“SHEIKH (Mselem) kafanyiwa udhalilishaji mkubwa wa kuachwa uchi wa mnyama huku amening’inizwa kwa pingu.”huku hawa wawili ndio atii maraisi atii wanaswali
“Huyu ni Sheikh anayesoma kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu, akisikika akisoma Qur’an tukufu katika Redio nyingi Afrika Mashariki, lakini anafanyiwa ushenzi kama huo”
MAKANZU NA MAKOFIA MAKUBWA LAKINI NINI WANAWAFANYIA VIONGOZI WA DINI
-Sheikh Farid Hali za watuhumiwa atii wa ugaidi mbaya. Hivi sasa baadhi yao wamegoma kula.Ni katika hali hiyo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika, imeambiwa isubiri kupokea maiti za watuhumiwa hao, ikiwa hatua za mahimu hazitachukuliwa kunusuru afya zao ndani ya gereza la Segerea.
Kauli hiyo imetolewa na Sheikh Farid Hadi Ahmed, mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wakoloni Weusi Tanganyika nchini Tanganyika hiyo anayesikiliza kesi yao ya kubambikiwa, Renatus Rutta, Jumatatu wiki hii.Sheikh Farid Hadi Ahmed akimpa Hakimu histori fupi ya kesi yao iliyopo mbele yake, alisema kuwa, wamebambikiziwa kesi ya ugaidi kwa kudai nchi yao huru ya Zanzibar na kusema mfumo wa Muungano uliopo hawautaki. Alisema, kesi yao ni ya kisiasa na si vinginevyo na kwamba, walikamatwa na kuletwa nchini Tanganyika kuja kudhalilishwa tu na polisi wa kike na wakiume.Sheikh Farid alimtambulisha Hakimu huyo kuwa wao ni Viongozi wa Taasisi mbalimbali na yeye akiwa ni kiongozi Umoja wa Mihadhara na Sheikh Mselem Ali Mselem ni kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, zote za Zanzibar.
“Sheikh Kama huyu (Mselem) kafanyiwa udhalilishaji mkubwa wa kuachwa uchi wa mnyama huku amening’inizwa kwa pingu, huyu ni Sheikh anayesoma kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu, akisikika akisoma Qur’an tukufu katika Redio nyingi katika Afrika ya Mashariki, lakini anafanyiwa ushenzi kama huo” Alisema Sheikh Farid mbele ya hakimu huyo.
Naye mshitakiwa Salum alimkumbusha Hakimu Rufaa kuwa wiki iliyopita Na Bakari Mwakangwale aliahidi kuwa atafuatilia hali zao gerezani na kuhoji mbona hawakumuona....?? Alisema yeye ni moja wa waliodhalilishwa na Polisi kwa kutiwa chupa na majiti, lakini alisikitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe ambaye alisema hawajatendewa chochote huku akijua sio kweli. Awali, kabla ya kupanda kizimbani watuhumiwa hao wa kesi za kubambikiwa, siku ya Jumamosi wiki iliyopita, zilienea taarifa kuwa watuhumiwa atii wa ugaidi katika Gereza la Segerea wamegoma kula.Wakati taarifa hizo zikitoka, taarifa nyingine zilibainisha kuwa mmoja wa watuhumiwa hao aliyetajwa kwa jina la Said, anaumwa jambo ambalo limeilazimu Kamati ya Maafa ya Shura ya Maimamu kupambana kutaka kusimamia matibabu yake.Sheikh Farid, ambaye ni Amir wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar, alisema Mahakamani hapo kuwa kuna watuhumiwa wamegoma kula huku wengine wanne hali zao kiafya zikiwa sio nzuri kiasi cha kuhifadhiwa katika chumba maalum.Kulingana hali hiyo Sheikh Farid, aliiomba Mahakama kufika katika gereza hilo kuangalia hali halisi ya watuhumiwa hao ili hatua stahiki zichukuliwe.
“Tunaiomba mahakama kuja kule gerezani mjionee hali halisi, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa, vinginevyo subirini kupokea maiti na muingie katika historia ya Zanzibar.” Alisema Sheikh Farid Mahakani hapo bila kufafanua zaidi.
Askari Magereza ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, alikiri kuwepo kwa hali hiyo kwa watuhumiwa hao walio bambikiwa kesi ya ugaidi baada ya Hakimu wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika anayesikiliza kesi hiyo Renatus Rutta, kupokea maelezo na taarifa hiyo ya Amir Farid Hadi na kumuhoji askari huyo.
Hakimu alimtaka Ofisa wa Magereza aeleze ni kwa nini watuhumiwa hao watatu hawakufika mahakamani. Afisa huyo aliieleza mahakama kuwa wameshindwa kufika kutokana mgomo na wametoa masharti kuwa wanahitaji Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Zanzibar na wa Tanganyika pamoja na Jaji Mkuu, wawatembelee huko gerezani.Watuhumiwa ambao hawakuweza kufika ni Said Amour, Salum na Said Shehe, Sharifu na Abdallah Hassani Hassani.Hata hivyo Sheikh Farid Hadi Ahmed, ambaye ndiye mshitakiwa namba moja alimweleza Hakimu yale wanayohitaji na kumwambia, washitakiwa watatu ambao hawakuweza kufika mahakamani ni kwa sababu ya mgomo na wengine hawakuweza kufika kwa maradhi.
Hakimu Rutta alipofanya juhudi za kuwasihi waliohudhuria mahakamani hapo kuwasihi waliogoma waache na kumtaka Sheikh Farid awafahamishe kwamba waje mahakamani, jibu la Sheikh Farid lilikuwa kwamba wenzao wameanza na wao watakwenda kumaliza kwa kuwa lao ni moja.Akiongea na gazeti la An-nuur kufuatia taarifa za watuhumiwa hao kugoma kula gerezani na wengine kuugua, Katibu wa Kamati ya Maafa ya Shura ya Maimamu, Ustadhi Ally Mbaruku, alisema taarifa hizo wamezipata na wanazifanyia kazi.Alisema wanayo taarifa ya kuugua kwa Said Amour na wapo katika mchakato wa kumshughulikia.
Kuhusu kugoma kula, alisema ni suala ambalo lipo nje ya uwezo wao kwani madai yao yameelekezwa katika mamlaka husika.Alisema baada ya kupata taarifa za kuugua kwa Amour, walilazimika kuuandikia uongozi wa Magereza barua ya kupatiwa kibali cha kumtibia chini ya uangalizi wao (magereza) na Waislamu watagharamikia matibabu yake.Ust. Mbaruku, alisema kwa mujibu wa maelezo waliyo nayo kutoka kwa mtuhumiwa huyo, anadai kuwa sehemu zake za siri zimevimba na zina dalili ya kuwa na usaha kutokana na kuminywa na askari wa usalama baada ya kukamatwa kabla haja fikishwa gerezani.
“Hiki ni kilio chao cha muda mrefu kuwa wanahitaji kufanyiwa uchunguzi afya zao kwa ujumla kutokana na madhila waliyoyapata lakini hakuna anayejali, kwa sasa tunahitaji kibali (ruksa) ya uongozi wa Magereza ili tumpatie matibabu.” Alisema Ust. Mbaruku.
Alisema Amour ni miongoni mwa watuhumiwa walioshindwa kuhudhuria Mahakamani siku ya Jumatatu (Mei 11, 2015) kutokana na maradhi yanayomsumbua, huku wengine ikiripotiwa kuwa wameshindwa kufika kutokana na kukosa nguvu.Alisema Kamati ya Maafa ilikuwa inategemea kupata majibu mapema wiki hii, lakini mpaka Jumanne wiki hii bado hawajajibiwa, jambo ambalo linazidi kuchelewesha tiba ya uhakika kwa mtuhumiwa huyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa Ust. Mbaruku, alisema mke wa Said Amour, alifika gerezani hapo kujua hali ya mumewe na kuelezwa kwamba Jumatano (wiki hii) kuna daktari atakwenda kumwangalia kwa ajili ya kumpatia matibabu.“Pamoja na majibu hayo lakini mle ndani wanapewa huduma za hapa na pale ambazo kwakweli hazikidhi haja ya matatizo waliyonayo, ndio maana athari zinazidi kujitokeza.“Hata hivyo tunaendelea kuwasiliana na uongozi mara kwa mara juu ya kupatiwa majibu ya barua ya maombi yetu ya kutoa huduma kwa Muislamu huyo”. Alisema Ust. Mbaruku.Akizungumzia mgomo wa watuhumiwa hao kula gerezani humo, Ust. Mbaruk alisema waliuanza tangu Jumamosi ya wiki iliyopita na kutoa masharti kadhaa.Alisema baadhi ya madai yao ni kutaka wafutiwe mashitaka ya ugaidi kwa sababu ni tuhuma za kubambikizwa zisizo na ukweli wowote, ndio maana ushahidi mpaka sasa hakuna.
Jingine ni kwamba wamechoshwa kupigwa danadana kwa rufaa yao, wakihoji ni kwa nini haitolewi maamuzi kwa wakati huku wakiendelea kunyimwa dhamana.Ust. Mbaruku, alisema mgomo huo umeanza kwa watuhumiwa wachache miongoni mwa watuhumiwa hao na kwamba, si wote waliogoma kwa sasa.Hata hivyo Ust. Mbaruku alisema, tayari Sheikh Farid Hadi, ametoa kauli kuwa watuhumiwa wote wataungana na wenzao ikiwa madai yao hayatotekelezwa.
Wakati huo huo kulikuwa na Kesi nyingine inayomkabli mtuhumiwa mwingine Ust. Sharifu Suleiman Sharifu kutoka Zanzibar nayo imeahirishwa huku akiwa kwenye mgomo wa kula.Waislamu wanaotuhumiwa atii kwa Ugaidi, wapo gerezani humo kwa makundi tofauti tofauti kulingana na tuhuma zinazowakabili ambazo zote sio za kweli, ambapo inakadiriwa kuwa mpaka sasa wapo zaidi ya arobaini katika gereza la Segerea. Kesi imeahirishwa hadi Mei 24. Sheikh Mselem Ali Mselem, kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho.
YOYOTE ATAKAE IPIGIA KURA CCM CHAMA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA MWEZI OKTOB AJUWE ANAIPA NGUVU ILI AENDELE KUTHALILISHA MASHEIKH NA WAZANZIBARI KWA UJUMLA TAFUTA JIBU LAKO KABISA SIKU YA KIYAMA KWA KUSHADIDIA MADHALIM HAWA WAENDELE KUKA MADARAKANI.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
No comments:
Post a Comment