Monday, May 23, 2011

JUHAA MWENGINE AZUKA NA POROJO LAKE KUITETEA TANGANYIKA BILAL





BILAL AKERWA NA CHOKOCHOKO ZA MUUNGANO
MAKAMO wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal anakerwa na watu wanaoleta chokochoko za Muungano na kufanya vitendo vinavyohatarisha amani na utulivu nchini.
Akiivitaja vitendo vya kuchoma moto vibanda vya biashara vya wananchi huko Mkoa wa Kaskazini na kuchana mswada wa marerekisho ya katiba ni ishara ya kuwepo kwa watu wanaoleta chokochoko za Muungano ambao umedumu kwa miaka kadhaa bila ya matatizo yoyote.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Mwera Misufini ikiwa ni moja ya ziara yake ya miradi ya maendeleo na kutoa shukurani kwa wananchi kufanikisha uchaguzi mkuu uliokwenda salama na kukipa ushindi chama chake kwa Unguja na Pemba Makamo amesema mswaada wa katiba hauna lengo la kuhatarisha Muungano au kuvuujunga bali umekuja kwa ajili ya kuuimarisha.
Alisema wenye kuleta chokochoko hawataachiwa na kamwe serikali hazitavumilia kuona baadhi ya watu wanatumia mwanya huo kwa ajili ya kuwadhoofisha wenzao kwa kisingizio cha kuukataa Muungano.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tayari umetimia umri wa miaka 47 sasa ni ishara ya upendo na mshikamano wa wananchi wa pande mbili hizo ambao wamekuwa wakiishi kama ndugu tangu zamani hivyo serikali inataka kuona umoja huo ukiendelea na sio kuvunjika.
Alisema yeye kama makamo wa rais pamoja na mwenzake waziri anayeshungulikia mambo ya muungano Samia Suluhu watahakikisha kwamba matatizo na kero za muungano zinapatiwa ufumbuzi kwa kutumia vikao halali vya pande mbili ili zile kero zilizokuwa hazijapatiwa ufumbuzi zinapatiwa.
“Mimi ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ofisi yangu ndio yenye jukumu la mambo yote ya Muungano na mwenzangu Samia Suluhu huyu hapa tupo kwa ajili ya kuangalia maslahi ya Muungano kwa upande wa Zanzibar basi sisi tutahakikisha kero zote zinapatiwa ufumbuzi” aliongeza kiongozi huyo.
Aidha aliwataka wananchi kuachana na ndoto za kufikiria kuuvunja Muungano kwa wakati huu ambapo dunia ndio kwanza inazidi kufanya harakati za kuungana pamoja na kuunganisha nguvu hivyo sio jambo la busara kwaZanzibarkufikiria suala la kuuvunja muungano wa pande mbili hizo.
“Ulimwengu wa sasa unahitaji umoja kwa sababu umoja ni nguvu hebu angalieni kule ulaya wao wameungana na ipo jumuiya ya ulaya lakini pia kuna bara la Asia kule wameungana hadi bara la Arabuni kwa lengo la kukuza uchumi na kudumisha umoja inakuwaje watanzania tuwe na mawazo ya kukataa kuungana na kuimarisha nguvu zetu pamoja” alisema Dk Bilal.
Dk Bilal alisema ni kweli hivi sasa ndani ya Muungano kumekuwa kukijitokeza kero mbali mbali lakini bado haijawa ni kigezo cha kuutenga ama kuukataa kwani unaweza kuwaumiza wengi.
Alisema hivi sasa sehemu kubwa ya watanzania hasa wazanzibari  wameonekana kuwapo sehemu mbali mbali zaTanzaniana haitakuwa busara kuanza kufikiria kuvunja Muungano.
“Hatutafanya kuandika katiba mpya kwa kuutenga Muunganohilohapana ‘No’ watu wanachoma miswada kuchokonoa Muunganokamahaufai waacheni CCM wao ndio waliowafikisha hapo” alisema Dk. Bilal.
Kinachotakiwa kuona kuwa wananchi wanafaidika na Muungano uliopo na kuuendeleza ili vizazi vijavyo viweze kupata matunda yake kwani dhamira ya viongozi walioanzisha Muungano ilikuwa inatizama zaidi kuunganisha nguvu za pamoja.
Dk. Bilal alisema, serikali ya Muungano na Serikali yaZanzibaritahakikisha kuwa inaandaa mipango mbali mbali ya kuzitatua kero ziliopo kwa haraka ili kuweza kuona wanaenda vizuri.
Alisemahiloserikali hizo italifanyia kazi kutokana na hivi sasa baadhi ya mataifa wameamua kuitumiaZanzibarkujifunza namna ya kuendesha muungano wan chi mbili.Kutokana nahiloDk Bilal, alisema Muungano ambao serikali itahahakikisha inaufanyia kazi ni ule utaoleta nuru kwa wazanzibari wote.
Mapema Wanachama wa Chama hicho katika risalayaowalieleza dhamirayaoya kuona wanashirikiana na serikaliyaokwa kuhakikisha wanadumisha Muungano pamoja na kufanya mabadiliko katika chama kwa kutoa wanachama bora wataokiwezesha Chama kupata ushindi 2015.
Dk. Katika zira hiyo alifuatana na viongozi mbali mbali mbali wa Wilaya hiyo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.Mapema Dk Bilali alitembelea bonde la mbunga la Bumbwisudi  na kuitaka serikali kuongeza nguvu katika sekta ya kilimo.

HUYU jamaa vipi anasema kuwa yeye ni makamo wa raisi wa tanganyika sawa ni watanganyika sio znz hilo la kwanza nakujibu.kisha la pili kasema kama hakuna matatizo yoyote ktk serekali ya muungano ndio tukafika hapa sasa wewe bilal umesoma historia ya znz asili au umesoma historia ya nyerere ya vita vya maji maji kama umesoma ya nyerere sawa sikulaumu.mana umezamishwa kwenye kundi la majuha ila kama umesoma historia ya znz asili ilivyo kuwa na sasa ilivyo basi usingeli inuwa hata mdomo wako.wewe ushakula haramu na ushashiba sasa ukiona haramu uliyonayo inataka kukutoka lazima uwongope ndio unakuja na vitisho vyako vya kunguru wewe umesahau tulikuleya wenyewe hapa znz tukakupa uwaziri kiongozi leo unamdomo wakusema wazanzibar wanachokonowa huku na kule kuvunja muungano na wewe utahakikisha hauvunjiki sio muulize gaddafi,ben ali na mubarouk wanajuwa nini guvu za umma wewe bora nyamaza uwendele kula haramu zako na mvi zishakutoka kama baba yako nyerere na simuda mfupi inshaa allah utakwenda mbele ya haki ukamweleze vizuri allah.unasema mambo ya muungano yako ktk ofisi yako sasa ofisi yako ni kuweka majiwe ya msingi sio maana toka uwe makamo wa raisi wa tanganyika hiyo ndio kazi yako kuwe majiwe ya msingi nyamaza bilal usiwachokoze wazenji haswa ktk mdaa mgumu kama huu njoo tuishi jangombe kwenye nyumba hazina hata taa basi kama ndio kweli muungano mzuri huna moja unalolijuwa wewe na samia ni pikipiki posta to nyinyi kazi yenu nu kuchukuwa barua na kupeleka basi nyamaza usijidai kujifanya kama wewe ni nyerere mpya utakuja kujikuta pabaya sana.hapo uliposimama na kuhutubia angaliya nyuma yako kuna nyumba ya makuti je ndio maendeleyo ya muungano hayo ya miaka 47 unataja ulaya kungana ulaya lazima waungane washazijenga nchi zao na waku mahali pazuri sana znz imejengwa hospital ya mnazi moja toka enzi za sultan mahakam toka enzi hizo kila kitu toka enzi hizo wewe ulikuwa waziri kiongozi hapa znz umefanya nini zaidi ya kuiba na kuwajengea maisha wake zako na watoto wako na familia yako usitake tusema bilal wewe ni juhaa tu kama hao majuwa wengine waliyokuweko huko bungeni nchi inadidimiya nyinyi bado tu muungano sawa sisi tuta vunja muungano na nyinyi bakini tanganyika ndio demokrasi ati hatuwalazimishi muje znz bakini huko huko na watang.

No comments:

Post a Comment