MIAKA 50 YA UHURU WA NCHI YA TANGANYIKA NA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA NCHI YA ZANIBAR MAJI 20% UMEME 20% ELIMU 0% HOSPITALI 1% MADAWA 0% MLO MOJA KWA SIKU TAFAKARI SANA.CCM MNASHANGA LOWASSA KUPANDA DALADALA HAMSHANGAI TWIGA KUPANDA NDEGE.VIONGOZI WA CUF WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI 2015 WAKIONYESHA SHAHADA ZAO ZA USHINDI ZILIZO SAINIWA NA KUPIGWAMUHURI NA ZEC CCM HAYA HAMUNA,AIBU HAMUINI,FEDHEHA HAMUHISI,UBINADAMU UMEWATUKA,M.MUNGU HAMUMUOGOPI HEBU JIULIZENI NYINYI VIUMBE WA AINA GANI...?????
Monday, July 1, 2013
MUNAUTAKA AU HAMUTAKI MUUNGANO-SIO UHAINI KUSEMA HIVYO LEO LAKINI WALIPOSEMA MASHEIKH WETU WA UAMSHO MBONA WAMETUPWA JELA..???
Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Benki Kuu, vyama vya siasa na Uhamiaji ni miongoni mwa mambo yanayo pendekezwa kuondolewa katika gazeti la Warioba.
Mapendekezo hayo yamo katika kijitabu cha Baraza la Katiba ya nchi ya Zanzibar (Bakaza) kilichobainisha maeneo muhimu ya kufanyiwa mjadala wakati wa mikutano ya mabaraza ya katiba ya wilaya.
Mwenyekiti wa Bakaza, Profesa Abdul Sheriff, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mapendekezo hayo yatakuwa miongoni mwa mambo ya kuelimishwa wajumbe wa mabaraza ya wilaya upande wa nchi ya Zanzibar.
Alisema hakuna sababu yoyote ya maana ya Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa kuendelea kubaki kama mambo ya Muungano katika mfumo wa serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa ja Jaji Joseph Warioba.
Sheriff alisema Ibara ya 217 katika rasimu hiyo ni vema ikafutwa na kuruhusu kila mshirika wa Muungano kuwa na Benki Kuu yake itakayoweka na kusimamia sera za fedha pamoja na kuangalia mwenendo wa uchumi wa mshirika, ikiwamo kudhibiti mzunguko wa fedha wa ndani ya Jamhuri ya Muungano.
“Ni vyema nchi ya Zanzibar ikawa na mfumo wa sarafu yake na Benki Kuu yake ili iweze kudhibiti na kuendesha uchumi wake bila ya kuathirika na Muungano kama ilivyo kwa Hong Kong na Macau ndani ya Jamhuri ya Watu wa China,” alisema Profesa Sheriff.
Mapendekezo ya Bakaza yameweka sharti kuwa kama suala la Mambo ya Nje litaendelea kubaki chini ya Muungano, basi ni muhimu nafasi za watendaji na mabalozi zitolewe kwa usawa kati ya washirika wa Muungano.
.
Alipendekeza katika Ibara ya 2 ya rasimu hiyo kuingizwe haki ya nchi mshirika wa Muungano kujitoa kwa kutumia utaratibu wa kura ya maoni baada ya wananchi wa mshirika husika kuridhia kupitia kura ya maoni.
Bakaza wameunga mkono wazo la Mwanasheria Mkuu mstaafu, Jaji Mark Bomani ya haja ya kwanza kuitishwa kura ya maoni kwa ajili ya kuwauliza watu wa pande zote mbili kama wanautaka Muungano au laaa hawautaki muungano.Hii ni ishara moja ya na nyengine nyingi zitafuatia kuwa wote sasa waana anzaa kufuata njia ile ile waliyokuwa wakisema aumsho na kuonekana kuwa ni wachocheze na wafanya furugu kumbe ile ndio haki na ndio njia peke ya ukweli wakumaliza matatizo haya ni kuwa kwanza waulizwe Watanganyika MUNAUTAKA au HAMUTAKI na wakati huwo huwo waulinzwe Wazanzibari MUNAUTAKA au HAMUTAKI jawabu likitoka basi ndio lakufatwa na sio watu kutishana na ubabe.
Bakaza inatarajia kuanza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu yaliyomo kwenye rasimu hiyo katika kipindi ambacho mabaraza ya wilaya pamoja na ya kitaasisi yanajiandaa kukutana kwa ajili ya kuichambua rasimu na kuitolea maoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment