HUYU NI MZUNGU WA KIKWETE KUTOKA NCHINI TANGANYIKA NA WAZUNGU WENZAKE KUTO NCHI ZA ULAYA WAKIJIVIJARI KWENYE NCHI YATU YA ZANZIBAR ILIO SAFI WAO WANAINAJISI KWA UCHAFU WAO WAKWENDA TUPU NA MENGINE MENGI TU HATA HAYASEMEKI.
ZANZIBAR ni njema…atakaye aje. Huu ni usemi maarufu wa wahenga wa Visiwani ambao umekuwa na lengo la kuwaonesha majirani zake na ulimwengu kwa ujumla kwamba Zanzibar hakuna matatizo ya kimaisha pia ulikuwa ni msemo wakuwatarifu wazanzibari walio kimbia mauwaji ya 1964 kuwa sasa nyumbani ni kwema na ataye aje.Walilenga kuuambia umma kuwa Wazanzibar ni ni wema, wakarimu na atakaye kwenda kuishi au kutembelea Zanzibar anakaribishwa kwa mikono miwili na moyo mkunjufu.
Kumbukumbu zinaonyesha jamii yoyote ile duniani, bila ya kujali imani zao, tofauti za dini au makabila, siku zote huwa inapendelea na kuweka sheria zitakazohakikisha mila, utamaduni na desturi za watu wake zinaendelezwa na mtu yeyote yule, awe mwenyeji au mgeni, anayezibughudhi , kuzikejeli au kuzidharau huonekana hana nia njema na jamii hiyo adhabu hupata mtu huyo ya kifugo au kutolewa kabisa katika nchi.
Ni kweli katika zama hizi za hivi sasa za utandawazi dunia imeshuhudia mabadiliko mengi ya kijamii na maisha kwa jumla. Jambo ambalo miaka ya nyuma hapa kwetu lilionekana sio la kawaida.
Kama mwanamume kuvaa herini au kidani, limekuwa likikubalika siku hizi. Wapo walioipokea hali hio kwa furaha na wapo walioiridhia kwa shingo upande, lakini hio ndio hali ya dunia ya leo.
Mambo kama haya ndio yaliyosababisha Waswahili wa kale kusema kiingiacho mjini sio haramu, lakini wapo watu hii leo wanaotofautiana na kauli hii na kusema si kila kinachoingia mjini ni halali.pia kuna msemo usamao hatakama ni kuinga basi usiige ovyo inamanisha yako ya kuingwa na mangine bora hata usiyangaliye.
Katika mambo ambayo watu wa Zanzibar wamekuwa wakiyajali sana na kutoyafanyia mzaha ni mavazi. Kwenda uchi au nusu uchi hadharani ni mambo ambayo watu wa Visiwani wamekuwa hawayakubali na hata anapotokea mtu mwenye matatizo ya akili anafanya hivyo watu hujitolea kumsitiri kwa kumvisha nguo. Hayo ndiyo maisha ya watu wa Zanzibar.Visiwa hivi vimekuwa kwa muda mrefu na sheria zake za mavazi. Sheria hizi zilikuweka miaka na kaka na baadaye zilitiliwa mkazo zaidi baada ya Mapinduzi ya 1964 ambapo hata watalii waliokuja Zanzibar wakiwa na mavazi ambayo kwa mila, silka, desturi na utamadini wa Zanzibar hayakubaliki walitakiwa kuchagua – kununua doti ya khanga au kitenge na kufunika sehemu ambazo watu wa Visiwani wanaona hazifai kuanikwa hadharani.
Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati mzee Abeid Amani Karume, aliwahi kusema : “Fedha za kigeni za watalii hazina thamani inayozidi mila na desturi zetu. Akitaka kwenda mtu uchi aende kwao si hapa kwetu Zanzibar.”huyu alikuwa raisi wa kwanza japo nae hakuchanguliwa kikura lakini alipenda nchi na kuioneya uchungu tafauti na hawa wanaojita mapidunzi daima wana wa kampuni ya mapinduzi daima wamekuwa hawajali ni mila wa nini disturia za visiwa hivi wao pesa tu basi.hata kama nchi nzima watu wako kama wanyama wao hawajali kwa kuwa kuna pesa hawa kweli ni viongozi hawa au ni madudu mwitu yanayo ila zanzibar na kuifisidi..?Katika mwaka 1965, aliyekuwa Rais wa Liberia, William Tubman, alipokuwa amepanga kufanya ziara ya Zanzibar alitaka watu wote watakaokwenda Uwanja wa Ndege wa Zanzibar kumpokea wavae suti.kumbuka yeye ni raisi wa nchi nyengine anatowa amri kwa raisi wa nchi nyengine nini kilotoke.Marehemu mzee Karume alikasirishwa na maelekezo yale na yeye alimpelekea salamu Tubman kumwambia kuwa mgeni yeyote anayefika Zanzibar kwa matembezi ya kiserikali basi lazima avae kanzu, koti, kofia na viatu vya makbadhi.hii inatufundisha ukiwa raisi wa zanzibar uwe mjasiri na mkakamavu na usikubali kusikiliza amri ya raisi yoyote kutoka nchi za jirani bahati mbaya toka kufa mzee karume nchi hii inaendeshwa na DODOMA na maraisi wamegeuzwa na kuwa mawaziri wasio kuwa na wizara maluum msiba msiba msiba mkubwa.Matokeo yake baada ya mazungumzo marefu ya kidiplomasia Tubman alikuja Zanzibar akiwa amevaa suti yake na watu waliompokea walivaa kanzu, koti, kofia na makbadhi yao na alipewa vazi hilo kama zawadi alipoondoka. Hili lilikuwa somo kuwa watu wa Zanzibar hawakuwa tayari kuona wageni wanachezea utamaduni wao.
Wakati ule watalii walielezwa tokea huko kwao kabla ya kufanya safari ya kuja Zanzibar aina ya mavazi ambavyo wanatakiwa wavae wanapokuwepo Visiwani na kuambiwa kuwa kutotii maelekezo hayo ni kosa la jinai.
Wapo watalii waliojaribu kukejeli maelekezo hayo na matokeo yake ni kusukumwa jela kwa wiki kadhaa na kunyolewa vipara. Hili lilikuwa fundisho kwa wengine.
Hivi sasa sheria hizi bado zipo, yaani hazijafutwa. Lakini kinachoonekana ni kufumbiwa macho na kupelekea watu kulalalama pembeni na hadharani kwamba utalii unavuruga mila, utamaduni na desturi walizorithi watu wa Zanzibar kutoka kwa wazee wao.
Ni kawaida siku hizi kuona kundi la watalii wanatembea na vichupi katika soko kuu la Zanzibar na kuwabakisha watu wanatikisa kichwa na kujiuliza: Hii ndiyo Zanzibar tunayoitaka?
Huko vijijini mambo hayasemeki. Watalii wanaofikia katika hoteli za fukwe za bahari huenda vijijini kutembea wakiwa wamevaa bikini (vazi la chupi na sidiria) na kupelekea vizee kukimbilia nyumbani kwao kujificha kwa vile macho yao hayawezi kuona aibu ile.
Ni kweli utalii kwa hivi sasa unaiingizia Zanzibar asilimia 73 ya pato lake la fedha za kigeni na kuchangia wastani wa asilimia 25 ya pato la taifa kila mwaka. Hapa suala linalofaa kujiuliza ni je, ni haki na sawa kwa fedha za kigeni ziruhusiwe kuvuruga utamaduni, mila na desturi za watu wa Zanzibar?
Ni vizuri kwa wahusika katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuitafakari hali hii kwa sababu manung’uniko ya wananchi juu ya watalii kwenda uchi au nusu uchi hadharani, mambo ambayo hata huko kwao hawayafanyi, yamekuwa makubwa na yanawaudhi watu.Hivi sasa watu wanalalamika na wanaonekana kuvumilia mwenendo huu kwa unyonge, lakini ipo hatari ya kutokea watu namanisha wazee na vijana kuonyesha hasira zao na matokeo yake kuwa mabaya. Ni kweli watu wanao uhuru wa mavazi, lakini si kwenda uchi hadharani.Inawezekana wakatokea wale ambao watasema huwezi kuwachagulia watu aina ya nguo za kuvaa, lakini hapa tukumbuke kuwa hao wazungu wanaokuja kwetu na kutembea nusu uchi pia wanazo sheria za mavazi huko kwao .Miongoni mwao ni kukataza wanafunzi wasivaie hijabu wanapokuwa shule na wale wanaojifunika gubi gubi au kuvaa “Ninja” kutoruhusiwa sehemu nyeti, kwenye benki,ofisi za serekali,hospitali pia kuna nchi nyengine hata ukiliva vazi la ninja nje tu sio kuwa unakwenda kweye benki au ofisi ya serekali laa nje tu pia unatozwa faini au unaishia jela washapitisha sheria hii france,belgum,swiss na holland pia na hili ni vazi la hishma la kujifinika gubi gubi au ninja lakini haliendani na madili yao au desturi zao ndio hawalitaki kwa nini sisi hapa zanzibar tuwaone haya kuwambia kuwa hilo vazi la vichupi pia kwetu hapa sio vazi la heshma na haliendani na mila na desturi zetu..kwanini hatuwambi hivyo..? na kuwalazimisha wavae vizuri.ila hilo halipo maana akili za viongizi wetu ziko kwenye wimbi la pesa tu basi hata kama mila,desturi zinaharibika wao wanapata pesa basi ni poa tu maneno ya mtaani poa tu.Sasa kama watu wengine wanaweza kuwa na sheria za mavazi na kuambiwa lengo lake ni kulinda usalama wao, kwa nini Zanzibar ione tabu kuendelea na kuwa na sheria za mavazi za kulinda mila, utamaduni na desturi za watu wake?Hili ni suala nyeti ambalo kampuni ya Mapinduzi Zanzibar haistahili kulipuuza.naita kampuni ya mapinduzi zanzibar kwa sababu mimi naona hatuna haswa serekali maana kama tuna serekali nchi hii sio ya kuwa ovyo ovyo kama tambara la kupingia decki. hii nchi sio maaskhara ukijuwa historia yake huko ilikotoka leo ipo ipo tu kama kishungu cha taka kinasubiri rikwama la wazoa taka lije likiondoshe.Ni ukweli usiokuwa na ubishi kuwa zaidi ya aislimia 99 ya watu wa Zanzibar ni Waislamu na imani ya dini yao ndio siku zote imekuwa mhimili mkuu wa sheria za nchi na mwenendo wa maisha yao. Utandawazi isiwe sababu ya kuvuruga mwenendo wao wa maisha.Watalii wanaweza kuvaa hizo bikini zao vyumbani mwao, kwenye ufukwe wa bahari au wanapokuwa kwenye maeneo ya hoteli walizofikia, lakini si kwenda na vivazi hivyo sokoni au mitaani na kuwaudhi watu ambao hawataki mila na utamaduni wao kuvurugwa na wageni wala wenyeji.Watu kuingilia mila na tamaduni zao na Wazanzibari wanayo haki ya kuringia mwenendo wa maisha waliorithi kutoka kwa wazee wao.Kama wengine watasema watu wa Visiwani hawajaendelea ieleweke kuwa Wazanzibar maendelo kwao si kwa mwanamume kuvaa herini au kidani, watu wa jinsia moja kufunga ndoa au mtu kwenda uchi hadharani.Ni matumaini yangu kuwa kiu ya kupata fedha za kigeni kutokana na sekta ya utalii haitakuwa sababu ya kuvuruga mila na utamaduni wa watu wa Visiwani.
Zanzibar inaweza kubakia kuwa ni njema na atakae aje, lakini aje kwa heshima, wema na hisani na anapaswa kutodharau mila, utamaduni na desturi za wa watu wake.
VIONGOZI MUONGOPENI MWENYZI MUNGU MUTAULIZWA SIKU YA KIYAMA ULIZICHUMA VIPI PESA ZAKO NA HATA RIZIKI ULIO KULA UMENUNU NA PESA ZIPI.

No comments:
Post a Comment