MZEE MOYO AKIMUONYESHA PIC YA KUMBUKUMBU MUANDISHI SIKU SHEIN ALIYO SHINDWA UCHAGUZI NCHINI ZANZIBAR.
Mwanasiasa mkongwe aliyevuliwa uanachama wa CCM, Mzee Hassan Nassor Moyo (80) amesema yeye ndiye aliyefanya kazi kubwa, usiku kucha, kumshawishi Maalim Seif Sharrif Hamad, aliyekuwa mgombea urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya CUF, akubaliane na matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 kabla ya hata kutangazwa.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake Tanga siku chache baada ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Magharibi, Unguja nchini Zanzibar kumvua uanachama, Moyo alisema alitumwa na Rais Amani Abeid Karume kufanya kazi hiyo kwa bidii, utiifu na uadilifu hadi akafanikiwa.
Moyo alisema kuwa Mohamed Riyami, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Maridhiano, alikwenda nyumbani kwake na kumpa ujumbe huo kutoka kwa Rais Karume, na baada ya majadiliano naye, alikubali. “…Ni kweli Mohamed Riyami alikuja kuniamsha saa 10:00 alfajiri hivi akisema ametumwa na Rais Karume aje aniambie nikamwombe Maalim Seif aridhie matokeo ya uchaguzi mkuu yatakayotangazwa,” alisema Moyo.
“Nilimuuliza Riyami tena, nikamwambie nini Seif....?? Akaniambia utajua wewe. Nikamwambia au ndo tumeshindwa....?? Riyami akatabasamu tu!!!
HII NDIO SIKU SHEIN ALIYO KATALIWA NA WAPIGA KURA WA NCHI YA ZANZIBAR 2010 SIKU ALIYO SHINDWA KATIKA UCHAGUZI HUU WA 2010 KAMA UNAVYO MUONA YUMAJIIiiii
“Kwa hiyo, nilikwenda kuzungumza naye. Nilimwambia wewe (Seif) umezoea kushindwa na mimi (CCM) nimezoea kushinda, kubaliana na matokeo,” alisema.
Alipoulizwa kama ni kweli maneno hayo tu ndiyo yalimlainisha Maalim Seif aridhie matokeo hayo, Moyo alijibu; “Hapana, nilizungumza naye kwa kina historia ya mabadiliko, tulikotoka, kufikia kuundwa kwa kamati za miafaka mpaka sasa, naye alikubali.”
Baada ya kukubaliana, Moyo alisema kuwa Maalim Seif alikwenda kuwaambia vijana wake waliokuwa kwenye kituo cha kuhesabia kura katika Hoteli ya Bwawani waondoke, na baada ya vijana wake kuondoka, Tume ya Uchaguzi ya nchi ya Zanzibar (ZEC) ikatangaza matokeo yaliyompa ushindi Dk Ali Mohamed Shein.
SHEIN AKISHEREHEKEA USHINDI WA KUPEWA KAMA UNAVYO MUONA YEYE SHEIN NA MKEWE KWENYE SURA ZAO WAKIJITAHIDI KUJICHEKESHA LAKINI NDANI YA MOYO WANAJUWA KUWA WAMESHINDWA FETHEHA INAWALA NDANI KWA NDANI.
Hata hivyo, Moyo alikataa kuweka wazi kama hatua yake kwenda kwa Maalim Seif ililenga kumshawishi akubali kushindwa wakati matokeo yalionyesha ameshinda. Pia, hakutaka kuweka bayana kama wakati anakwenda kwa Seif alikuwa anajua matokeo.
Alipoulizwa kama atakuwa tayari mwaka huu kutumwa tena kwenda kumshawishi Maalim Seif akubaliane na matokeo, alisema:“Hapana. Sithubutu. Hapa inatosha.”
Aidha, Moyo amewashauri wanaCCM wasimbeze wala kumdharau Maalim Seif.“Watu wajiulize, miafaka mingapi ilifikiwa nchini Zanzibar, lakini haikutekelezwa....?? Mwafaka wa sasa uliowezesha kufanyiwa marekebisho ya Katiba na kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni matokeo ya mchango wa Maalim Seif na Rais Karume.”
Awaonya CCM
Pia, amewataka wana-CCM kujifunza historia ya chaguzi zilizopita kuanzia ule wa mwaka 1963 ambao ASP ilijinasibu kuwa itashinda na ikapeleka hivyo ujumbe kwa Mwalimu Julius Nyerere wa nchi ya Tanganyika, lakini muungano wa ZNP (Zanzibar Nationalist Party) na ZPPP (Zanzibar na Pemba People’s Party ndio ulishinda.
“Lakini historia ya leo inaonyesha Pemba nzima iko chini ya CUF, CCM haiko kule iko Unguja tu ambako CUF imeanza kushinda viti. Tunatumia sana hisia kwamba tutashinda, dhana hii ni potofu,” alisema.
“Na mwaka huu CUF wanapata nguvu zaidi kwani wanaungwa mkono na vijana wanaotaka misingi iliyoasisiwa na Afro Shiraz Party ya kupinga ukabila, rangi na udini; vijana ambao wanapigania nchi ya Zanzibar iwe na mamlaka yake.”
Alipoulizwa kuwa haoni kwamba alifanya kosa kuhudhuria na kuhutubia mikutano ya hadhara ya CUF, alijibu kuwa hakwenda kama mwana-CCM bali alialikwa kama mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano na kwamba CCM hawana kawaida ya kumwalika.
Mzee moyo na hakma zake
Pia, alipoulizwa anawaambia nini waliomfukuza, Mzee Moyo alijibu: “Sina cha kuwajibu kwa sababu daima mwanasiasa hupaswi kuongeza maadui bila sababu za msingi. Wao hawanitaki basi na wala sina mpango wa kujiunga na chama chochote cha siasa.”
Mzee Moyo ni kati ya waasisi wawili wa Muungano feki wa Tanganyika na Zanzibar ambao wako hai, mwingine akiwa rais wa zamani wa nchi ya Zanzibar, Alhaji Aboud Jumbe.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
No comments:
Post a Comment