1. Wizara wa Sheria Abubakar imeoza na inanuka,dhulma imezidi – mfano:zile kesi zinazowahusu ndugu zetu wa UAMSHO.Wanakamatwa vijana bila sababu yeyote, hata inashindikana kuunda au kutengeneza charge ya kubuni. Mbaya zaidi, siku hizi polisi wanataifisha vyombo vya moto katika mihadhara hiyo,na kama utakwneda kudai, unaambiwa ‘ahh wewe ndiye tuliyekuwa tunakutafuta’ hivyo uko chini ya ulinzi.
Baadhi ya vespa, baiskeli tayari wanaendesha askari polisi, wamewanyanganya watu hivi hivi.je kama sio thulma nini..?
Baadhi ya gari za wafuasi au viongozi wa uamsho – zinahujumiwa na kuvunjwa kwa makusudi. Kweli haki hiyo, bwana Abubakar..? Haya yanatokea mchana na wizara yako inahusika na inajuwa kila kitu ila umebana kimya unaacha dhulma endele–kisha mnakaana nakupiga kelele kuwa mnataka haki ya zanzibar ndani ya Muungano wakati nyinyi hamfanyi haki hata chembekwa rai wenu ndani ya nchi yenu.
Tunataka haki Abubakar na wewe ushalikoroga sana kwa hiyo ujiuzulu pia.
2.Rushwa iliyokithiri ndani ya mahakama, majaji, hupati haki kama hujatoa rushwa tunakufa kwa mengi, sio kupinduka kwa meli tu.Ama pale Wizara ya Elimu nayo kumeoza, harufu mbaya ya kila uoza: vyeti zaidi ya 200 fake, wanalipwa bure na hatimaye wanazalisha wanafunzi fake. Hivi karibuni walikuwa wanafanya uhakiki SMZ wote watumishi kumbe ilikuwa KIINI MACHO -yaani wanataka kujua nani na nani yumo na nani na nani hayupo, ili wawezi kupenyeza watu wao waziwa wa elimu pia ajiuzulu.
Kuna ofisa mmoja ya wizara ya fedha yeye huwa ana kwenda Pemba kila mwisho wa mwezi, na ukimtaka utampata pale Island hotel chake chake, na usiku pale kwa‘hababuu panapo uzwaa mishkaki’near Madungu huyu kazi yake ni kwenda kukusanya mishahara hewa ya wafanyakazi hewa.
Huu ndio uoza uliojaa ndani ya SMZ-GNU: hili Kishein pamoja ya kuwa ‘huogopi mtu’unalijua,maalim Seif-1 na balozi Seif-2 pia mnalijua lakini hamuthubutu na hamuwezi kuchukua hatua yoyote ya kubadilisha thulma hii je kishein hivyo ndio huogopi mtu kweli..?, maana wanaofanya haya ni watoto wenu wenyewe. hamuwezi kufanya chochote. Mtabaki kuuwa watu kwa boti au kuwapiga mabomu wanyonge katika misikiti na kuendele kutuletea vyakula vibovu kutoka bara na nje.
3.Wizara ya Afya, hakufai: dawa takriban 100% zinazoletwa Zanzibar ni fake na mbovu zishakwisha mdaa wake lakini munazileta ili masikini tufu watoto wenu watajirike maana ndio biashara zao,nasi tunaendele kufa kwa mengi.waulizeni watu idara ya mkemia mkuu wa serikali, wanajua lakini wanaogopa kusema, wanafumba macho maana ni biashara ya wakubwa na watoto wa wakubwa. Rushwa,rushwa,rushwa
4.Wizara ya Biashara imeoza inanuka: mpaka leo,tende mbovu ndio zinazoletwa hapa nchini Zanzibar, mchele mbovu,wa mabembe,na unga wa ngano mbovu ukitowa rushwa OK, utaruhusiwa, na kama hujatowa basi mchele wako utamwagwa: philosophy yetu: UKITAKA KULA, NA WEWE LAZIMA UKUBALI KULIWA.TUNAKUFA KWA MENGI NA TUTAZIDI KUFA SIO KWA KUZAMA MELI TU BALI KWA VYAKULA VIBOVU, DAWA MBOVU, NA ELIMU MBOVU,NA JESHI SIO LA ZANZIBAR WA POLISI WOTE NI WAKURIA WATAENDELE KUTUUWA WEEE MPAKA MWISHO WA HABARI.
Msisahau rushwa na dhulma iliyojaa katika sekta ya ardhi,mawaziri wanaiba ardhi za wananchi kwa kutumia nguvu zao za mamlaka ya dola, na raisi Kisheini analijua hili, ila anasema ‘wanaosababisha migogoro ya ardhi wataitatua wenyewe. Umeona wapi mhalaifu akajihukumu mwenyewe..?
No comments:
Post a Comment