Tuesday, May 10, 2011

JE WAZENJI TUKO TAYARI KUANZISHA CHAMA CHENGINE CHA WZANZIBAR TU....?KISICHO HUSISHA WATANGANYIKA

Na CCM-ASP Zanzibar
Wazanzibari wengi hawawezi kutofautisha baina ya serikali ya Muungano ( Tanzania ), Tanganyika , CCM-Kampuni/Kanisa na CCM-TANU (inayoiburuza CCM-ASP), wao wanahisi wote hawa ni neno moja.
Nyerere alikuwa mpole sana akifika Zanzibar na wala alikuwa hafanyi mambo ya kuwakera wazanzibari kwasababu alijua hasara zake, na alikuwa anafanya mambo yake taratibu hayuko tayari kufa ili kuikamilisha mbinu na ndoto yake ya kuimeza Zanzibar , ambayo inasemekana ingechukua muda wa miaka 100 kuikamilisha. Sasa chakushangaza CCM-TANU na CCM-Kampuni wakileo wanatafuta njia za mkato hata miaka 50 haijafika wameshaanza kuwakejeli Waungwana ambao kwa miaka mingi wameonekana kuwa wapole na wastaarabu mbele ya Watwana, wanajinafasi wakati bado safari yao ni ndefu hata nusu hawajaifikia. Wakati mwengine ni kosa la Watanganyika kutokufanya utafiti na kuwaamini zaidi baadhi ya viongozi wa CCM-ASP wanaojipendekeza na walionauchu wa madaraka kwa kuwapa ripoti feki juu ya wazanzibari na badala yale Watanganyika wanapofika Zanzibar mambo ni tofauti wanapigwa na butwaa.
Makosa makubwa yaliyofanywa na CCM-TANU ambayo yamewafanya Wazanzibari kumjua mchawi wao na makosa ambayo hayazibiki, Ufa wake unaongezeka taratibu siku hadi siku ni :- Kuliendeleza neno MAPINDUZI DAIMA kwa kejeli hata baada ya Maridhiano ya Zanzibar, Kuleta mbinu ya kizamani ya wakoloni Wagawe Watawale , kuitangaza Zanzibar kuwa si nchi, Kuingiza Mafuta kwenye mambo ya Muungano, Kuwachagulia CCM-ASP Raisi , Kujificha kwa Tanganyika ndani ya Muungano ,Kuleta Utumbo wa Katiba ya Muungano kuipiku katiba ya Zanzibar kipindi ambacho kuna maridhiano kwa lengo la kuleta Uchochezi wa Machafuko na kumwaga damu Zanzibar.
Sasa hivi wamejivua Gamba la Nyoka muda mfupi tu baada ya kuwakera wazanzibari na kutegemea wazanzibari wawe na imani na Watanganyika. CCM wamejivua Gamba muda mbaya sana, na walichokifanya ni kuwaondoa viongozi mafisadi na wamechagua viongozi Mumiani (wanyonya damu wala watu ambao hawana urafiki na watakitenganisha chama na wananchi wa Zanzibar), huku ni kutangaza vita baina ya chama na wananchi hamujui kama baada ya kujiroga sasa munakula chano chenu wenyewe , maana chama ni wananchi na siku zote wananchi ndio watashinda vita
Kujivua gamba kwa CCM-TANU kuna maana kubwa na nzito sana kuliko wepesi wa neno wenyewe linavyoonekana. Kila mtu ametabiri vyake, Wengine wametabiri kuwa kuwa sasa hivi wamevua gamba la nyoka kwa lengo la kukiri uovu wao walioufanya kabla, kuonekana wapya na kujisafisha kwa kutubia makosa yao, au pengine kujivua gamba kuonekana kijana na kuongeza sumu ya kutafuna, na wengine wanafikiri kuwa lile gamba ni kama ngozi ya Kondoo ambayo walikuwa wakionekana wema au gamba kongwe kuonekana wazee wenye hikma kwa muda mrefu na sasa hivi wameamua kuvua gamba na kutoka hadharani na kutomuonea haya mtu. Yote hayo yanamantiki ndani yake , lakini mimi naungana na wale wanaodhani kuwa huenda CCM-TANU ikafa moja kwa moja lakini ikazaliwa ndani ya chama kingine cha upinzani na kuendeleza ule ule ukoloni wa mwanzoni wa kuimeza Zanzibar kwa kutumia jina jipya na watu wapya wakiongozwa na wale wale wazamani Christian Church Movement ( CCM ). Hapa ninawataja zaidi Christian Church Movement – TANU kwasababu ni miezi michache tu iliyopita asilimia kubwa ya wazanzibari wametanabahi wengi wao hawapendezwi na kusifia ‘’Mapinduzi’’ yaani kusifia Vifo vya Waislamu Babu zao ( wengi wanaoshadidia sifa hizo ni Wazanzibara ) na pia wametanabahi kuwa hapa Zanzibar hakuna historia ya chama kinachoitwa Chama Cha Mapinduzi, na wala hili jina halijulikani lilianzia wapi kwasababu halina uhusiano wowote na Chama kilichofanya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kujivua Gamba la Nyoka au Ngozi ya Kondoo, huko kote ni kutapatapa kwa Watanganyika jinsi ya kuimeza Zanzibar , kwasababu kama kweli hawa ndugu zetu wanania njema ya kukinusuru chama cha Christian Church Movement ( CCM ) basi wangefanya kile ambacho wananchi wa Tanganyika na wazanzibari wanakitaka. Kwa upande wa Zanzibar hata ukimuuliza mtoto mdogo anauwezo wa kutamka kwa ufasaha kabisa kwa kile ambacho Wazanzibari wenzake wanakitaka. Kwa Watanganyika kujifanya wajanja kutotekeleza matakwa yao basi huko ndio kujichimbia kaburi kwa Christian Church Movement-TANU kwasababu sio muda mrefu ASP ( Wazanzibari) watajitenga na TANU pamoja na KAMPUNI kukosa mwega. Wazanzibari wanaweza kuishi kwa amani zaidi pale ambapo hakuna watanganyika na vyama vyao vya siasa.
Siku zote Sumu ya Watanganyika imo ndani ya vyama vya siasa, na ukitaka kujiepusha na sumu hii basi ni kuchagua viongozi wasiokuwa na vyama vya siasa au kushirikiana kwa pamoja viongozi wa Zanzibar bila kuburuzwa na vyama vyao. Baadhi ya wazanzibari wanajua kuwa kinachowaunganisha Zanzibar na Tanganyika sio Muungano Feki (kisheria haupo) bali ni vyama vya siasa tu. Na iwapo kama wazanzibari wakitofautisha baina ya Serikali ya Zanzibar, jeshi la Polisi na chama kinachoongoza nchi CCM ( Christian Church Movement ), na wakiamua kuvigawa vyama vya siasa kubaki na ASP na TANU, au kuvisusa vyama vyote CUF na CCM wasiwe na chama chochote, au wakianzisha vyama vyao vya siasa visivyofungamana na watanganyika, basi watanganyika hawatokuwa na nguvu yoyote ya kuingilia mambo ya ndani ya Zanzibar ambayo ni nchi huru na yenye mamlaka yake kamili. Jiulize swali Watanganyika wataanzia wapi kuingilia mambo ya Zanzibar iwapo kama hawana Chama wala Dini yao huku kwetu? Ukiangalia historia ya vitendo vyote vya kuimeza Zanzibar vinapitishwa ndani ya CCM na wala serikali ya Muungano haina nguvu ya kuimeza serikali ya Zanzibar , iwapo kama hakuna CCM-TANU inayoiburuza CCM-ASP.
Kujivua Gamba kwa CCM-TANU hakuna faida kwa CCM-ASP wala wazanzibari bali ni hasara kubwa sana kwa serikali ya GNU iwapo kama hawatokuwa makini, ni lazima viongozi wetu wadumishe ushirikiano ndani ya serikali ya Zanzibar na pia kujaribu kujinasua na vyama vyao vya siasa, kwani hivyo ndivyo vinavyowaunganisha viongozi wetu wa nchi na watu waovu wasiokuwa raia wa nchi yetu na wenye nia mbaya na maendeleo yetu. Ubaya zaidi hata vyama vya upinzani vinalijua hili lakini siku zote vinanyamaza kimya kwasababu pengine tukijivua gamba la vyama vya siasa na kuijenga serikali ya Zanzibar ambayo itachagua viongozi kutoka kwenye jumuia binafsi na taasisi za serikali kutoka kila mkoa, huo ndio utakuwa mwisho wa ajira za wanasiasa Tunajua viongozi wetu hawakotayari kuliona hili, lakini kutokana na TANU walivyojivua gamba hali sio shwari tena kama ilivyokuwa zamani, na sasa hivi kwa wazanzibari hawana mbinu nyingine yoyote iliyobaki, utakapokaa kutafakari na kufikia upeo wa kufikiri utagundua kuwa sasa hivi sio sunna tena bali ni faradhi kwa CCM-ASP kujitenga kwa lengo la kuinusuru Zanzibar.
Kwanini Katibu Mkuu wa CCM hawezi kutoka Zanzibar ? Tunashindwa na hata vyama vipya vya upinzani. Mimi niliposikia Chama chetu kimejivua Gamba nilifurahi sana nilitarajia kimezaliwa upya na kuja na fikra mpya za kisomi na za kisasa kwa lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi na kukiokoa Chama ambacho kiko Hoi Bin Taabani. Nilitarajia kimebadilisha jina na kuweka neno ‘’Maendeleo’’ na kuliondoa neno ‘’Mapinduzi’’ ambalo haliingii akilini kwa wananchi wengi hususan kwa Wazanzibari Alwatani ni kama kuwakejeli. Pia nilitarajia kwa mara ya kwanza yanafanyika mabadiliko kwa Mwenyekiti wa CCM kutoka Zanzibar kitu ambacho hakijawahi kufanywa na chama chochote cha upinzani, ili kuonesha Umma kuwa zilizoungana ni nchi mbili na kila nchi inauwezo sawa wa kutoa Mwenyekiti, sio lazima Mwenyekiti atoke Tanganyika na Katibu Mkuu atoke Zanzibar. Matokeo yake ni kuvunjwa moyo kwa wazanzibari hata huyo Katibu Mkuu wanadodishwa kama rambi rambi. Kilichoonekana ni majaribio tu ya kulivua Gamba la CCM-TANU kwa kubadilisha sura za watu na kulipangusa vumbi gamba la CCM-Kampuni kwa kuwabadilisha vyeo mafisadi na matajiri / wafadhili na pia Kanisa kunyoosha mkonge wa tembo kwenye vyama vya upinzani. Lakini tunathubutu kusema kuwa kwa huku Zanzibar gamba hata halijaguswa. ( Wazanzibari wameelimika kwenye siasa na kijamii , kila raia anajua haki zake hawaangalii sura ya mtu, wala kupotezewa muda kwa kusikiliza taarifa za kuoteshwa za maji ya babu, isipokuwa wanaangalia chanzo cha matatizo yao kiko wapi , na tayari wameshagundua hicho chanzo hata vumbi bado hakijafutwa ).
Huku ni kutapatapa kwa mfa maji, Chama hakitakiwi kujiandaa na uchaguzi isipokuwa kinaandaa sera za kuwaletea maendeleo wananchi na baadae ndio wananchi watakipigia kura na kupata ushindi, kinachofanyika sasa ni kuwapotezea muda wananchi kwa kila miaka 5 ni kujiandaa na uchaguzi tu. Lakini bado ninaimani kuwa chama kimetoa miezi 3 ili Gamba lote limalizike kuvuka na kiweze kujisafisha zaidi ili ile minong’ono ya CCM-ASP kujitenga ifutike, na wasipojisafisha na kubadilisha jina la Chama ndani ya miezi 3, sasa itabidi kabla ya uchaguzi ujao livuliwe Gamba jengine pamoja na Ngozi, na hapo ndio utakuwa ndio mwisho wa uhai wa Christian Church Movement ( CCM ).na ndio mwanzo wa cha kipya cha wazanzibar ndio tunacho kihitaji sasa cha cha wazanzibar ambacho kitawapinganiya watu wa zanzibar. bila ya kuwashirikisha watanganyika maana CCM kimeunganishwa na bara na CUF pia kimeunganishwa na bara. sasa hata kama CUF ikishinda watatumiya waya ule ule kuwakandamiza wazanzibar kilichobaki sasa nikuwa na cha hapa hapa zanzibar ambacho hakihusiyani na watanganyika hata kidongo. ndio tutajikombowa ishaa allah tushikamane sote wazanzibar letu liwe moja tu basi na ni zanzibar kuwa huru na uhuru wake na wananchi wake na kila kitu kiendeshwa na wazanzibar. kuanzia raisi,makamo,mawaziri,wabunge,makatibu,majeshi,polisi,hospitali na airport na bandarini,kila kitu ni wazanzibar wenyewe ndio nchi itainuka na mimi namini haya tunaweza kufanya wenyewe na ustarabu wetu na hashima yetu ya watu wa zanzibar. mimi namini kabisa na  nawaomba wazanzibar sote tuliyokuwepo hapa zanzibar na nje pia tuwe na msimamo moja tu zanzibar zanzibar zanzibar na allah atatusaidiya ishaa allah
Mungu Ametubarikia Unguja na Pemba visiwa vyelivyo na nemaa na baraka pia na iko siku Sote Tunashangiria INSHAA ALLAH

No comments:

Post a Comment