatumika kwa Safari za nje kwa viongozi wa kitaifa wa Serikali pamoja na viongozi wake wastaafu Zanzibar.Aliwataja viongozi watakao nufaika na kasma hiyo kuwa ni marais wastaafu ambao ni Ali Hassan Mwinyi, Dk Salmin Amour Juma, Amani Abeid Karume, naa Aboud Jumbe Mwinyi.Aidha aliwataja mawaziri kiongozi wastaafu kuwa ni Ramadhani Haji Faki, Dk Mohammed Gharib Bilali na Waziri wa Mambo ya ndani Shamsi Vuai Nahodha.
Hoja yangu ipo hapa.Ukiangalia kwanza viongozi hawa wameitumikia serikali ya jamuhuri ya muungano takriba wote,kwanini wapatiwe budget hii wakati katika serikali ya jamuhuri ya muungano inawawapitia budget yao ?Na kwanini waekewe budget hii hali yakuwa hawana tena uwongozi na hawahitajiki tena kwa wakati huu kwa sababu wao muda wao umemaliza ispokuwa wanahitajika kulipwa malipo yao ya kawaida kama mishahara yao tena kwa kiwango flani kutokana wameitumikia serikali kama ni viongiz wa staafu.
Ukiangalia tena hao viongozi walitajwa hapo juu wengine bado wanaitumikia serikali ya jamuhuri ya muungano,sasa hivi leo hii hi wapatiwe budget yao ya nje haliyakuwa wanatumikia serikali ya jamhuri ya muungano mambo haya vipi na mbona yako hapa znz nchi nyengine husiki ? Inamana siasa zao za kitanganyika zitumike pesa zetu kwa kuwahudumia viongozi hawa ?Ukiangalia Nahoza waziri wa mambo ya ndani ambaye alikowa waziri kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar,ameshatengewa budget yake wakati huko Tanganyika anafanya kazi zao na ana budget vile vile na leo tumuekee budget ?Ukiangalia waziri huyu katika utendaji wake wa kazi kama muakilishi basi hawawakilishi wananchi wa jimbo lake ipasavyo kutokana na vyeo vyake viwili vipi leo apewe budget ambayo inaingiliana na mambo ya muungano ?
Haya Dr Gharib Bilal makamo wa muungano,alikuwa waziri wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar lakini sasa yupo makamo wa muungano vipi leo atengewe budget yake kwa ziara zipi ambazo atakazo fanya kwa Zanzibar kupitia serikali yetu kuipa faida zaidi ya budget tulio mpangia ? Huyu tuseme hana Budget yake katika serikali ya muungano wa Tanzania ?Tukija sasa kwa marais wastaafu,Mwinyi au mzee kondom,alikuwa Rais wa muungano na pia kaitumikia Zanzibar kama rais jee kwa nini apatiwe budget mbili ambazo ndani ya Zanzibar na Tanganyika ?Mh Jumbe nae alikuwa makamo wa rais ya muungano na alikuwa rais wa Zanzibar vipi leo apatiwe budget zanzbar at the same time na Tanganyika kuna budget ?Dr Salmini Amour nae ametumikia Tanzania/ Tanganyika na huku akiwa rais mtaafu wa Zanzibar vipi nae budget yake vipi ?
Kwa kweli mimi sitoongelea sana katika haya na hao viongozi wengine,hiii budget kama mimi ni muakilishi siipitishi hata uninyonge kwa sababu haina ulazima wowote kwa wastaafu hawa hali yakuwa wananchi wanakufa na njaa na hawana pahali pa kuishi vizuri.wakati hawa maraisi wastafu kila moja ana nyumba zaidi ya tano na mashamba na mabiashara kila mahali na bado tunawawekeya mipesa mengine na hali tunajuwa kuwa kunawatu hata mkate hawana.na pia kutokana na kukosekana huduma muhimu kuliko hizi ziara za viongozi.Ipo haja ya kupinga Budget hii na ikiwezekana kama katiba yetu inasema matumizi haya ni lazima basi yatolewe ili kuweza kupunguza matumizi ambayo serikali yetu inakuwa ni mzigo mkubwa,ukiangalia uchumi wetu ni mdogo.Kuna mambo mengi ya huduma za wananchi kama hospital na elimu,na kama fedha hizi tungelizitumia basi tungelipiga hatua zaidi kuliko kuzitumia kwa viongozi hawa ambao wameshapita muda wao na sio lazima matumizi haya kwao tena.Hapa mimi naona kuna mchezo ambao unachezwa na viongozi wetu katika matumizi haya,lazima viongozi mulifikirie hili kwa kina sana juu ya budget hii munayotaka kuipitisha.

No comments:

Post a Comment