Pengine ulikuwa hujaiona ripoti hii inayosema kuwa,
Baada ya uchaguzi mkuu wa kugombea urais uliofanyika tarehe 31 Oktoba 2010, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia taasisi, idara na mashirika mbalimbali ya umma ilitumia shilingi 175,639,750/= kwa ajili ya kutoa salamu 217 za pongezi zilizochapishwa katika vyombo mbalimbali vya habari kama magazeti kuanzia tarehe 8 Novemba hadi 8 Decemba 2010.
Nani Alipongezwa?
Kutokana na utafiti uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali la Sikika ambalo hushughulikia utawala bora katika sekta ya afya inaonesha kuwa mengi ya matangazo yalihusiana na kutuma pongezi kwa washindi wa uraisi kwa Tanzania bara na Zanzibar baada ya kuapishwa tarehe 6 November 2010. Jumla ya matangazo ya salamu za pongezi 132 yalitangazwa kumpongeza rais na yaligharimu kiasi cha shilingi 108,239,300 na wakati huo huo kiasi cha shilingi 25,350,500 kilitumika kugharamia matangazo 32 yaliyompongeza raisi na waziri mkuu huku matangazo sita yakitolewa kumpongeza raisi, waziri mkuu na mawaziri na kugharimu kiasi cha shilingi 4,863,000.

Nani aliyelipa Fedha hizo?
Katika utafiti, Sikika imeonyesha jinsi matangazo ya pongezi yalivyotumia fedha za walipa kodi kwa kuwa taasisi zilizotoa matangazo haya yanagharimiwa na serikali. Shirika la Maendeleo ya Taifa ndilo linaloongoza kwa kulipia matangazo nane kwa shilingi milioni 10,185, 900 ili hali Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania MKURATIBA uliopo chini ya ofisi ya Rais unafuata kwa kulipia matangazo 16 kwa shilingi 9,574, 300 na kwa upande mwingine, Mfuko wa hifadhi ya mashirika ya Umma (PPF) inafuatilia kwa kulipia matangazo 12 kwa shilingi milioni 8, 356,700.

Nani aliyepokea kiasi gani?
Utafiti unaonesha kuwa Tanzania Standards Newspapers Ltd iliongoza kwa kulipwa jumla ya kiasi cha shilingi 88, 430,900 huku IPP Media Solutions ikipokea kiasi cha shilingi 31, 575,600 na Mwananchi Communications ikipokea kiasi cha shilingi 31,350, 00. Pia Business Times Limited ilipata shilingi

13, 816,250 huku New Habari Ltd ikilipwa kiasi cha shilingi 10, 075,500 na Free media Ltd wakipata kiasi cha shilingi 1, 512,000.
Matatizo katika sekta ya afya na jinsi ambavyo fedha hizo zingeweza kutumika Katika kuzungumzia swala hili, Mkurugenzi mtendaji wa Sikika bwana Irenei Kiria, amedokeza matatizo yanayoikumba sekta ya afya na nini kingeweza kufanyika kwa kutumia kiasi hiki cha fedha.” Kiasi hiki cha fedha kingeweza kutumika katika miradi ya maendeleo katika afya na elimu. Kwa mfano sekta ya afya inakabiliwa na matatizo mengi kama ukosefu wa rasilimali watu, fedha na madawa” alieleza Sikika imekuwa mstari wa mbele kukumbushia serikali kuondokana na matumizi yasiyo na ulazima kama ilivyo kwa siku za hivi karibuni tulipotayarisha chapisho la matumizi yasiyo ya ulazima kwa kushirikiana na Policy Forum.
Mapendekeo ya utafiti
Katika utafiti huu Sikika imeelezea kwamba, kutuma matangazo ya pongezi kwa viongozi hakumsaidii mlipa kodi ila shirika linalotuma pongezi linawajibika kufanya kazi kwa ufanisi ili kuunufaisha umma wa watanzania kuliko kutumia vibaya fedha za serikali.

Pia wananchi wanashauriwa kutofumba macho pindi wanapogundua kuwa fedha zao zinatumika vibaya na ni jukumu lao pia kuangalia kwa jicho angavu na kushughulikia matatizo yanayowakumba wakati wa utolewaji wa huduma.
Sikika inahimiza serikali kutotumia vibaya fedha za walipa kodi ila zitumike katika njia muafaka na zenye tija kwa jamii. Kwa maneno mengine serikali itekeleze ahadi zake za kupunguza matumizi yasiyokuwa na tija kwa walipa kodi na izingatie kuelekeza fedha hizo katika miradi ya maendeleo na kunufaisha maslai ya wananchi wote kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment