Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Katiba ya Misri, Adly Mansour ameapishwa jana kuongoza Serikali ya mpito.
Jeshi la Misri limempindua Rais Mohamed Morsi na kumteua Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Katiba, Adly Mansour kuongoza Serikali ya mpito.
Akihutubia kupitia televisheni ya taifa ya Misri, Mkuu wa Jeshi la Misri, Jenerali Abdel-Fatah El-Sisi alisema itaundwa kamati ya mapatano ili kurudisha amani na umoja wa kitaifa.
Wakati Jenerali El-Sisi akitangaza mapinduzi hayo, alikuwa amezungukwa na viongozi wa jeshi, dini na wanasiasa maarufu.
Kiongozi mwandamizi wa Chama cha Muslim Brotherhood, alisema Morsi amewekwa kizuizini katika kituo cha jeshi akiwa na wasaidizi wake.
“Morsi na timu yake ya wasaidizi wanashikiliwa na Kikosi cha Wanajeshi Wanaomlinda Rais kinachoitwa Presidential Republican Guard,” alisema Gehad El-Haddad ambaye mtoto wa mmoja wa washauri wakubwa wa Morsi wakati alipohojiwa na Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) jana. Baba yake, Essam El-Haddad pia amewekwa kizuizini.
No comments:
Post a Comment