Saturday, July 14, 2012

KULIKUWA HAKUNA NCHI ITWAYO TANGANYIKA 1832 TAYARI ZANZIBAR NI DOLA HURU KISHEIN AMKA ACHAA KUPIGA MAGOTI KWA DODOMA KISHEIN KNOW THE HISTORY OF UR COUNTRY ZANZIBAR.


(Amri zikitoka Zanzibar kwenda Oman, Tanganyika na maeneo mengine ya afrika)
Nianze makala yangu kusimulia kwamba wengi hawajui nini ZANZIBAR na hapa ndipo wanapopata tabu kukubali ukweli unaozungumzwa na wazanzibari kudai mamlaka ya taifa lao.
Zanzibar ikijuulikana tokea zamani (miaka mia tano kabla kuzaliwa nabii Issa), ilikua ni dola yenye nguvu sana kipindi hiko hata mataifa makubwa yakija kukopa Zanzibar na yakiitambua Zanzibar kwa heshma iliyonayo na wasifu wake wa kiutawala, eneo lake lilianzia kaskazini Kismayuu hadi Msumbiji sofala (kuanzia hapa zanzibar ya sasa hadi kongo) hii ilikua kabla ya kukatwana kugawiwa na na wakoloni, na ndio mana katiba yetu (Baada ya marekebisho ya 10) inatambua mipaka yetu kwa kuviongelea mpaka visiwa vidogo vidogo kama ni sehemu halali za Zanzibar.
Zanzibar ni Dola kongwe miongoni mwa dola za Afrika na ndio mana katika ramani iliyogunduliwa na chuo kikuu cha Oxford uengereza iliyochorwa katika karne ya kumi na moja viswa vya unguja na pemba vilikuwemo na makao makuu yake yalikuwa unguja ukuu, katika ramani hiyo hakuna Tanganyika.
Zanzibar ilitambulikana kuwa dola huru mnamo mwaka 1832, hadi mataifa makubwa ya magharibi yakafungua balozi zao Zanzibar, Kwa mfano Marekani alifungua balozi yake hapa mnamo mwaka 1837 na mwingireza nae akafungua balozi yake 1841, ufaransa akafungua balozi yake hapa 1844 na ujerumani akafungua nae mwaka 1847, hakuna nchi yeyote kusini mwa jangwa la sahara iliyokua ikijuulikana kama dola na kuwa na mahusiano ya kibalozi na mataifa makubwa zaidi ya Zanzibar.
Zanzibar ilikuwa na Benki kuu yake na pesa zake, na uchumi wake ulikua ni mzuri kuzidi mataifa mengi tu, ukenda WORLD BANK wakikupa takwimu za kifedha za miaka ya Raisi Karume Utakuta ni Nchi ya pili ama ya tatu kiuchumi kwa afrika (wachumi huita GDP), huku ikiwa na akiba ya Paundi milioni 800 katika banki ya kiengereza.
Zanzibar kibiashara ilijuulikana kama “THE INTERNATIONAL TRADE GATE WAY” LANGO KUU LA KIBIASHARA, serikali za wakati huo zikijifunza biashara kutoka hapa kwakua na uzoefu mzuri wa kuendesha biashara za ndani na nje ya nchi. Zanzibar ilikua ni kituo kikuu kibiashara, kisiasa na kiuchumi katika miaka hiyo.
Historia ya Zanzibar bado imbaki ya kipekee na imeshazungumzwa sana nyakati tofauti, nimekusudia kugusia haya ili kuwaomba wenzangu turejeshe mamlaka yetu ya utawala wa zanzibar.
Wazee wetu walitabiri na kusema “UTAWALA WA ZANZIBAR UTARUDI NA UTAKUWA NA NGUVU ZAIDI KULIKO ULE WA ZAMANI” M/mungu athibitishe maneno haya ya wazee wetu.
Utawala ni kitu kikubwa sana, na kujitawala ni bora kuliko kutawaliwa, kujitawala ni ile hali ya kuwa na mamlaka kamili ya kuendesha serikali bila ya kuingiliwa na upande wowote.
Hivyo basi ili kuwa na utawala kamili wenye nguvu zake kimadaraka turudishe yafuatayo:-
1. Mambo ya Nje na uhusiano wa kimataifa
2. Ulinzi na usalama (Jeshi kamili la Zanzibar kama ilivyokua Nyuki)
3. Polisi.
4. Mamlaka yanayohusiana na mambo ya hatari.
5. Uraia wa Zanzibar.
6. Uhamiaji liwe chini ya Zanzibar.
7. Mikopo na biashara ya Nchi za Nje.
8. Bandari, mambo yanahusiana na usafiri wa anga, posta na simu.
9. Benki Kuu, Mambo yote yanahusiana na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yeyote halali (pamoja na noti), Mabenki (pamoja na mabenki ya kuweka hakiba) na shughuli zote za kibenki, fedha za kigeni na usimamizi wake.
10. Leseni ya viwanda na takwimu.
11. Elimu ya juu.
12. Maliasili ya Mafuta.
13. Usafiri na usafirishaji wa anga.
14. Utafiti.
15. Vyama vya siasa view chini ya mamlaka ya Zanzibar.
Haya tukiyadai yakarudi na kuyaweka katika katiba yetu ya Zanzibar yatakidhi yale marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar.
Katika maswala haya na maslahi ya Zanzibar tuache kuchezewa na wanasiasa, sisi tunakuwa na tunazaa tuwaandalie urithi mwema vizazi vijavyo, kutumiwa kisiasa ni kosa kubwa lililotufikisha tulipo mpaka viongozi wetu wakayagawa mamlaka yetu DODOMA.
Vyama hivi vya siasa vinazaliwa na kufa (kwakua ni fikra na mawazo tu ya kundi Fulani la watu wanaosaka mamlaka ya kuendesha Nchi), ila Zanzibar ilikuwepo na itaendelea kubakia, ikibaki na mamlaka kamili ndio utakua natija kwetu na urithi mwema wa vizazi vyetu.

No comments:

Post a Comment