Wednesday, May 4, 2011

MAKUCHA YA SHEIN YA ANZA SASA KUJITOKEZA HATHARANI


je wananchi mutanichangua tena ili nilete 5star hotel nyingi zanzibar?

SMZ AU SUK ((GNU) yaruhusu hoteli ijengwe Mji Mkongwe 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amempendeleya zaidi mwenye hotel hiyo thaidi ya wananchi wake kuhusu mradi mkubwa wa ujenzi wa hoteli yenye hadhi ya nyota tano eneo la Mji Mkongwe baina ya mwenye hotel hiyo na rai wa zanzibar..

Kampuni ya Zamani Zanzibar Kempinski imo katika hatua za mwisho kujenga hoteli hiyo baada ya kukamilisha taratibu zote serikalini ikiwemo kufuata na kuzingatia sheria za uhifadhi na uendelezaji wa Mji Mkongwe unaolindwa kimataifa.
“Kama kuna watu wanataka kwenda mahakamani kupinga ujenzi waache waende, lakini uamuzi wa Serikali utabaki pale pale kwamba ujenzi wa hoteli iliyokusudiwa utaendelea,” alisema Dk. Shein katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu usiku.
Dk. Shein alifanya mkutano huo na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kurejea kutoka ziara ya kiserikali nchini Uturuki, na aliulizwa swali kuhusu pingamizi inayokusudiwa kuwekwa kuzuia ujenzi wa mradi wa hoteli na msimamo wa Serikali.
“Ile ni mali yetu hakuna wa kutuzuia na nataka kusema kuwa hili jambo Serikali imeamua, sasa sioni tatizo liko wapi kwani mtu akiamua kuuza chake, nani atakuzuia…hakuna,” alisisitiza.
Mkazi mmoja wa Unguja, Juma Ali Khatib na wenzake, wanakusudia kuishitaki Serikali kupinga ujenzi wa hoteli hiyo wakidai utaratibu wa uuzaji wa mali za umma umekiukwa.
Vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya Serikali vinaeleza Kampuni ya Kempinski imelipa Sh bilioni 2.8 kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na fedha hizo kuwekwa katika Hazina ya Serikali.
Chini ya mradi huo, Kampuni ya Kempinski inatarajia kuwekeza Dola za Marekani milioni 30 zitakazohusisha ukarabati wa jengo la kihistoria la Mambo Msiige, ujenzi wa bustani ya kisasa na hoteli yenye hadhi ya nyota tano itakayojengwa ilipokuwa Starehe Klabu.
Utaratibu ukodishwaji wa ardhi kwa mgeni Zanzibar ni hekta moja ikiwa sawa na eka 2.4 inakodishwa kwa Dola za Marekani 5,000 kwa mwaka ambapo Kempinski eneo alilokodishwa halijafikia hata eka moja wamekodishwa kwa Dola 10,000 kwa mwaka.
Dk. Shein amewahakikishia wananchi kwamba miradi hiyo itazingatia sheria za uhifadhi na uendelezaji wa Mji Mkongwe wa Zanzibar unaotambuliwa kuwa ni urithi wa dunia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Nchini Tanzania, Kampuni ya Kempinski imewekeza katika miradi mikubwa ya hoteli za kitalii zenye hadhi ya nyota tano ikiwemo Zamani Zanzibar Kempinski, Bilila Lodge, Kempinski Serengeti, Hotel Ngorongoro Kempinski na Kilimanjaro Hotel Kempinski.


susu 04/05/2011 kwa 6:45 mu · Jibu
Mali ya serikali ni mali ya wananchi. Wananchi wakikataa kuuzwa kwa mali ya serikali, serikali haitakiwi kuuza, na ikiuza itakuwa inawadhulumu wananchi. Huu ni UDIKTETA.


WATU WALIFIKIRI KUWA SUK AU GNU NI MTETEZI WA WANYONGE ALIKUWA KABANA MAKUCHA NDANI SASA TARATIBU YANACHOMOZA TEMBO HOTEL TU UKIPITA UFUKWENI UNAMBIWA MWIZI NA WEWE NI MZANZIBAR JE 5STAR HIYO IKISHA JENGWA ITAKUWA VIPI?
WAZANZIBAR BADO HATUNA VIONGOZI KABISA WEWE USHAWASIKIYA WANCHI WAKO WALIO KUCHANGUWA KUWA HAWATAKI SASA HUYO MAKAPISKI SIJUWI NDIYE MUHIMU ZAIDI KULIKO WANCHI WALIYO KUPINGIYA KURA NA KUKUPA IKULU UNAYOKULA KUKU UKASHIBA KISHA UKAJA KUWATOLEA UFETHULI ATI NENDENI MUKASHATAKI ANGALIYA KEBEHI ALIZO NAZO.
UKISIKIYA UDIKTETA NDIO HUWO WANCHI HAWATAKI WEWE UNAWALAZIMISHA KISA WEWE NDIYE WAZIRI HUNA WIZARA SINDIVYO WATANGANYIKA WANAVYOKUJUWA SAWA 1015 WAKATI WA UCHANGUZI MUAMBIYE((Nchini Tanzania, Kampuni ya Kempinski imewekeza katika miradi mikubwa ya hoteli za kitalii zenye hadhi ya nyota tano ikiwemo Zamani Zanzibar Kempinski, Bilila Lodge, Kempinski Serengeti, Hotel Ngorongoro Kempinski na Kilimanjaro Hotel Kempinski)) WAKUTILIYE KURA ILI UWE TENA WAZIRI HUNA WIZARA SIO WAZANZIBAR.



No comments:

Post a Comment