Wednesday, May 27, 2015

KESI YA MASHEIKH DANADANA-NYERERE JUU YA UBAYA WAKE ZAIDI YA WAZANZIBARI NA NCHI YAO YA ZANZIBAR ALIWAPA HISHIMA KIDOGO MASHEIKH SHEIN NA KIKWETE MNAWAFANYA NINI MASHEIKH.....???



LINA FAIDA GANI KUITWA MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR IKIWA HALITUMIKI BORA TU WAPE WATU WASIO NA UWEZO WA KUKODISHA MADUKA WAUZIE UROJO NA MANDAZI

Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho wakiongozwa na askari wa magereza katika viunga vya mahakama ya Mkoloni Mweusi Tanganyika ya Kisuta, jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika

KIONGOZI wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu nchini Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed (45) na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya kubambikiwa na Mkoloni Mweusi Tanganyika atii ya ugaidi wakati watu wanadai nchi yao ya Zanzibar hawaataki tena Muungano feki, wamesema upande wa Jamhuri unachelewesha kesi hiyo kwa makusudi. Washitakiwa hao walidai hayo jana baada ya upande wa Jamhuri kudai, upelelezi wa kesi hiyo upo katika hatua ya mwisho, lakini wanashindwa kuendelea kutokana na rufaa waliyoikata katika Mahakama ya Rufani. Upande wa Jamhuri umekata rufaa hiyo kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya jiji la Dar es Salaam nchini Tanganyika kwa Makaburu Weusi ulioitaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza hoja za washitakiwa na kuzitolea uamuzi.Kupitia wakili wao, Abdallah Mohamed washitakiwa hao walisema kuwa sababu wanazotoa upande wa Jamhuri, siyo za msingi kwa kuwa rufaa hiyo haihusiani na kukamilika kwa upelelezi huo. Alidai wanachofanya upande wa Jamhuri ni kupoteza muda wa mahakama na kuendelea kuwaumiza washitakiwa ambao hawana hatia, hivyo aliiomba mahakama izingatie sheria. “Kama wanaona washitakiwa hawana kesi ya kujibu muhimu wawaachie huru na endapo watabaini kuna mashitaka dhidi yao wawakamate tena,” alisema Wakili Mohamed. Kuhusu afya za washitakiwa, alisema washitakiwa bado wanaendelea kuumwa, na hawezi kusema wanachoumwa lakini Abdallah Said sehemu zake za siri zimevimba na hawalilaumu Jeshi la Magereza kwa kuwa linajitahidi kuwahudumia lakini hawana dawa za kutosha. Aliomba mahakama iruhusu ndugu zao wawatibu kwa kuwa hata dawa wanazoandikiwa wananunuliwa na ndugu zao. Hakimu Mkazi, Renatus Rutha aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 8.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment