MIAKA 50 YA UHURU WA NCHI YA TANGANYIKA NA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA NCHI YA ZANIBAR MAJI 20% UMEME 20% ELIMU 0% HOSPITALI 1% MADAWA 0% MLO MOJA KWA SIKU TAFAKARI SANA.CCM MNASHANGA LOWASSA KUPANDA DALADALA HAMSHANGAI TWIGA KUPANDA NDEGE.VIONGOZI WA CUF WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI 2015 WAKIONYESHA SHAHADA ZAO ZA USHINDI ZILIZO SAINIWA NA KUPIGWAMUHURI NA ZEC CCM HAYA HAMUNA,AIBU HAMUINI,FEDHEHA HAMUHISI,UBINADAMU UMEWATUKA,M.MUNGU HAMUMUOGOPI HEBU JIULIZENI NYINYI VIUMBE WA AINA GANI...?????
Friday, July 27, 2012
WAZIRI ASIYEKUWA NA WIZARA SHEINI AMEAGIZA WIZARA YA FEDHA KUSAKA FEDHA ZA KUNUNUWA MELI
Waziri asiye kuwa na wizara maluum wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Ali Mohamed Shein, ameiagiza Wizara ya Nchi Afisi ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo kuandaa utaratibu wa kupata fedha ndani ya wiki moja kwa ajili ya kununua meli kubwa mpya ya abiria wapatao 1000 na yenye uwezo wa kuchukua mizigo ya tani 100.
Shein ametoa agizo hilo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na uongozi wa Shirika la Meli pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Shirika hilo ambapo pia kikao hicho kilihudhuriwa na uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na Wizara ya Nchi Afisi ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo. Katika kikao hicho maalum
Shein ameiagiza Wizara hiyo kutafuta fedha hizo kutokana na vianzio vya ndani au nje ya nchi ama kutokana na taasisi zinazohusiana na mambo ya fedha.
Alieleza kuwa katika kipindi kisichozidi miezi miwili ujumbe maalum uende kwa Kampuni zinazotengeneza meli nchini Korea Kusini, China au Japan kwa ajili ya kuwasilisha fedha za utangulizi kwa ajili ya ujenzi wa meli hiyo.
Mapema uongozi wa Shirika la Meli, ulimueleza Shein kuwa kwa kawaida ujenzi wa meli yenye ukubwa huo, huchukua mwaka mmoja kukamilika.
Kikao hicho ambacho kilikuwa na lengo la kuangalia mwelekeo na Mipango ya Shirika la Meli pia, kilijadili hali halisi ya meli za Shirika la Meli na baadae kujadili masuala ya ununuzi wa meli mpya itokayowaondoshea usumbufu wa usafiri wa baharini wananchi wanaosafiri kati ya Unguja, Pemba na nchi ya Tanganyika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment