Thursday, July 11, 2013

UAMSHO WAKO JELA KAMATI YA MARIDHIANO TAHATHARINI NA NYINYI MUSIJE MUKAISHIA JELA KAMA UAMSHO KWA FITNA ZA WAHAFIDHINA.


MASIKINI NCHI YETU YA ZANZIBAR HAIENDELEI KWA FITNA ZA WAHAFIDHINA WALIO JAA NDANI YA SEREKALI NA KIKUNDI CHA TAARAB CHA CCM
Wala haishangazi kuona haya yanayoendelea kupitia kwa CCM na jumuiya zake, ndivyo mara zote walivyo mnawashangaa nini.
miaka ya 1995 ni hawa hawa waliotumia kila aina ya vitimbi kupaka matope upinzani ,kwa wakati ule walikuwa na dili ya kufanya uovu na kuwasingizia wapinzani eti wananchi waogope na kukataa mawazo mbadala kwa faida za wananchi licha ya propaganda upinzani taratibu ulikuwa kwa kasi na ikawa tishio kwa wahafidhina. Hatujasahau uripuaji, upakaji vinyesi na mateso kwa baadhi ya watu huu ulikuwa ni wakati halisi wa wahafidhina walishika hatamu kila kona.
haikuishia hapo zikaletwa fitna za kuwagawa wazanzibari kwa misingi ya maeneo ndipo kama mtakumbuka watu kutoka kisiwa cha Pemba walianza kupata misuko suko, kufukuzwa kazini, kubaguliwa katika ajira na kunyimwa fursa mbali mbali. katika kipindi hiki kuelekea 2000 ndipo serikalini kikaanzishwa kitengo cha GSO kudahili waajiriwa tumedokezwa kwamba kitengo hiki asili yake ilikuwa ni kuhakikisha kila mtu mwenye asili ya upinzani hapati fursa ya kuingia serikalini kilitumika ndivyo kupalilia hujma na migawanyiko katika ajira hapa Zanzibar sijuwi leo kimebadilsha dhamira yake? mambo haya yalisimamiwa na wahafidhina wa utawala wa wakati ule- kweli uhasama ukamea zaidi na ilikuwa wazi mgawanyiko wa kimaeneo umeshika kasi ingawa ulikuwa ni wa kutengenezwa, ulilelewa na ukaaminishwa kama hivyo ndivyo hali ilivyokuwa na baadhi ya vizazi vilianza kuamini hivyo. hawa waliotengeneza hivi ni wahafidhina na walitumika sawa sawa kuwagawa wazanzibari ili yao yatimie bila kuangalia mustkbali wa nchi huko mbele. Ajira wakajaa watu wa upande mmoja na wageni, kuanzia ikulu, mawizarani, vikosini na katika taasisi mbali mbali si UVCCm wala serikali wenyewe hawakupiga kelele kwamba nchi itakosa AMANI NA MSHIKAMANO WA KITAIFA kwao wao ili wadumu ni kutumia hila za kuwagawa wazanzibari ili kuhakikisha ushindi wa chama chao- mustakbali wa Zanzibar kwao si kitu.
Hivyo ndivyo mara zote walivyo kwa awamu zote hubadilisha tu mbinu na uzuri wake wanajulikana.
miaka ya 2000-2010 walikuja na staili mbaya zaidi vitisho na mateso kupitia Janjaweed ,kuanzisha makambi maeneo mbali mbali kwa ajili ya hujuma na kuzuru watu. kipindi hiki pia walipata Baraka za utawala kwani chama kiliongoza kila kitu serikalini baada ya kuasisiwa maridhiano yaliyoleta GNU viongozi wetu wakaona imetosha wakati hali ya uhasama inazidi ndivyo Zanzibar inavyotokomea na kuwaacha wenzetu wakinufaisha upande wao. Zanzibar ilitumiwa na ilikuwa kama kinyanganyiro kwa maslahi ya CCM / wahafidhina.
LA KUVUNDA HALINA UBANI.
walishazowea hawa kubebwa sana na dola na bado wanaendelea kubebwa na dola lakini kuna asilimia Fulani imeanza kupotea baada ya kuja kwa GNU- hii wahafidhina waliipinga kwa nguvu zote na mpaka leo wanalia na DR Karume . Matatizo anayoyapata kiongozi huyu asieyumba si ya bahati mbaya hata kidogo, wanamuona adui yao mkubwa kwa kule kutanguliza maslahi ya Watu wa Zanzibar na nchi ya Zanzibar kwanza, kuwaunganisha wazanzibari, na kukubali kuwaingiza walioitwa wapinzani KIKATIBA katika serikali kamwe hawatomsahau na leo ndio hizo jitihada za WAHAFIDHINA zinashika kasi ingawa inaonekana wamechelewa lakini hawajakata tama utasikia kila aina ya vitimbi. hawa jamaa ni wabaya si wazalendo hata kidogo. Zile fitna zao kwa sasa zinapata shida kukubaliwa katika baraza la mapinduzi ili kupata Baraka kama ilivyokuwa hapo awali. sasa wameona kwa hali ya GNU maslahi ya CCM yanaanza kugwaya ndio wakaona afadhali warejeshe zile zama za uhasama kwa njia yoyote ile kwa visingizio vyovyote vile.
walianza kumkejeli makamo wa kwanza wa Rais, na walifika wakati hata katika sehemu za kiserikali ambazo hawa wahafidhina wengi bado wanazishikilia humpiga chenga kiongozi huyu kwa visingizio mbali mbali lakini wamejikuta hawana namna kiongozi ni kiongozi tu.wanaendelea kuwanyima ushirikiano na kufanya hujuma katika zile wizara zinazo ongozwa na wapinzani wakijuwa itawasaidia bado mambo yame wajiya vigumu kila baya wanalopanga kuihujumu GNU linapata tabu na kogonga ukuta.
Kuelekea mchakato wa katiba mpya waliilazimisha GNU kuwadhibiti wanaharakati mbali mbali kwa kisingizio cha KUPOTEA AMANI NA UTULIVU. hiki ndio kimekuwa kichaka chao cha kufanyia hujuma . walianza kuitisha mikutano kuwatukana viongozi wa serikali kutoka upinzani, kuanza matusi na ubaguzi wa wazi na hawakuchuliwa hatuwa yoyote. baada ya kuona bado wakaitahadharisha serikali ikiwa watashindwa kuwachukulia hatuwa wa vunjifu kama wanavyo waita wenyewe basi wao watawachukulia hatuwa. hapa walilengwa UAMSHO zaidi walikuwa mwiba kwa maslahi ya CCM na VITIMBAKWIRI WAO kipindi hicho. wakapanga waliyopanga kupitia vyanzo vyao katika dola tunavijuwa vijiwe vyao na kufanya hujuma. Pale UV- CCM kuna vijana wengi wa usalama wa taifa wanafanya kazi za kichama na wamepata kazi hizo kupitia mlango wa chama huwa tayari kutekeleza lolote lenye maslahi na chama wanajulikana ni suala la wakati tu. wengi wao Ni watoto wa WAKUBWA au wana MNASABA NA WAKUBWA.Mkakati wa kuwakamata UAMSHO uliandaliwa ili kile kisingizio cha uvunjifu wa amani kiweze kufanya kazi iwepo sababu ndio kimetokea series ni kubwa lakini wengi mnaijuwa.Hawa ndio wahafidhina ilipofikia hatuwa hii SERIKALI ikalazamika kutaka isitake iingie katika kadhia si mumeona Shein  ndio kapata pa kuanzia ninin kimetokea..? mpaka leo UAMSHO wako ndani – walishasema wao watawashughulikia yalitimia.
Kwa sasa ni kamati ya MARIDHIANO na Kumuandama makamo wa rais V1. mkutano wa juzi tayari salamu zimetoka tunaangalia hatma. jitihada hizi za wahafidhina jee zitafaulu hilo analijuwa muumba lakini hata hivyo wakati ni UKUTAA
MASKINI  KISHEIN.
tatizo la Shein, si mweledi wa siasa na kalazimishwa kukubaliana na wahafidhina kwa sasa. ana wakati mgumu ingawa alikuwa na wakati rahisi bado hajachelewa ikiwa atataka. kakosa vision ya kuongoza serikali ya GNU anadhani bado CCM wako peke yao. hapa kila kitu mnakubaliana na wenzako ili muende sambamba. hii picha inayojitokeza kushindwa kuwachukulia hatuwa wahafidhina inazidi kutia doa utawala wake na bahati mbaya kapata weledi wa siasa za Zanzibar watamfundisha siasa. Shein  ana mawili ama akubali wimbi la mabadiliko yanayotakiwa na wengi au akubali wahafidhina wamuharibie na kuiharibu Zanzibar katika mikono yake
VIONGOZI ZANZIBAR ITANGILIZWE KWANZA  SHENGESHA BAADAYE.

No comments:

Post a Comment