Monday, May 2, 2011

HATA KAMA NYARAKA ZA MUUNGANO ZIKO JE WAZANZIBAR MUNAUTAKA MUUNGANO?

Mzee Moyo, Zito Kabwe na wengine , Wanaposema Hati za Muungano zimepotea haiingii akilini, hati zipo Bungeni na watu wameziona.

Dr. Yussuf mwanasheria Mkuu Zanzibar hajaziona nyaraka hizo, Baraza Mapinduzi hazipo , Muungano umepandikizwa juu ya wazanzibar na sasa wazanzibar washauchoka wala hawana haja nao makubaliyano ya mzee karume na nyerere sio kuimeza zanzibar.

baali kuikuza na kushirikiana ktk bara la africa sasa mzee karume alipokufa ndio mambo yote yakabadilika na ndio mpaka leo wazanzibar wanajiona wako ndani ya nakama maana nchi mbili lakini hakuna msukumo wowote unao onyesha kama hizi ni nchi mbili zenye haki sawa.kila ukiangaliya utakuta kuna kasoro zilizo jaa na mambo mengi kufichwa fichwa.

tuseme ndio hizo nyaraka ziko ndio watu wa zanzibar waendele na muungano?kwa kuwa kuna nyaraka japo kuwa hauna faida nao je wanchi wa zanzibar hawana haki ya kusema au kuchanguwa kuwa nchi yao iwe na muungano au isiwe na muungano hawana haki hii?

watu wote wanajuwa kuwa hata mzee karume hakuwauliza wanchi kama je munataka kujiunga na watanganyika au laa je sasa baada ya miaka 47 munataka kufanya tena mchezo ule ule wakutokuwauliza wanchi kama wanataka au hawataki?mzee moyo asema nyaraka ziko na yeye aliziona basi yeye pia anajuwa ziko wapi mbona hazitowi?

hii ni nchi ya watu wa zanzibar sio nchi ya karume wala nyerere sio nchi ya kikwete wala shein hawa ni viongozi tu na viongozi hujiamuli tu wewe unavyotaka huo sio uwongozi bora kiongozi ni mwenye kuwasikiliza wanchi wake wanapoleta malalamiko na sio kuwatumiya polisi kuwapinga na kuwazima kwa wanayotaka kusema huo sio uwongozi bora huwo ni UDIKTETA.

tumefikia mahali paa ukweli sio kudanganyana na wanchi wako macho wanaona nchi za wenzao zinavyo endeleya na wakiangaliya nchi yao inazidi kudidimiya sasa viongozi wasikilizeni wanchi wanavyotaka na wazanzibar washasema hawataki muungano hawataki muungano ila kwa kufata sheriya basi ipingwe kura ya maoni ya kuchanguwa nani anataka muungano na nani hataki muungano kisha hapo ndio jawabu la misho na lakutatuwa ugomvi uliyoingia na kila moja atakuwa na furaha na tutaendelea kuisha kwa amani na utulivu.

No comments:

Post a Comment