Sunday, July 7, 2013

MARAISI NA VIONGOZI MBALI MBALI WA AFRIKA WAFIKISHWA ICC KWA MAUWAJI YA RAI NI LINI MKAPA NA SALMIN AMOUR NAO WATAFIKISHWA ICC KWA MAUWAJI YA WAZANZIBARI WALIO WAUWA..???



MMOJA mmoja, wauaji wa Afrika wanakiona cha mtema kuni. Mmoja mmoja wanafikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kwamba walipokuwa na madaraka waliyatumia vibaya madaraka yao kwa kuwaua na kuwatesa wananchi wenzao.Charles Taylor, aliyewahi kuwa Rais wa Liberia, alihukumiwa mwaka jana kifungo cha miaka 50 gerezani.  Alipewa hukumu hiyo na Mahakama Maalumu ya Sierra Leone iliyoundwa na Umoja wa Mataifa.
Alishtakiwa kwa shtaka la kuwasaidia na kuwachochea waasi wafanye jinai wakati wananchi wa Sierra Leone walipokuwa wakipigana wenyewe kwa wenyewe baina ya 1991 hadi 2002.
Taylor alikuwa na mbwembwe na akijiona kuwa hakuna kama yeye. Safari moja 1997 hata kabla hakuwa rais nusura niwe ‘muathirika’ wa kibri yake nilipokuwa nikimsaka nchini Liberia. Watu aliokuwa akiwatumia kumlinda walikuwa ni watoto wadogo aliowatwika silaha.
Wakati nilipokuwa nikimsaka nilikumbana na mmojawao. Alikuwa na kimo kifupi mno kushinda silaha aliyokuwa akiibeba. Nina hakika pia kwamba alikuwa amevuta bangi.
Nilikutana naye ghafla nje ya nyumba mpya Taylor aliyokuwa akiijenga kando ya barabara inayoelekea Congo Town ambako Taylor akiishi karibu na balozi za Nigeria na Ujerumani.
Taylor mwenyewe alikuwa ndani ya nyumba akisimamia ujenzi. Lakini hapa si mahala pake kuihadithia kadhia nzima iliyojiri hapo. Naitoshe tu kueleza kwamba yalizuka mabishano baina yangu nahuyo kijana aliyekuwa akimlinda.
Nilifanya ujinga kushikilia kushindana naye, tena kwa kutumia maneno makali wakati yeye akiwa na bunduki ya aina ya AK-47 na kichwa chake kikielea katika bahari ya andasa za bangi.
Miezi kadhaa baadaye Taylor alichaguliwa Rais wa Liberia na akaanza kuyatumia madaraka yake kwa kuwasaidia waasi wa Sierra Leone waliokuwa wakiua, kukata watu mikono na kuwafanyia wananchi wenzao mateso mengine yasiyosemeka.
Kiongozi mwengine aliyetiwa mbaroni na hatimaye kufikishwa kwenye Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC) ni Laurent Gbagbo aliyekuwa Rais wa Côte d’Ivoire hadi alipokamatwa Aprili 2011.
Kabla ya hapo Gbagbo alishindwa na Alassane Outtara kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliofanywa Novemba 28, 2010.Gbagbo alikataa kuwa ameshindwa. Alichofanya baadaye ni kuchochea mauaji mjini Abidjan ya watu waliotoka sehemu za kaskazini mwa nchi yake, sehemu aliyotoka Outtara.
Inasemekana kwamba waliokuwa wakiuua walikuwa wanajeshi wake, wengi wao wakiwa askari wa kukodiwa kutoka Liberia. Wawakilishi wa Umoja wa Mataifa mjini Abidjan wamekuwa wakipokea taarifa kuhusu vikosi vya mauaji vya Gbagbo na pia inasemekana kwamba makaburi ya halaiki yamegunduliwa mjini Abidjan.
Shutuma hizo ndizo zilizosababisha Gbagbo na mkewe Simone kukamatwa na kushtakiwa na mahakama ya ICC.
Vigogo wengine waliokamatwa ingawa si marais ni pamoja na Jean-Pierre Bemba, kiongozi wa Vuguvugu la Ukombozi wa Congo (MLC), Saif al-Islam Gaddafi, mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Mu’ammar Qadhafi naGermain Katanga, almaarufu kwa jina la ‘Simba.’
‘Simba’ anashtumiwa kuwa ndiye aliyekuwa kamanda wa jeshi la Force de résistance patriotique en Ituri, kundi la wapiganaji wa kabila la Ngiti waliokuwa wakipigana huko Ituri, Congo-Kinshasa.
Shutuma inayomkabili ‘Simba’ ni kwamba siku moja mwezi wa Februari 2003 aliwaamrisha wapiganaji wake wakishambulie kijiji cha Bogoro na kuwaua watu wa kabila la Hema.
Mwengine anayeshikwa na Mahakama ya ICC ni Bosco Ntaganda aliyesalim amri mwenyewe Machi mwaka huu alipokimbilia Ubalozi wa Marekani mjini Kigali, Rwanda, akiutaka Ubalozi umsaidie kumfikisha mbele ya ICC, mjini Hague, ambako kesi yake sasa inaendelea.
Wa karibuni kutiwa mbaroni ni Hissène Habré, Rais wa zamani wa Chad, aliyekamatwa Jumapili iliyopita huko Dakar, Senegal.
Habré anakabiliwa na shtaka la kuwaua na kuwatesa maelfu kwa maelfu ya wapinzani wake. Kwa mujibu wa  Tume moja ya Uchunguzi iliyoundwa baada ya Habré kupinduliwa mwaka 1990 Habré aliwaua watu wapatao 40,000 kwa sababu za kisiasa na wengine laki mbili waliteswa katika muda wa miaka minane ya utawala wake.
Mara ya mwanzo kulisikia jina la Hissène Habré ilikuwa 1974 pale kundi lake la waasi wa FAN walipowateka nyara Wazungu watatu. Habré alisema hatowaachia wazungu hao mpaka kwanza alipwe fidia ya faranga za Kifaransa milioni kumi.
Mmoja wa mateka hao alikuwa Françoise Claustrealiyekuwa mwethnolojia na mwanaakiolojia. Mwanamke huyo Wakifaransa, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 37, alishikwa na akina Habré kwa muda wa miezi 33 katika mapango ya milima ya Tibesti kaskazini mwa Chad.
Habré aliyesomea sheria na siasa Ufaransa kwanza alizivaa siasa alipopelekwa na serikali ya Chad kwenda kuyashawishi makundi mawili ya waasi yasalim amri. Badala yake alijiunga na moja ya makundi hayo lililokuwa likiongozwa na Goukouni Oueddei. Na Goukouni alipokuwa Rais alimteua Habré awe waziri wa ulinzi.
Katika siasa za Chad za siku hizo Goukouni alikuwa akiiunga mkono Libya, kiasi cha kufikiriwa kwamba alikuwa kibaraka wa Libya. Wakati Goukouni alipokuwa Rais kulikuwa na minong’ono kwamba kulikuwa mpango wa kuiunganisha Chad na Libya.
Habrékwa upande wake akiungwa mkono na Marekani pamojana Ufaransa ambayo iliufumbia macho uharamia wakeHabré wa kuwateka nyara wale wazungu watatu mwaka 1974.  Wengi wakiamini kwamba Habré alikuwa kibaraka wa mataifa ya Magharibi.
Habré alimpindua Goukouni 1982 wakati majeshi ya Libya yalipokuwa yakipigana katika eneo la Aouzou lenye madini nyingi ya urani. Kuna ushahidi kwamba Habré alisaidiwa na shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, kumpindua Goukouni.
Habré alitawala kwa mabavu kwa muda wa miaka minane mpaka 1990 alipopinduliwa na Rais wa sasa wa Chad Idriss Debby, mshauri wake wa zamani wa kijeshi.
Majaribio kadhaa ya kumpindua Habré yalifanywa wakati wa utawala wake. Naye alilipiza kisasi kwa kuua na kutesa. Baadhi ya mateso yananikumbusha niliyokuwa nikiyasikia kwa walioteswa kwa ‘Ba Mkwe’, sehemu ya jela kuu ya Zanzibar.
Baadhi ya walioteswa na utawala wa Habré na walionusurika wanasema kwamba watesaji wakipendelea kuwarusha kwa umeme, kuwachoma kwa moto wa sigara, kuwakaba roho mpaka karibu wafe na kuwarushia gasi machoni.
Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limesema kwamba baadhi ya wafungwa wa kisiasa wakiwekwa chumba kimoja na maiti waliokuwa wakitoa harufu.
Mtu mmoja alisema alifikiri kichwa chake kitapasuka kilipowekwa kati ya fito zilizofungwa kamba na halafu zikafikichwa. Mateso hayo yakiitwa ‘supplice des baguettes’ (mateso ya fito).
Ni wazi kwamba Habré alitumia vitisho na hofu ili kuunyamazisha upinzani dhidi yake. Mwaka 1984 Habré aliwatesa na kuwaua watu wa kabila la Sara, mwaka 1987 ilikuwa zamu ya watu wa kabila la Hadjeri na Waarabu wa Chad na watu wa kabila la Zaghawa waliouliwa na kuteswa baina ya mwaka 1989-1990.  Zaghawa ni kabila la Debby.  Habréni wa kabila la wachungaji la Toubou la kaskazini mwa Chad.
Baada ya kupinduliwa,Habré alikimbilia Senegal ambako amekuwa akiishi Ouakam, kiunga kimoja cha mji wa Dakar. Majirani zake wanampenda.Wanamuelezea kuwa ni mtu mswalihina, mfuasi wa tariqa ya ahli Sufi ya Tijaniyya na mara kwa mara wakimuona msikitini siku za Ijumaa.
Majirani zake wanaendelea kumuelezea Habré kuwa ni mkarimu na mmakinifu. Hayaingilii mambo ya mtu mwengine. Wema wake wote huo ingawaje haukumnusuru asikamatwe kwa kuua na kutesa.
Kwa muda wa miaka 22 Habré alifanikiwa kuzipiga chenga jitihadi zilizokuwa zikifanywa na aliowatesa za kutaka kumfikisha mahakamani. Rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade alifanya ajizi ya kutomfungulia mashtaka Habré kwa visingizio mbalimbali.
Mara nne Senegal ilikataa kumpeleka Habré Ubelgiji ambako 2005 hakimu mmoja aliamrisha akamatwe.  Sheria za Ubelgiji zinayaruhusu mahakama ya nchi hiyo kumfungulia kesi mtu yeyote yule aliyekiuka haki za binadamu kokote duniani.
Muungano wa Afrika (AU) ukaingilia kati na kuitaka Senegal imshtaki Habré “kwa niaba ya Afrika”.
Hatimaye Agosti mwaka jana serikali mpya ya Macky Sall ilikubalianana Muungano wa Afrika kuunda mahakama maalum yatayomfanyia kesi Habré. Kesi hiyo itapofanywa itakuwa ni mara ya kwanza kwa mahakama ya nchi moja kumfanyia kesi kiongozi wa zamani wa nchi nyingine je mkapa na salmin nilini na wao watahukumiwa kwa mauwaji walio yafanya kwa Wazanzibar...???

No comments:

Post a Comment