Sunday, July 29, 2012

SHAMSI VUAI NAHODHA AJA NA FITINA MPYA ZA KUTAKA KUWAFITINISHA WAZANZIBARI


SI ULIKUWA WAZIRI KIONGOZI WEWE MBONA HUKUSEMA KUHUSU WIZI WA ARDHI
AU WAKTI ULE WEWE PIA ULIKUWA UKIBA NDIO MAANA HUKUSEMA KITI..?
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, amewaponda baadhi ya viongozi wa Zanzibar wanaozungumzia kero na Muungano kwa nia ya kuficha makucha ya ufisadi wao.
Alishusha kombora hilo wakati akichangia hoja kwenye semina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi iliyofanyika juzi mjini hapa.
Alisema kuna ubadhirifu, wizi, uporaji wa ardhi na rasilimali za Zanzibar unaofanywa na baadhi ya vigogo wa Zanzibar lakini vitendo hivyo vinafumbiwa macho.
“Viongozi wanaozungumzia matatizo ya Muungano kwa jazba hapa Zanzibar kwanza wanatakiwa kupima uadilifu na matendo yao ziwemo pia sheria zitakazowabana kujua walipataje mali walizonazo”, alisema
Nahodha ambaye aliwahi kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuanzia mwaka 2000 hadi 2010 kwenye awamu ya Rais Amani Karume alisema hakuna Mtanganyika anayepora ardhi, fedha au kodi za wananchi ila viongozi wa Zanzibar.
Alisema yeye ni muumini wa Muungano wa serikali mbili uliopo na kupendekeza suala la mafuta na gesi asilia litolewa kwenye Muungano kwa kufuata taratibu zilizoliingiza jambo hilo katika orodha ya masuala ya Muungano.
Pia Waziri Nahodha alimuuliza Waziri wa zamani wa SMZ na Serikali ya Muungano Hassan Nassor Moyo kueleza matukio yaliyolitishia usalama wa ndani kuanzia mwaka 1964 hadi 1972.
Moyo akionekana kubabaika, hakujibu swali hilo na kujikuta akipata wakati mgumu kutokana na kutokea kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume aliyepigwa risasi na Luteni Homuod Mohamed.
Nahodha alisema ana hakika ya kutokea matukio 14 ya njama kwa maelezo ya kiintelijensia yalipangwa kuipindua SMZ ambayo yaliandaliwa na wapinzani na kwamba tukio la 15 katika njama hizo lilifanikisha kifo cha Mzee Karume April 7 mwaka 1972.
Moyo alieleza msimamo wake kuwa Muungano uliopo wa serikali mbili unahitaji kufanyiwa marekebisho na maboresho makubwa ili uendane na wakati.

No comments:

Post a Comment