Thursday, July 26, 2012

BAKH-RESA MFANYA BIASHARA ANAMILIKI MELI NA BOTI ZA KISASA SEREKALI YA ZANZIBAR HIMILIKI HATA BOTI YA DAGA-UJUHA WA MAPINDUZI DAIMA


MAKAMO MZEMA WA RAISI ATI ANAKWENDA NYUMBANI KWA KABACHORI KUPIGA MAGOTI KUSAIDIWA KUKOPESHWA MELI TOKA NENDA NCHI ZA NJE UKAONE MELI NA MABOTI YA ABIRIA ACHENI UJINGA NA UZUKA UNA KITU HICHI UNAKWENDA KWA KABACHORI ATAKUPA NINA KAMA SIO DENGU CHEE BAJIA CHEE HATUNA VIONGOZI ZANZIBAR TUNA MAJUHA NA WAHUNI BASI WAKUUWA WATU KWENYE MISIKITI NA SI ZA UCHANGUZI LAKINI VIONGOZI HATUNA KABISA.
Baada ya kujiuzulu kwa alie kuwa Waziri Mawasiliano na Miundo mbinu Mh. Hamad Massoud inaonekana wazi kwamba amewajibika kisiasa.Kwa mara ya mwanzo Zanzibar tumeshuhudia kiongozi wa ngazi ya juu kuchukua uamuzi mgumu kama huo. Iwavyo na iwe ikiwa kaladhimishwa au yeye mwenyewe ameamua ,ngoma imekuwa ngumu basi na iwe hivyo cha msingi ni kwamba Waziri huyo hayupo tena katika wadhifa wake, hili ni jambo la msingi kisiasa.Jee kwa sasa ni ipi hatma ya nchi yetu baada ya majanga yaliotokea ?
Nimesema kisiasa nikiwa na maana kwamba hapa kilichofanyika sio kuboresha au kutengeneza bali ni kiini macho tu,udhaifu na ukosefu wa utendaji upo pale pale,Serikali yetu ni kampuni ya Mapinduzi LTD.Naamini kuna watu wamefurahi kuundoka kwa Mh Hamad ni sawa na ndivyo ilivyo kimsingi lakini tujiulize jee hili ndio suluhisho la Wizara hii nyeti ? Tusisahau kwamba Serikali imekuwa kama  kampuni kwani suala la utendaji sio kigezo kwa  mhusika isipokuwa kauli ya tajiri na wapambe wake ndio wenye uwezo .
Wananchi walio wengi  wanashindwa kuelewa kwamba Zanzibar hatuna Serikali bali tuna kikundi cha Wahafidhina ambao wanatumiliwa na kuifanya Zanzibar kama kampuni ya Biashara na sio Serikali. Kampuni hii ambayo huendeshwa kwa njia ya majungu,chuki na ubinafsi ndio unaowafanya Wazanzibar hadi leo kuwa katika hali duni ya umaskini na unyonge usio kikomo.Viongozi wetu wanachojali ni kuvimbisha matumbo yao,huku wananchi wanateseka na wengine kupoteza maisha yao kwa uzembe ambao inawezekana kuepukika.
Hapo zamani Kampuni hii ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikuwa ikitumia kila mbinu kuwatesa Raia wake kwa kisingizio cha siasa, lakini baada ya joto la kisiasa kuwa kubwa na Wananchi wanaokandamizwa kuwa wengi, Kampuni hii imekuja na mbinu mpya sasa kuwapunguza Raia wake kwa Majanga ya uzembe na utendaji mbovu. Majanga haya ya uzembe yakitokea moja kwa moja hupelekewa Muumba kwamba yeye ndie alietaka hilo litokee.Lakini iman hizi kwa watawala wetu sio kweli,ukweli ni kwamba huko ni mafichoni kwao ili watu washindwe kujadili,waone hii ni kudra ya Muumba, lakini wanasahau kwamba wanajificha gongo nje,kwani huyo wanaemtupia lawama ndie huyo huyo wanaemtilia moto nyumbani kwake na kunajisi (Misikitini)
Inashangaza kuona kwamba Viongozi wengi wa Serikali yetu ni watu ambao hawana”VISION” yeyote ya uongozi wala utendaji,walaji rushwa,wazembe na viongozi ambao ni mbumbumbu, nashindwa kuelewa kwamba hawana Elimu lao ni  kasumba tu na ujinga walionao hawa Wahafidhina,hili nashindwa kulielewa.Mara nyingi ushabiki wa Serikali yetu hujipanga katika dhulma kwa kuwasulubu Wananchi wake bila kuwa na kipande cha huruma na ubiadamu na kusahau hata ule wajibu wao kama Viongozi.Inashangaza kuona Jeshi la polisi linawashambulia raia wake bila makosa lakini hata kuvamia nyumba za ibada wakati mwengine,huu ni uhuni si vyenginevyo.
Nasema hivi kwa sababu Nchi hii Muasisi wake Hayati Karume hakuwa msomi lakini aliiongoza nchi hii kwa ufanisi mkubwa tu,licha ya kufanya mabaya kwani hakuna mkamilifu lakini mazuri mengi alioyafanya hadi hii leo yanaonekana. Ukweli ni kwamba alioyafanya Karume hakuna hata kiongozi mmoja hadi hii leo alieyafanya hata wakia wa mazuri yake.Leo hii tunaambiwa kwamba Zanzibar tunaongozwa na Madokta wenye PHD lakini Serikali hiyo inashindwa hata kujua wapi pakununulia licha ya meli hata boti ya mtumba.Raia zake kila kukicha wanaliwa na kina na kiza  kinene cha mawimbi makubwa ya bahari na kuwa kitoweo cha samaki.
Nchi hii imegeuzwa kama kampuni binafsi ya Wahafidhina,inashangaza kumuona Makamo wa pili wa Serikali ambae ndio kiini cha utendaji katika Serikali yetu anatafuta meli kwa niaba ya Serikali na kumfuata mtu nyumbani kwake mambo haya viereje,hii inashangaza na ni aibu kweli.Hivi huu ni mtindo gani wa uendeshaji wa Nchi,inakuwaje Waziri anatoka mguu mosi ,mguu pili mpaka ”local shop” anaenda kununua vifaa vya uokozi kwa kutumia fedha ya serikali kiholela kama hivyo?Halafu anakuja anasema Serikali imenunua hichi na kile, hata hiyo kampuni ya mtu binafsi lazma kuwe na utaratibu wake.Hapa rushwa ndipo inaponukia na kuibiwa kwa Wananchi.
Leo hii napata picha halisi kwamba vile watani wetu wa jadi Watanganyika wanaposema kwamba Zanzibar ukivunjwa Muungano wata shindwa kujiongoza inawezekena kuwa na ukweli fulani kama viongozi wetu watakuwa ni hawa Wahafidhina akina Balozi Seif na wenzake akina Vuai na Borafia.Mimi nobe,basi nikiwa na nia ya kununua meli kwa ajili ya biashara yangu binafsi sio serikali basi lazima nifanye uchunguzi wa kina siwezi kumfuata mtu tu ”private” kiholela holela kama anavyofanya Mh,makamo wa Rais ambae yeye ndio kitovu cha utendaji katika kampuni hii ya Mapinduzi ya Zanzibar.Hii ni ishara mbaya na mwisho wake sio mzuri kwa maslah ya nchi.
Angalieni Watanganyika ni karibuni tu Mizengo pinda alikuwa korea kufuatilia utengenezwaji wa meli yao ya kufanya utafiti wa Mafuta kwa Tanganyika ,vile ndivyo anavyotakiwa Waziri Mkuu utendaji wake.Sisi Wazanzibar tunakaa na kutupiana lawama pamoja na kupikiana majungu. Serikali haiwezi kununua vitu kama vile kariakoo au Darajani,kunahitajika uchambuzi wa kina sio kwenda kwa Magabachori na kuwaangukia miguuni,eti tunataka mutukopeshe meli, huku ni kujidhalilisha kiserikali na Wazanzibar.Wahafidhina kubali matokeo,wapeni watu wenye uchungu wa Zanzibar waendeshe nchi yetu,mumeshindwa kuongoza,uongozi sio majungu ni utendaji na uwajibikaji.
Haingii akilini kuona kwamba Serikali inashindwa na mfanya biashara mdogo tu ,eti Serikali mzima inashindwa kununua meli yake basi hata boti , basi kuna haja gani ya kuwa na Serikali na mashangasha kibao pamoja na ving’ora badala yake tukamchagua Bakh-resa kuwa Raisi wetu yeye peke yake tukaachana na hawa wakuu wa mikoa manake wameshindwa kutuongoza.Leo hii mfanya biashara anamiliki,boti za kisasa,viwanda vya kila aina lakini Serikali wao ni kuwapiga raia na kuendeleza ujinga wa Mapinduzi daima,hivi jamani hamufikiri basi hata macho hamna. Tumechoka na kampuni hii ya Mapinduzi

No comments:

Post a Comment