MAKADA WA CCM NA FITINA ZAO
BAADHI ya makada wa CCM na maofisa wa chama hicho Visiwani Zanzibar wanadaiwa kuandaa mkakati wa siri wa kudhoofisha Utendaji wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar , Amani Abeid Karume. Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya CCM kinaeleza kwamba tayari makada hao kwa kushirikiana na maofisa waandamizi wa CCM Visiwani hapa wameanza kutayarisha mkakati wa kutokumpa ushirikiano makamu mwenyekiti wao, Karume kwa kisingizio chsa kutofurahishwa na Wajumbe wa Sekretarieti.Wiki iliyopita, katika kikao chake,Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar ilipitisha Wakuu wa Idara za Chama hicho kwa upande wa Zanzibar, Haroun Ali Suleiman aliongoza Idara ya Uhusiano wa Kimataifa, Machano Othman Said,Idara ya Oganizesheni, Issa Haji Ussi,Idara ya Itikadi na Uenezi na Mansoor Yussuf Himid, Idara ya Fedha na Uchumi.Habari zaidi zilieleza kwamba mpango huo utatekelezwa kwa kuyatumia baadhi ya matawi ya CCM katika Mkoa wa Mjini Magharibi na Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kuwandaa baadhi ya wanachama kupinga uteuzi wa sekretarieti mpya na pia kutumia suala la mafuta na gesi asilia kisiasa.Mmoja wa viongozi wa Jimbo la Kiembesamaki ambaye hakupenda kutaja jina lake gazetini kwa maelezo sio msemaji wa CCM alisema juzi kwamba makada na maofisa wa CCM walifika tawini kwao kuwashawishi kutomuunga mkono Makamu Mwenyekiti Karume na baadhi ya Wajumbe wa NEC.Hata hivyo, watu hao walikumbana na ugumu baada ya viongozi wa matawi ya jimbo hilo kuwakatalia wakisisitiza wao bado watiifu kwa CCM na viongozi wake na kwamba wasingependa kukivuruga Chama.
Taarifa zaidi zinaeleza kutokana na majibu hayo, makada na maofisa hao walikwenda Jimbo la Mji Mkongwe kufanyakazi kama hiyo, ambayo haikuzaa matunda.Makada na maofisa hao wa CCM wanatetea suala la mafuta na gesi asilia lisiondolewe kwenye orodha ya mambo ya Muungano jambo ambalo linakwenda kinyume na uamuzi wa Baraza la Wawakilishi wa kuitaka Serikali kuliondoa katika mambo ya Muungano.
Ilielezwa kuwa chini ya mkakati huo Wana CCM hao watawashutumu Mawaziri wa SMZ, Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati, Ali Juma Shamuhuna na Waziri wa Kilimo na Maliasili, Mansoor Yussuf Himid kwa misimamo yao katika kutetea maslahi ya Zanzibar hasa suala la mafuta na gesi asilia libakie katika usimamizi wa Zanzibar.Habari zaidi zinasema kuwa makada na maofisa hao wa CCM watapita katika baadhi ya matawi kushawishi wanachama kutokuwa na imani na viongozi hao kwa kisingizio cha kulinda muundo wa Muungano wa Serikali mbili.Chanzo chetu cha habari kinasema ikiwa mpango huo utafanikiwa wana CCM hao watakuwa wamefanikiwa katika mkakati wa kukivuruga Chama na hususan kumwekea taswira mbaya Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume ambaye ni Makamu Mwenyekiti wao kuwa amekiua Chama.
Makada na maofisa hao wa CCM wanafahamika kwa misimamo yao ya kupinga suala zima la Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar ambao tangu awali walikuwa wakifanya kampeni za chini kwa chini kuwashawishi watu kukataa Serikali ya SUK.Katika vikao vya Baraza la Wawakilishi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilisisitiza kuliondoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano ambapo Waziri Shamuhuna aliweka bayana hatua za utekelezaji wa utafutaji na uchimbaji wa mafuta bila kuihusisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .Juhudi za kumpata Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Vuai Ali Vuai kwa jana zilishindikana kwa kuwa muda mrefu alikuwa katika vikao vya Kamati Kuu.
SEREKALI INAWAJUWA HAWA WATU NA NDIO MABAKIYA WANAMAPINDUZI WALIYO UWA WAZANZIBAR 1964 LAKINI LAJABU SEREKALI INAWAWACHIYA HAWA WATU NA FITINA ZAO MPAKA LAKUTOKEYA LITOKE KAMA 1964 SIOMBEI MABAYA ILA WASWAHILI TUNAMSEMO USAMAO TAHATHARI KABLA YA ATHARI NA HAWA WAMO KUTIA FITINA HUKU NA KULE NA SEREKALI INAWAJUWA KWANINI HAIWATI BARONI NA KUWAFUNGULIA MASHATAKA..?AU MUNASUBIRI TENA ULE MSEMO WALIYOSEMA WAKATI ULE WAPINDUWE KWANI KISAHANI CHA CHAI HICHI KISHA WALIPO PINDUWA WAO VIONGOZI WAKAKIMBIA SISI RAI NDIO TULIYO ULIWA NA KUCHINJWA KAMA KUKU NA DADA ZETU KUOLEWA NA MAGOVI KWA LAZIMA SASA HAYO YANAA ANZA TENA WATU KIMYA WANAWAWACHIYE TU MPAKA LETOKE LAKUTOKEA SIO.......?
No comments:
Post a Comment