Monday, May 30, 2011

MADEREVA WA VIONGOZI WALIA KWA KUTUMIKISHWA KAMA PUNDA


TUNA AMBIWA ZNZ NI NCHI MASIKINI MAGARI YA VIONGOZI
NI KAMA HAYA JE UMASIKINI HUO NI KWA RAI TU......?
 

BAADHI ya madereva wa wabunge,wakuu wa polisi,majenerali, mawaziri na naibu wao wamewashutumu mabosi wao kwa kuwatumia zaidi kama wafanyakazi wa nyumbani, jambo ambalo ni kinyume cha taratibu.

Madereva hao pia wamelalamikia magari ya serikali kutumika vibaya ,kinyume na taratibu za kazi.Baadhi yao waliozungumza na mwandishi wetu na  kwa maombi ya kutotajwa majina walidai kuwa, wamekuwa wakifanyishwa shughuli kuanzia asubuhi hadi usiku wa manane kwa wiki nzima, katika mambo ambayo si ya kiofisi.

"Tunaomba matumizi sahihi ya gari la serikali yazingatiwe na maslahi ya madereva yaangaliwe kwa kina kwa kuwa, tunafanya kazi saa nyingi na kipato ni duni hususan kwa madereva wa mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi," alisema mmoja wa madereva hao na kuongeza:
"Hatuna mapumziko, wala sikukuu. Kila siku tupo kazini kwa kuwa waziri anapojisikia kukutuma hata kama ni shughuli yake ya nyumbani, anafanya atakavyo na huwezi kumkatalia maana ukimkatalia unaweza hata kufukuzwa kazi kisha sisi tunafamilia zetu zenatutengemeya kwa hiyo tunatumika tu kama mapunda."

Waliongeza kuwa kutokana na kutumika hivyo kwa kuwatii mabosi wao na kuwafanyia shughuli kwa matakwa yao, wamekuwa wakikosa hata nafasi ya kukaa na familia zao kama inavyostahili.Walidai kuwa kipato chao ni cha chini, lakini hukitumia kufanyia usafi na kuyatunza magari hayo yaliyonunuliwa kwa gharama kubwa na serikali, lakini watunzaji hao hawathaminiwi.

Walisema kuwa mshahara wao hauzidi Sh 200,000 wakieleza kuwa ajira yao iko katika 'Operation Service' jambo

ambalo linawafanya washindwe kuwa na kiwango cha mshahara kinachowawezesha kukopa kiasi cha fedha ambacho kingewawezesha kuanzisha mradi wowote wa kujiendeleza maana mshahara hauwatoshelezi katika mahaitaji yao na familia zao.

Kufuatia hali hiyo, wameiomba Ofisi ya Rais ya Utumishi wa Umma kushughulikia tatizo hilo na kuangalia maslahi yao kutokana na kazi wanazozifanya au kuzungumza na viongozi hao wanaowatuma kama punda.

Pia, wamemwomba Raisi, kuangalia suala la wao kuwekwa kwenye 'Operation Service' kwa muda mrefu huku kazi wanazozifanya ni kubwa na kukosa hata usingizi wa kulala na familiya zao na siku ya pili kama kawaida kazi mtu ambazo kazi hizo si za serekali kabisa.

Imedaiwa kuwa viongozi  hao wamekuwa wakitumia magari hayo kwenda kwenye starehe ikiwemo baa au disco au kwenye nyumba za mahawara wao yani wanawake wasio kuwa wake zao na imethibitika kuwa wengi wa viongozi wanawanawake wa nje zaidi ya wawili.pia huwafanya madereva hao kuwasubiri nje ya nyumba za hao wanawake wao wa nje na huku wao kuendeleya na starehe zao na  kuwaacha madereva wao wakiwasubiri kwa muda mrefu wao wakiendeleya kustarehe, jambo ambalo ni kinyume na taratibu za serikali.

Magari hayo ya serikali pia yanadaiwa kutumika kwa shughuli binafsi zikiwamo za kuendea shambani,kumtembeleya bibi na babu, kufuatilia ujenzi wa nyumba wanazozijenga pia imethibitika kuwa wanajenga nyumba mbili mpaka tatu kwa wakati moja, kupelekea watoto shule,au kuwapeleka wanawake wao wa nje sehemu mbali mbali kama sokoni,kwa fundi charahani anaye mshoneya nguo au hata kwa marafiki zake huyu mwanamke wa nje ambaye sio mke wake pamoja na kwenda kanisani au msikitini.

No comments:

Post a Comment