Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad, akimjuilia hali na kumfariji mzee Muombwa
Rashid wa Kajengwa Makunduchi, wakati wa ziara yake ya
kutembelea wagonjwa katika Mkoa wa Kusini Unguja
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad, akimjuilia hali na kumfariji Bi. Mkasi Jihadi
wa Kijini Makunduchi wakati wa ziara yake ya kutembelea
wagonjwa katika Mkoa wa Kusini Unguja nchini Zanzibar.
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad, akisalimiana na wananchi wa Makunduchi
wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Mkoa
wa Kusini Unguja nchini Zanzibar
Wananchi mbali mbali wakijumuika katika futari
iliyoandaliwa na Makamo wa Kwanza wa Rais nchini
Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake
Mbweni nchini Zanzibar
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad akimfariji mzee Ali Juma Makame wa
Mkwajuni, baada ya kumjulia hali ikiwa ni ziara ya Makamo
wa Raisi wa nchi ya Zanzibar ya kutembelea wagonjwa na
wafiwa.
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif
Hamad, akimjuilia hali mzee Faraji Mziwanda wa Chaani,
ikiwa ni ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wafiwa
katika Mkoa wa Kaskazini Unguja nchini Zanzibar
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad, akimjulia hali Haji Makame Sangire wa
Kigunda, ikiwa ni ziara yake ya kutembelea wagonjwa na
wafiwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja nchini Zanzibar.
Masheikh mbali mbali walio jumuika katika nyumba ya Makamo wa Raisi Maalim Seif Shariff Hamad nchini Zanzibar katika futari aliyo wandalia Masheikh hao.
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif Sharif
Hamad akiitikia dua wakati akimjuilia hali Bi. Maryam Omar wa
Kilimahewa Msikiti ngamia, wakati wa ziara
yake kwa wagonjwa Mkoa wa Mjini Magharibi nchini Zanzibar.
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amewahimiza waislamu kushirikiana na kusaidiana ili kudumisha umoja miongoni mwao.
Amesema umoja na mshikamano ndio nguzo ya kuzidisha mapenzi miongoni mwa waislamu, na kutaka utamaduni huo uendelezwe kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo alipokuwa akitoa shukrani kwa masheikh na wananchi waliojumuika nae katika futari aliyoiandaa kwa ajili ya viongozi hao wa dini, nyumbani kwake mbweni.
Amewashukuru masheikh kwa kujitokeza kwa wingi katika futari hiyo, na kwamba kitendo hicho kinaashiria mapenzi waliyonayo viongozi wa dini kwa viongozi wao wa kitaifa.
Wakati huo huo Maalim Seif amehitimisha ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wafiwa kwa upande wa Unguja nchini Zanzibar, baada ya kufanya ziara katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
Katika ziara hiyo ametembelea maeneo mbali mbali ya Wilaya za Mjini na Magharibi na kuonana na wagonjwa na wafiwa katika mitaa tofauti ikiwemo Mbweni, Tomondo, Magogoni na Mji Mkongwe.
Akiongozana na viongozi mbali mbali wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib Ferej na Naibu Waziri wa Elimu Zahra Ali Hamad, Maalim Seif alianza ziara mapema asubuhi katika mitaa wa Mbweni matrekta, Kiembe samaki na Mwanakwerekwe, kabla ya kusitisha ziara hiyo na kujumuika katika mazishi ya wanajeshi wawili wa Zanzibar waliouliwa Darfur nchini Sudan.
Alihitimisha ziara hiyo kwa kutembelea Jimbo la Mji Mkongwe alipokwenda kuwajuilia hali na kuwafariji mzee Salim Mzee wa Darajani na mzee Ali Yussuf wa Mkunazini.
Ziara kama hiyo inatarajiwa kufanyika katika mikoa ya Pemba nchini Zanzibar hivi karibuni, ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
No comments:
Post a Comment