WAWEKEZAJI katika sekta ya utalii Kisiwani Pemba wamelalamikia tatizo la miundo mbinu na ukosefu wa bidhaa muhimu zinazohitajika kwa watalii kukosekana jambo ambalo limekuwa likichangia kukosekana kwa watalii wengi kisiwani humo.
Wawekezaji hao wameyaeleza hayo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad katika ziara yake kisiwani humo ambapo alitembelea maeneo mbali mbali ikiwemo katika sekta za utalii ambazo kwa ksi kikubwa zinachangia pato la taifa nchini.
Meneja wa Pemba Misali Beach Resort, Ajuwedi Mrisho alisema ukosefu wa bidhaa muhimu, ikiwemo pombe, mboga mboga na baadhi ya vyakula vyenye viwango vinavyohitajika na wageni ni tatizo linalowakabili katika hoteli zilizopo kisiwani hapo ikiwem hoteli yake
Alisema tatizo hilo limekuwa likiwarejesha nyuma wawekezaji kwa kuwa wageni wengi wanapokuja katika hoteli za kitalii wanategemea kupata huduma za vinywaji na vyakula vyenye viwango hivyo kukosekana kwa huduma hizo muhimu kunawafanya wanapoondoka kutorejea tena katika hoteli hizo.
Alisema ingawa pombe hupatikana kwa baadhi ya wakati lakini mara nyingi hukosekana kama ambavyo hukosekana kwa mboga mboga ambapo kilimo cha mbogamboga bado hakijapewa msukumo mkubwa kisiwani humo na wamekuwa wakitegemea bidhaa kutoka tanga na sehemu nyengine zaTanzaniabara .
Kwa upende wake Meneja wa Hoteli ya Mbuyu Mkavu Resort, Seif Said alimweleza Maaalim Seif na ujumbe wake kwamba wamekuwa wakiendesha biashara zao kwa hasara kutokana na ukosefu wa maji safi na salama na jinsi tatizo la umeme linavyowaathiri katika uendeshaji wa hoteli yake iliyopo Wawi Mkoa wa Kusini Pemba.
Alisema tatizo hilo linakwamisha lengo lake la kutoa ajira kwa vijana wapatao 150 na badala yake ameweza kuajiri vijana 15 pekee sambamba na kushindwa kuongeza vyumba kwa ajili ya wageni kutokana na mapato duni anayopata na kuiomba serikali kulichukua suala hilo ili kulifanyia kazi kwani wanafanya biashara katika mazingira magumu sana.
Akijibu malalamiko ya wawekezaji hao wazalendo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sherif Hamad amekiri serikali ya umoja wa kitaifa kukabiliwa na changamoto kadhaa katika utekelezaji wa mipango yake hasa katika sekta ya utalii lakini aliwaahidi wawekezaji hao kufuatiliwa malalamiko yao na kupatiwa ufumbuzi kwani serikali inajitahidi kukabiliana na changamoto zote zilizopo.
Alisema katika juhudi za serikali za kuimarisha sekta ya Utalii nchini serikali inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo miundo mbinu katika sekta ya barabara katika maeneo mbali mbali Kisiwani Pemba na miundo mbinu ya maji na umeme wa hakika katika baadhi ya maeneo.
Maalim Seif ameyasema hayo juzi kwa katika ziara yake ya siku mbili kutembelea miradi ya hoteli za kitalii zinazomilikiwa na wawekezaji wazalendo katika maeneo ya Vitongoji na Wesha huko Kisiwani Pemba ambapo katika ziara yake alifuatana na waziri wa Habari Utamaduni na Utalii, Abdillah Jihad Hassan na maafisa wa wizara yake..
Sekta ya utalii Kisiwani Pemba bado haijaimarika kutokana sababu mbali mbali ikiwemo ukosefu wa miundo mbinu ya barabara, ukosefu wa umeme wa uhakika na tatizo la majisafina salama katika maeneo kadhaa ya kisiwa hicho hasa katika maeneo yenye hoteli hizo kubwa za kitalii.
Kufuatia hali hiyo Maaalim Seif amesema mbali na changamoto hizo ambazo serikali ya umoja wa kitaifa inakabiliana nazo lakini serikali itaendelea kuthamini juhudi za wananchi katika kukuza sekta hiyo yenye kuongeza pato la Taifa, kutoa ajira na fursa za kibiashara kwa wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya uwekezaji huku akiwapa moyo wawekezaji wazalendo kuendelea na juhudi za uwekezaji nchini
Akizungumzia matatizo yanayowakabili wawekezaji hao, Maalim Seif alisema Serikali itayazingatia matatizo na changamoto zinazowapata wawekezaji hao hasa wazalendo kwa umakini mkubwa kwa lengo la kuyatafutia ufumbuzi wake ili kuvutia wawekezaji zaidi kuja kuwekeza katika kisiwa hicho ambacho kina utajiri wa rasilimali zake za asili.
Makamu wa kwanza wa rais alisema Serikali ina dhamira ya kulitafutia ufumbuzi tatizo la usafiri wa anga linalokikabili kisiwa hicho kwa kupanua na kuimarisha uwanja wake wa ndege,ili kutoa fursa kwa mashirika ya ndege kutoa huduma zao kwa uhakika na kuwepo ushindani, hatua itakayopunguza viwango vya nauli za ndege kwa watalii ili wafike katiak kisiwa hicho kwa lengo la kutanua biashara zaidi kisiwnai Pemba.
Aidha Maalim Seif aliwapongeza wawekezaji hao kwa mchango wao mkubwa kwa taifa licha ya kukabiliwa na changamoto hizo lakini wameweza kuwekeza katika nchiyaohuku wakikabiliwa na mazingira magumu katika uendeshaji wa miradi hiyo lakini bado hawajavunjika moyo katika kuwekeza nchi kwao.
Katika ziara hiyo ya siku mbili Makamu wa kwanza wa Rais alipata fursa ya kuyatembelea makumbusho yaliopo mjini Chake, ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya siku ya Makumbusho duaniani.
MIMI naona kama mrisho wewe sema kweli kuwa unataka wewe hiyo pombe. usisingiziye watali kuwa ati hawarudi tena kisa hakuna pombe na mboga mboga unayosema wewe tushaijuwa sisi ni kiti moto yani nguruwe usitake kufanya watu wapumbavu hapa.watali wengi wanaokuja africa hawaji kwasababu ya kunywa pombe wao wanataka kuona madhari na juwa na beach kuongeleya wanyama kama wakipata nafasi kuwaona wenyeji wa mji na wanavyo ishi hawana haja ya pombe.
huko kwao wanakunywa pombe toka wanamiaka 14 japo kuwa sio ruhusa mpaka wafike 18 lakini wanakunywa mpaka wanagarangara wewe leo unasema ati hawarudi tena kisa hakuna pombe wachee wee sema hujuwi kuwapangia mambo ya kufanya sasa wanaboweka ndio maana hawaji tena kwenye hiyo hoteli yako wewe sema unataka wewe hiyo pombe na huyo nguruwe upewe kibali uwe unakunywa na kula nguruwe wako au funga hilo banda lako kafunguwe kilimajaro au tanga usitulete machafu pemba tuliyonayo yanatutosha.
No comments:
Post a Comment