HAROUN SASA HIZI NDIO SCHOOL ULIZOJENGA?
UNAGHAGHANIYA MADARAKA NA HUNA MOJA UNALO
LIFANYA UMESHINDWA KUFANYA KAZI YAKO JIUZULU
USILETE ZA SIJUWI WAZIRI HUYU WALA YULE WEWE JIUZULU
KISHA NAWENGINE WATAFUATIYA IKIWA HAWATIMIZI KAZI
ZAO KAMA WEWE USHAWAFELISHA WATOTO SASA UNAIMBA
PIA WATU HAWATAKI TENA MUUNGANO SASA WEWE BADO UNA
WASAPOTI WATANGANYIKA BASI NENDA HUKO TANGANYIKA UKAWE WAZIRI WA ELIMU HUKO ILA ZNZ JIUZULU WACHA UROHO WA MADARAKA WANANCHI WANATAKA MAENDELEYO SIO VIJIZAWADI
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Haroun Ali Suleiman amesema haoni sababu za msingi za kuchukua hatua ya kujiuzulu wadhifa wake kutokana na wanafunzi kutoka Zanzibar kufanya vibaya katika kidatu cha nne mwaka huu.
Tamko hilo amelitoa jana katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake Mazizini Mjini hapa baada ya kujitokeza shindikizo kutoka kwa baadhi ya wananchi na wana siasa wakimtaka achukue uamuzi huo.
Amesema utamaduni wa kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya ya mitihani ya wanafunzi haupo Zanzibar na kama ungekuwepo hata kiongozi wa upinzani Maalim Seif Sharif Hamad asingesalimika kutokana na matokeo ya mitihani ya mwaka 1980.
Waziri huyo ambaye aliingia na urodha ya takwimu za viwango vya kufaulu kuanzia mwaka 1971 hadi mwaka 2008 alisema hivi sasa kumlaumu yeye ni kumtupia lawama zisizo na msingi kwa vile suala la kupasi wanafunzi limekuwa likipanda na kushuka.
Akitoa mfano mwaka 1971 kiwango cha kufaulu kilikuwa asilimia 99.5 lakini mwaka 1980 kilifikia asilimia 77.7 na mwaka 1984 kilifikia asilimia 55.2 na hakuna mwanasiasa yoyote aliyechukua uamuzi wa kujiuzulu.
Ingawa Waziri Haroun hakumtaja jina mwanasiasa huyo lakini kipindi hicho Waziri way Elimu alikuwa ni Maalim Seif Sharif Hamad na baadae kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
“Suala la kujiuzulu halipo Zanzibar na kama lingekuwepo wengi lingewagusa kwa sababu suala la wanafunzi kufaulu inategemea na msimu wakati mwengine hufnaya vizuri na wakati wmengine hufnaya vibaya bila ya kutarajia” alisema Ali.
Alisema wananchi wa Zanzibar wanapaswa kuipongeza Serikali ya Mapinduzi kwa juhudi wanayochukua ya kuinua sekta ya elimu kwa vile hivi sasa shule za sekondari zimefikia 134 kutoka 6 kabla ya mapinduzi mwaka 1964.
Alisema wakati anateuliwa kuwa waziri mwaka 2001 kiwango cha kufauulu kilikuwa asilimia 77.5 lakini kilipanda hadi kufikia asilimia 90.9 mwaka 2005 lakini jambo la kushangaza hakuna mwanasiasa au mwananchi aliyechukua hatua ya kumpongeza kutokana na juhudi zake za kuinua elimu.
Waziri huyo alisema matokeo ya mwaka huu yeye binafsi yalimsononesha kwa vile kiwango cha kufaulu kimeshuka kutoka asilimia 88.6 mwaka 2007 hadi asilimia 77.3 mwaka huu.
“Jambo la busara wazazi wasimamie vizuri maendeleo ya watoto wakati serikali tunachukua hatua za kuboresha mazingira yaliopo hivi sasa na tayari tumeondoa uhaba wa vitabu vya sanyansi kwa kushirikiana na Shirika la USAID na tunatarajia kujenga shule za sekondari 19” alisema Waziri huyo,
Hata hivyo Waziri Haroun alikiri kuna shule tatu zimefanya vibaya Kisiwani Pemba lakini suala hilo alisema isilaumiwe serikali peke yake kwa vile kumejitokeza tabia ya baadhi ya walimu kufanya kazi kisiwani humo wanapomaliza elimu ya juu.
Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar bado ina imani na baraza la mitihani katika utaratibu wake wa kusimamia mitihani hiyo na hakuna upendeleo wowote kati ya wanafunzi wa bara na Tanzania bara kwa vile Zanzibar wana uwakilishi wa kutosha katika mfumo wa uongozi wa baraza la mitihani.
Alisema makamu mwenyekiti wa baraza hilo anatokea Zanzibar na kuna wajumbe wawili ambao wamekuwa wakishiriki vikao vyote vya maamuzi na kuwataka wananchi kuondosha wasi wasi kuhusiana na suala hilo.
Akizungumzia hata ya kuwepo wizara moja alisema hakuna sababu ya kuwa na wizara moja ya elimu kwa vile suala la elimu ya juu ndio suala la pekee liliopo katika orodha ya mambo ya muungano kwa mujibu wa katiba ya muungano na mambo mengine kila upande unasimamia mambo yake ya elimu kupitia serikali ya Zanzibar na ile ya muungano.
Mapema juzi Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma Salim Bimani alimataka waziri Haroun kuomba radhi wazee na vijana wa Zanzibar kwa kushindwa kwake kusimamia vyema majukumu ya kuinua na kukuza elimu visiwani Zanzibar.
Alisema kuwa ni jambo la kushangaza idadi kubwa ya wanafunzi wanaofanya vibaya katika mitihani kidatu cha nne wakati elimu ndio msingi way maisha yao.
“waziri awe muungwana kwa kukubali mwenyewe kujiuzulu wadhifa wake kutokana na kufeli kwa wanafunzi” alisema Bimani.
Tangu kutangazwa matokeo ya kidatu cha nne baadhi ya wananchi zanizbar wamekuwa wakijadili suala hilo kwa mtazamo tofauti na wengine kuibebesha lawama serikali kuwa mazingira duni, ikiwemo ukosefu wa madawati, maslahi duni ya walimu kuwa chanzo cha kuzorota kwa elimu visiwani zanzibar.
No comments:
Post a Comment