Allah amesema ‘’ Hakika wanao amirisha misikiti ya Allah ni wale wanao muamini Allah, na Siku ya Mwisho, na wakashika Sala, na wakatoa Zaka, na wala hawamchi ila Allah. Basi huenda hao wakawa katika waongofu’’ {Quran 9:18}
Pia Allah amesem ’’Katika Nyumba ambazo Allah ameamrisha zitukuzwe na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni’’ {Quran 24:36}[Wanazuoni wame tafsiri ayah ii wanasema wale wanaojenga au kusaidia kujenga au kuziweka kwenye hali ya matumizi]Mtume Muhammad {SAW} alisema “Wale ambao watajenga msikiti kwa ajili ya Allah, basi Allah atawajengea nyumba kwa yao peponi”"{Bukhari}Ujenzi wa Msikiti Mustaqim ambao ndani yake kutakuwa na Madrasa inshaallah umefikia kutokana na michango ya Waislamu mbali mbali Wanawake na Wanaume walio Zanzibar na nje ya Zanzibar. Tunapenda kutoa shukrani za dhati Inshaallah Allah awalipe kwa wingi. Hatukuwa na kuweka majina ya wale ambao wamechangia kwa sababu wengi wameona itaharibu usiri wa sadaka zao. Nia yetu ilikuwa Masjid iwe tayari kwa ajili ya Ramadhan lakini hatujafanikiwa kuukamilisha kwani michango imekuwa hafifu bado tuna tunataka kuunganisha maji ama kutoka mains na kuchimba kisima na vyoo bado havija kamilika. Sehemu ya Kutilia udhu bado ipo chini ya ujenzi. Inshaallah fittings ya umeme na plaster itakamilika mwisho wa wiki ya tarehe 19/08. Madirisha yamekuwa donated tayari ya Aluminium kutoka dar yatafika mwisho wa wiki, Kinachofuata ni rangi mkono wa mwanzo inshaallah. Milango pia Alhamdulillah inachongwa Zanzibar na ni karibu kumalizika. Kwa sasa tunahitaji saruji, mchanga, changarawe (kokoto),fedha taslimu, mazulia ya msikiti na vitu vyengine vya ndani ya msikiti. Juu hatuanza enjenzi mpaka tukamilishe chini. Tafadhali tuchangie kuijenga nyumba ya Allah na sisi atatujengea nyuma peponi kama alivyo ahidi Mtume SAW. Hakuna kidogo hata kama utaamua kuleta vifaa inshaallah tutapokea.Michango kwa Zanzibar tafadhali WasilianaMr Salum Toufiq (Lawyer & Zantel Legal adviser) +255 774 412 060 {Mrs Toufiq} Mrs Talha Masoud (Construction Engineer & Zanzibar Ministry of Health Project Manager)+255 777 417 847.
Michango kwa United Kingdom wasiliana na Ustadh AbdulMalik +447534998494
Amina ishaAllah hii ni njia bora na ya kuigwa kwa waislam sote na mie Mola anaijua nia yetu,,
ReplyDeletetusikimbilie kuongeza wake tu kuna njia kama hii ni bora zaidi