Tuesday, July 10, 2012

SARAFU YA MAKABURU WEUSI WA TANGANYIKA INAWATIA UMASIKINI NCHI YA ZANZIBAR


SERIKALI ya Zanzibar imesema kuwa haiwezi kuanzisha sarafu yake (fedha zake) kutokana na kuwa katiba ya jamhuri ya muungano abayo ndio katiba ya tanganyika iliyotiwa viraka ili kuinyonya nchi ya Zanzibar hairuhusu kufanya hivyo. Hayo yameelezwa na waziri wa nchi ofisi ya rais fedha, uchumi na mipango ya maendeleo, Omar Yussuf Mzee wakati akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu aliyetaka kujua sababu za Zanzibar kutokuwa na sarafu yake ili kuimarisha uchumi wake.
Jussa alisema sarafu ya Tanganyika (Tanzania) inaendelea kushuka thamani dhidi ya fedha za kigeni (dola) siku hadi siku na kufanya Zanzibar kuwa katika hali ngumi kiuchumi ikiwemo wananchi wake kukabiliana na mfumko wa bei na kupelekea maisha kuwa magumu.
Akijibu suali hilo Mzee alisema kimsingi Zanzibar ina uwezo wa kiuchumi wa kuanzisha sarafu lakini katiba iliyopo hivi sasa sarafu ni suala la muungano na hivyo haitoi fursa kuanzisha sarafu yake hapa Zanzibar.
“Sio kweli kwamba sarafu ya Tanganyika(Tanzania) inaendelea kushuka thamani siku hadi siku lakini ni kweli kwamba thamani ya shilingi Tanganyika (Tanzania) ikilinganishwa na ile ya dola za kimarekani imekuwa na muelekeo wa kushuka” alisema waziri.
Akitaja sababu nyengine za kushindwa kuwa na sarafu Zanzibar, Mzee alisema hivi sasa nchi za Afrika Mashariki zimo katika mchakato (Process) za kuelekea katika kuwa na muungano wa fedha ambao utakapokamilika nchi zote katika jumuiya hiyo zitakuwa na sarafu moja tu.
“Mheshimiwa Spika kufuatia upepo huo unaovuma kuelekea katika sarafu moja haitayumkinika kwa Zanzibar kujitenga kwa kuanzisha, kuhudumia na kusimamia sarafu yake hata kama ina uwezo wa kiuchumi kufanya hilo” aliwaambai wajumbe hao.
Akielezea zaidi kuhusiana na sababu za kushuka thamani ya fedha ya Tanganyika(Tanzania) alisema ni kutokana na urari wa malipo ya nchi za nje, tofauti ya mfumko wa bei na nchi zinazofanya biashara na Tanganyika(Tanzania) na kuchafuka kwa masoko duniani.
Pia alitaja kuwepo kwa mahitaji makubwa ya fedha za kigeni kwa ajili ya miradi ya miundo mbinu kutokana na kuchelewa kwa fedha za wahisani na mikopo, na hisia za upungufu wa fedha za kigeni kuwa ni miongoni mwa sababu za kushuka thamani ya fedha za Tanganyika( Tanzania.)

No comments:

Post a Comment