ENZI ZA UNAFIKI WAKE KABLA YA
KURUDI KWA M/MUNGU ALIYEMUUMBA
KIKWETE PINDA
IDDI
WATOTO WA NYERERE WANAENDELEYA NA KAZI YA KUIUWA
ZANZIBARMsione taabu sana kusoma mada hii au mada zangu. Kwa jicho la ghafla, utadhani kama vile ‘jokes’; lakini nakuleteeni mada za Muungano kwa mujibu wa Ilani na Sera za CCM. Yaani yale wanayosema akina JK, Pinda, Seif Ali Iddi, Nyerere, Mwinyi n.k.
Kwa ufupi, katika kuujadili Muungano, Watanganyika wengi wamesahau ‘reality’, wameshahu uhalali wa Muungano, au sheria au haki za Wazanzibari, na wanarukia vitu vya kipuuzi kama hivyo vya kuwa “maduka ya wapemba’ dar au Bara kote, na hususan pale Dar, maarufu kwa jina la Namanga.
Siku moja nilikwenda pale Namanga, DAR. Na niliyahesabu yale maduka yaliyopo pale. Hayazidi kumi, na tuseme ukweli, hayafiki idadi hiyo. Sasa nilijiuliza: Je, maduka haya yanaingiza kiasi gani, tija yake, mpaka ikawa inalingana na thamani ya kupoteza nchi kama Zanzibar? Je, pato linalopatikana hapo linakwenda wapi?Je, Zanzibar inafaidika vipi na sales zinazofanywa hapo n.k.
Leo imekuwa fashion sana, kumsikia kiongozi wa siasa, hasa wa CCM, akitaka kuuhalalisha Muungano, anataja maduka ya Namanga (na anatia sheda na kisra, kuwa ni “maduka ya Wapemba”). Lakini hawataki kusema kuwa wao watawala wameanzisha kamati 49 tokea kuansisiwa kwa Muungano, zote zimekuwa hazina tija, mbali ya tume….nasikia tume zote ni 17. Mbali kile kitu kinachoitwa ‘joint committees”.
Kwa nini hawataki kusema kuwa misaada yote ya mabilioni inayotolewa na mataifa ya kigeni, wanachukua wao Tanganyika, hata ile misaada ya kujenga njia Sumbawanga, kasma ya Zanzibar inachukuliwa na wao. Hawataki kusema akina Samia, Mwinyi, Nyerere, JK, na wenzake kuwa portion ya Zanzibar (quota) ya ajira ndani ya taasisi za Muungano, zile 11 — Wazanzibari hawaingizwi ikiwemo Wizara ya mambo ya nchi za nje.
- Tunapigwa bao, eti wanasema kuwa ‘hatujui kiingereza’. Kuna mtoto mmoja wa Mkereteketwa Zanzibar, alifanyiwa interview ili aaajiriwe foreign affairs, moja ya oral question, alitakiwa aimbe wimbo wa taifa wa TZ. Alishindwa kuimba, maana haujui [sio wake]. Watanganyika walimcheka, na alikosa kazi? Mimi binafsi yangu ukiniuliza, siujui kuuimba.
Wanasahu kusema akina Samia kuwa hata zile nafasi ambazo ni zetu wenyewe, za taasisi za Muungano, zilizopo Zanzibar, pia siku hizi wanazichukua wenyewe. Tujaalie BOT, bank of Tanzania — mpaka mfagiaji, dereva, mpika chai, mpelekaji barua — wote hawa wanatoka Tanganyika. Zile ofisi za united Nations, kadhalika — taabu kuona species ya Mzanzibari. haya akina Samia, Mahadhi, Seif Ali Iddi n.k hawataki kuyasema: wao wamengangania kuwa ‘wapemba’ wanamiliki maduka namanga au maghorofa kariakoo.
Lakini yote haya ni kuwa, kama nilivyotangulia siku za nyuma kusema, bado TZ dunia imewapa uso mzuri. Iko siku Mmarekani, na Mngereza aliyefanya Muungano atasema basi, na itakuwa hakuna ujanja: sisi nina hakika hatuwezi kitu.Tunasema na kupayuka tu. Hawa akina JK wanatamba, sio kuwa wanajua sana, bado dunia imewapa uso mzuri. na hawaujui Muungano hata zero%. Waliofanya Muungano huu 1964 ni marekani, na akisaidiwa na mngereza, na local agent wao alikuwa/walikuwa comrades. Wao ndio waliokuwa wachuuzi kwa Zanzibar kama unavyoona wachuuzi wa dagaa mitaani siku hizi [najua watakasirika, lakini lazima wakubali ukweli]. Nimesema kuwa sisi hatuwezi, kwa sababu vidudu mtu akina comrades bado wapo zanzibar, ni hao akina Samia, Mahadhi, Pereira, Mohammed Seif Khatib na timu yao.
MAHADHI
MOHD SEIF KHATIB
SAMIA
VIBARAKA WA WATANGANYIKA WALIYOLETWA
KUMALIZA NA KUIMEZA
ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment